Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa

Makamu wa Rais mama Samia Suluhu ameanza rasmi ziara ya siku 6 mkoani Tanga akianzia wilaya ya Handeni ambako anapewa taarifa ya ujenzi wa jengo la ofisi za halmashauri za wilaya ya Handeni.

Tuko mubashara TBC.

Updates:

Madhumuni ya ziara yangu ni kuangalia miradi ya maendeleo, miradi yote ambayo tumeiahidi kwenye ilani ya uchaguzi, jinsi inavyotekelezwa, fedha zinavyotumika, nani anasimamia nini na ndio maana tupo na waheshimiwa mawaziri hapa, naibu mawaziri lakini pia wenyeji wetu wa huku pamoja na uongozi wetu wa chama kwasababu chama ndio kimetutuma muende mkafanye hili na hili na lile.

Niwashukuru kwamba nimeweza kusimama tumesalimiana, ninalotaka kuwahakikishia ndugu zangu, Tanzania tuko salama, Tanzania tuko salama. Ni kawaida ya mwanadamu kukaguliwa kaguliwa, mara mafua, mara homa mara chochote kile.

Lakini nataka niwaambie kwamba katika wakati muhimu watanzania kushikamana ni wakati huu, kujenga umoja, ni wakati huu. Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje nasi yakatuparaganya vichwa.

Nawaomba wote tushikane kwa umoja kwa mshikamano wetu kama watanzania, tuendelee kuchapa kazi kama sisi tulivyokuja tunachapa kazi, tunaangalia miradi, watu wote shughulikeni na mambo yenu, jengeni Taifa lenu tujenge umoja na mshikamano wetu ili Tanzania yetu iwe Taifa Imara.

Na hichi ndicho kinachotuchongea, uimara wa Taifa letu unaleta maneno mengi.
View attachment 1726532
Leo siku ya pili mbona Tanga ameondoka.
 
..tumezoea bwana mkubwa akifanya ziara huwa anagawa MAHELA kila anapopita.

..sasa mama samia anapiga maneno tu, amesahau kwamba "mkono mtupu haulambwi."
 
Masikio hayafungwi ili yasisikie. Wala pua haizibwi ili isinuse wala macho hayazibwi yasione, bali hufungwa kwa muda wakati wa kulala.
 
hii kitu nilivyoisoma kule TL imeniuma sana , TZ nchi yangu inaenda wapi sijui[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Mbona mzee anaendelea vizuri..fuatilia updates zake,viongozi wa kidini + serikali wameenda kumuona
 
Kazi njema kwake Makamu wa Rais
Anatuandaa kisaikolojia kupokea taarifa nzito. Kidogo kidogo mpaka baada ya wiki mbili tutazoea kujua kuwa mtu anaweza kuwa mgonjwa na baada ya ugonjwa kuna kupona, kutenguka au kufa. Basi tutajumlisha na kutoa mpaka tupate jibu kwa upole.
 
Serikali haramu, Bunge haramu hakuna wanachojali zaidi ya matumbo yao. Hiki kipindi kwa kutumia huo mgongo wataiba sana huo ni mwanzo tu na hakuna wa kuuliza hata kama wasamaria wema watatupenyezea kiasi ambacho hawa wahuni watakuwa wanajichotea.
hii kitu nilivyoisoma kule TL imeniuma sana , TZ nchi yangu inaenda wapi sijui😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Serikali haramu, Bunge haramu hakuna wanachojali zaidi ya matumbo yao. Hiki kipindi kwa kutumia huo mgongo wataiba sana huo ni mwanzo tu na hakuna wa kuuliza hata kama wasamaria wema watatupenyezea kiasi ambacho hawa wahuni watakuwa wanajichotea.
inasikitisha sana
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu ameanza rasmi ziara ya siku 6 mkoani Tanga akianzia wilaya ya Handeni ambako anapewa taarifa ya ujenzi wa jengo la ofisi za halmashauri za wilaya ya Handeni.

Tuko mubashara TBC.

Updates:

Madhumuni ya ziara yangu ni kuangalia miradi ya maendeleo, miradi yote ambayo tumeiahidi kwenye ilani ya uchaguzi, jinsi inavyotekelezwa, fedha zinavyotumika, nani anasimamia nini na ndio maana tupo na waheshimiwa mawaziri hapa, naibu mawaziri lakini pia wenyeji wetu wa huku pamoja na uongozi wetu wa chama kwasababu chama ndio kimetutuma muende mkafanye hili na hili na lile.

Niwashukuru kwamba nimeweza kusimama tumesalimiana, ninalotaka kuwahakikishia ndugu zangu, Tanzania tuko salama, Tanzania tuko salama. Ni kawaida ya mwanadamu kukaguliwa kaguliwa, mara mafua, mara homa mara chochote kile.

Lakini nataka niwaambie kwamba katika wakati muhimu watanzania kushikamana ni wakati huu, kujenga umoja, ni wakati huu. Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje nasi yakatuparaganya vichwa.

Nawaomba wote tushikane kwa umoja kwa mshikamano wetu kama watanzania, tuendelee kuchapa kazi kama sisi tulivyokuja tunachapa kazi, tunaangalia miradi, watu wote shughulikeni na mambo yenu, jengeni Taifa lenu tujenge umoja na mshikamano wetu ili Tanzania yetu iwe Taifa Imara.

Na hichi ndicho kinachotuchongea, uimara wa Taifa letu unaleta maneno mengi.
View attachment 1726532

Itafamika tu...UBAYA UBAYA...Hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom