Mama Samia kuifumua NIDA juu chini, anatafuta bosi ambaye ni chini ya miaka 35

Tukipata Rais mwingine naye atatuambia anaenda kuifumua NIDA.... Kisha tutamshangilia ....anakuja mwingine naye anaifumua...

Kudadeki tuendelee kufumuana tu.
Pale Jiji la Mwanza Wilaya ya Nyamagana, Ofisi nzima ya NIDA ina watumishi wasiofika wanne na kwa siku wanapokea watu wasiopungua mia mbili halafu unataka ufanisi. Ajirini watumishi wa NIDA hadi ngazi ya Mtaa ikiwezekana na maamuzi yawe decentralised!!!
 

Hili la mpaka ngazi za mitaa nijema pia
 
Ahmed Shabiby akiwa na Miaka 21 alikuwa na ma Youtong matano
 
Acha hayo mawazo ww hata maandiko yanasema Bora kijana mwerevu kuliko mzee mpumbavu.
Kuna dogo langu alipewa Kijiji akiwa na 21 hajaoa Wala nn fresh to chuo kaja pewa kata yupo na 26 na hajaoa ishu ni mtu na si umri
 
Vitambulisho vyenyewe ukiangalia ni vurugu tupu
Mtu anashindwa hata kunakili Jina na kuliandika
Ukiona kadi nyingi na assilimia kubwa sana zimekosewa kuandikwa

Matatizo ya kukosea majina kuyaandika yapo kila sehemu kuanzia hospitali, uhamiaji, nida, yaani ubongo wa wengi umejaa maji I swear

Chunguza uliza marafiki na ndugu uone ID zao au phone registration zao ni vurugu tupu

Hela zimepotea bure na zitapotea zaidi
 
Suala si Mkurugenzi Mkuu.
Suala la Utambuzi si la kukimbizana na kutoa Vitambulisho ni kuhakikisha kuna uchujaji wa kina ili kutoa Vitambulisho kwa kila kundi kama waombaji wanavyostahili. Kawia Ufike.
 
Safi sana ondoa wote mafisadi na wakabila wakabila

Uhamiaji wanafanya nini??Hivi ni kukamata Wasomali na Waethiopia wanaoenda Afrika ya Kusini?Wao wangeweza kutoa vitambulisho kwa haki kuliko hao NIDA.
Kabisa kabisa mkuu.Katika taasisi za hovyo na zilizofeli totally ni NIDA.Huko RITA at least kunajikongoja
 
Moja ya taasisi ya Wanakula mishahara ya burebure.

Kwa Sasa wako ofisini wanapiga soga tu.

Umbea kwa kwenda mbele wamekalia meza za serikali.

Hii taasisi ifutwe labda na hizo wakabidhiwe taasisi nyingine ambao wako shapu labda wale NAOT wanaweza ifanya
 
Kabisa kabisa mkuu.Katika taasisi za hovyo na zilizofeli totally ni NIDA.Huko RITA at least kunajikongoja
Mbona taasisi unazotaja zinafanya kazi kwa kushirikiana na NIDA au tatizo ni Mkurugenzi Mkuu?
Kwa sababu wanaohakiki Uraia ni Uhamiaji na umri ni RITA na akoishi mwombaji Serikali ya Mitaa.
 
Fumua mama tena ukiweke na kitengo maalumi cha kufanya maboresho kitaifa maana hilo ni jipu kubwa yani unaweza kukata hadi tamaa kufwatilia technology inakuwa mno tunakoelekea kila kitu ni NIDA sasa mama liangalie hilo mno
 
Utakuta wenyewe wanajitetea kuwa ni suala nyeti kama ni hivyo wapewe kazi JWTZ ambao yunawaamini ili mradi tupate vitambulisho vyetu sio kupotezeana muda tu.
 
Fumua mama tena ukiweke na kitengo maalumi cha kufanya maboresho kitaifa maana hilo ni jipu kubwa yani unaweza kukata hadi tamaa kufwatilia technology inakuwa mno tunakoelekea kila kitu ni NIDA sasa mama liangalie hilo mno
Acha mvua inyeshe tuone panapovuja.
 
Kati ya taasisi takataka ni hii NIDA sijui wanafanya kazi,gani kwa kuanzia mama angefuta NIDA na wafayakazi wote hadi mpika chai wao,waanze upya na hata wabadili jina na kutangaza ajira mpya hao waliopo kazi yao ni kuchezea simu na kupiga story.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…