Mama Samia ni Amir jeshi Mkuu au Amirat Jeshi Mkuu?

Mama Samia ni Amir jeshi Mkuu au Amirat Jeshi Mkuu?

Sisi sio warabu
Natamani kumuona Akivaa gwanda za JWTZ atafananaje?

Kuvaa hilo gwanda sahau Mzee, huyo mama anajitambua,anajiheshimu na anamuogopa Mola wake, unadhani huyo ni kama wale wavaa vimini, vichupi vikionekana na minywele yote ikionekana! Aise hahahahaaaa
 
Wakuu, hii kitu imenichanganya, Marais wa kiume huitwa Amir jeshi mkuu. Msingi wa neno Amir ni neno la kiarabu ambalo lina maana kiongozi.

Kwa kiarabu na uislamu kiongozi wa wa kiume huitwa Amir na wakike huitwaw Amirat .Je kwa mama Samia ataitwa Amir jeshi mkuu au Amirat?

Wazee wa Itifaki naomba ufafanuzi
Suggestion ya Amirat itakuwa ni kuchanganya Kiarabu na Kiswahili, kwa sababu kwa sasa sio kwamba tunaita Amir bali Amiri!! Kimsingi hakuna tofauti na tulivyokopa neno "wazir" na kuwa "waziri" ingawaje kwa Kiarabu, wazir ni mwanaume, na mwanamke anaitwa "wazira" lakini sisi tulivyotohoa neno wazir, likaja kuwa waziri na linatumika kwa wanawake na wanaume.
 
Wakuu, hii kitu imenichanganya, Marais wa kiume huitwa Amir jeshi mkuu. Msingi wa neno Amir ni neno la kiarabu ambalo lina maana kiongozi.

Kwa kiarabu na uislamu kiongozi wa wa kiume huitwa Amir na wakike huitwaw Amirat .Je kwa mama Samia ataitwa Amir jeshi mkuu au Amirat?

Wazee wa Itifaki naomba ufafanuzi
Ni AMIRI siyo AMIR tafadhali
 
Hilo neno Amirat halina maana labda utoe T ambapo litakuwa Amira
Na Amira maana yake ni Princess
Kama tukiangalia neno hilo kiarabu

Kama tuliamua maneno mengi kuwa kiarabu na hili la Amiri jeshi kwa mwanamke litakuwa tofauti kabisa na sio Amira
Hivyo basi inabidi litafutwe jina au title nyingine kabisa kwa mwanamke kwani hili ni geni kabisa kwetu
Rais linatumika kwa wote ila la Amiri jeshi lingekuwa tofauti
 
indeed we are focusing on very minimal matters , this shows the way we are not serious at all, one researcher used to say that the quality of voters we have is the quality of leaders we have
 
Emiir = Amiri
Limetoholewa kutoka kwenye kiarabu kama lilivyo, vile Tanzania haitumii lugha ya kiarabu.
Itabaki Amiri jeshi mkuu
 
Jamani neno mfalme nalo ni kutoka lugha nyingine ambayo niya kibantu,kiarabu ni maalik kama ni mwanamume na maalkiya ni mtawala wa kike.itoshe tu tuelewe kuwa kwa kiswahili safi ni mfalme kwa kiingereza king, kuna namna nyingi za kufafanua vyeo hivi lakini pia neno sultan ni la kiarabu pia lenye maana ileile ya maalik na ndilo jina ambalo wazungu wanapenda kulitumia zaidi wanapotaka kuelezea juu ya mfalme kwa kiarabu,wao wazungu humwita sultan
 
Kwa hiyo Samia tumuite vipi?
Jamani neno mfalme nalo ni kutoka lugha nyingine ambayo niya kibantu,kiarabu ni maalik kama ni mwanamume na maalkiya ni mtawala wa kike.itoshe tu tuelewe kuwa kwa kiswahili safi ni mfalme kwa kiingereza king,kuna namna nyingi za kufafanua vyeo hivi lakini pia neno sultan ni la kiarabu pia lenye maana ileile ya maalik na ndilo jina ambalo wazungu wanapenda kulitumia zaidi wanapotaka kuelezea juu ya mfalme kwa kiarabu,wao wazungu humwita sultan
 
Hilo neno la kiswahili amiri jeshi mkuu.
La kiarabu Ni amir.
Sisi tunalitumia kwa wote awe mwanamke au mwanamme.

RIP Magufuli,RIP Ben Saanane, RIP Azory Gwanda hii ndiyo maana halisi ya kila nafsi itaonja mauti.
Hili ni jibu sahihi, NI amiri siyo amir.
 
Watu wa itifaki wataweka mambo sawa baada ya kujifunza hapa
Nalog off
 
Wakuu, hii kitu imenichanganya, Marais wa kiume huitwa Amir jeshi mkuu. Msingi wa neno Amir ni neno la kiarabu ambalo lina maana kiongozi.

Kwa kiarabu na uislamu kiongozi wa wa kiume huitwa Amir na wakike huitwaw Amirat .Je kwa mama Samia ataitwa Amir jeshi mkuu au Amirat?

Wazee wa Itifaki naomba ufafanuzi
... Rais Samia akitoa order za kijeshi kwa subordinates wake jeshini kwa lugha ya Kiingereza watamwitikiaje? Yes Sir! Au Yes Madam? Au? Lete jibu.
 
Back
Top Bottom