Mama Samia ni Amir jeshi Mkuu au Amirat Jeshi Mkuu?

Sisi sio warabu
Natamani kumuona Akivaa gwanda za JWTZ atafananaje?

Kuvaa hilo gwanda sahau Mzee, huyo mama anajitambua,anajiheshimu na anamuogopa Mola wake, unadhani huyo ni kama wale wavaa vimini, vichupi vikionekana na minywele yote ikionekana! Aise hahahahaaaa
 
Suggestion ya Amirat itakuwa ni kuchanganya Kiarabu na Kiswahili, kwa sababu kwa sasa sio kwamba tunaita Amir bali Amiri!! Kimsingi hakuna tofauti na tulivyokopa neno "wazir" na kuwa "waziri" ingawaje kwa Kiarabu, wazir ni mwanaume, na mwanamke anaitwa "wazira" lakini sisi tulivyotohoa neno wazir, likaja kuwa waziri na linatumika kwa wanawake na wanaume.
 
Sio watu, sema “watu wa dini ile” wanapenda kudeal na mambo madogo madogo sana

Mkuu kujumuisha hivyo inakua hatutendei wengine haki maana hata Rais mwenyewe hana hizo mambo
 
Ni AMIRI siyo AMIR tafadhali
 
Hilo neno Amirat halina maana labda utoe T ambapo litakuwa Amira
Na Amira maana yake ni Princess
Kama tukiangalia neno hilo kiarabu

Kama tuliamua maneno mengi kuwa kiarabu na hili la Amiri jeshi kwa mwanamke litakuwa tofauti kabisa na sio Amira
Hivyo basi inabidi litafutwe jina au title nyingine kabisa kwa mwanamke kwani hili ni geni kabisa kwetu
Rais linatumika kwa wote ila la Amiri jeshi lingekuwa tofauti
 
indeed we are focusing on very minimal matters , this shows the way we are not serious at all, one researcher used to say that the quality of voters we have is the quality of leaders we have
 
Emiir = Amiri
Limetoholewa kutoka kwenye kiarabu kama lilivyo, vile Tanzania haitumii lugha ya kiarabu.
Itabaki Amiri jeshi mkuu
 
Jamani neno mfalme nalo ni kutoka lugha nyingine ambayo niya kibantu,kiarabu ni maalik kama ni mwanamume na maalkiya ni mtawala wa kike.itoshe tu tuelewe kuwa kwa kiswahili safi ni mfalme kwa kiingereza king, kuna namna nyingi za kufafanua vyeo hivi lakini pia neno sultan ni la kiarabu pia lenye maana ileile ya maalik na ndilo jina ambalo wazungu wanapenda kulitumia zaidi wanapotaka kuelezea juu ya mfalme kwa kiarabu,wao wazungu humwita sultan
 
Kwa hiyo Samia tumuite vipi?
 
Hilo neno la kiswahili amiri jeshi mkuu.
La kiarabu Ni amir.
Sisi tunalitumia kwa wote awe mwanamke au mwanamme.

RIP Magufuli,RIP Ben Saanane, RIP Azory Gwanda hii ndiyo maana halisi ya kila nafsi itaonja mauti.
Hili ni jibu sahihi, NI amiri siyo amir.
 
Watu wa itifaki wataweka mambo sawa baada ya kujifunza hapa
Nalog off
 
... Rais Samia akitoa order za kijeshi kwa subordinates wake jeshini kwa lugha ya Kiingereza watamwitikiaje? Yes Sir! Au Yes Madam? Au? Lete jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…