Nilishangaa na kuona huruma sana unakuta mbaba mtu mzima kabisa lakini lugha yake ya asili hawezi hata kusalimia, japo kidogo wanaotokea mikoani kama Moshi, Mwanza na Kagera hujaribu jaribu lakini wengi wa hapo Dar ni hovyoo kabisa, wamemezwa na mambo ya Uswahilini mpaka wamekua watumwa wasiokua na asili yoyote, mtu hajui lugha yake ya asili na pia uandishi wa Kiswahili ni umagumashi, Kingereza ndio hajui chochote kabisaaaa.
Wanakuambia kuongea Kingereza ni ukoloni, kuongea lugha ya asili ni ushamba, na hata hicho Kiswahili bado anayumba yumba kwenye uandishi. Kile hunishanga, mtuhumiwa akikamatwa kwenye uhalifu wowote hutajwa kabila lake kwenye dodoso, check hii...