Mama Samia Suluhu na Mwigulu Nchemba, huu ni ushauri wangu kwenu nnaoamini wenye manufaa makubwa kwa uchumi wa Tanzania.

Mama Samia Suluhu na Mwigulu Nchemba, huu ni ushauri wangu kwenu nnaoamini wenye manufaa makubwa kwa uchumi wa Tanzania.

Kabla ya kuanza ushauri wangu nachukuwa nafasi jujitambulisha.

Kwa wasionielewa, binafsi nilifanya kazi kwa miaka mingi sana nje ya Tanzania. Kazi zangu zote zilihusu sayansi ya mawasiliano na biashara. Nilipostaafu nje huko, nilirudi nyumbani nikafunguwa kazi za Ushauri wa Kibiashara (Business Consultancy) nayo ikazaa kazi zingine kadhaa ndogo ndogo. Sasa ni nusu Mstaafu (semi retired) na kazi zote nazifanya kutokea nyumbani kwangu.

Ushauri Wangu :

Kwa kuwa Tanzania tumedhamiria na tumeshaamuwa kuukuza uchumi kwa kukaribisha wawekezaji ili wawekeze Tanzania. Hilo ni jambo jema sana.

Ili tupate mafanikio ya haraka kama nchi na wananchi. Naamini mafanikio yoyote ya nchi kwanza ni muhimu sana yaonekane kwa maisha ya wananchi siyo kwenye takwimu tu. Kila mwanachi ni lazima yeye mwenyewe binagsi ayahisi mabadiliko, siyo mpaka zipigwe propaganda za kumuaminisha mwananchi kuwa Tanzania kuna mafanikio. Kama wsle. Ndugu zangu (Waarabu wa kuchovya) ambao ukimuuliza wewe kabila gani? Kukujibu mpaka aanze kwa kuapa "Wallahi mimi Mwarabu" 😂😂😂. Kwa nchi yenye mageuzi ya kweli ya kimaendeleo haitakiwi iwe hivyo hivyo, maendeleo na mafanikio ayahisi mwenyewe mwananchi.

Ni muhimu sana mambo mengibya namna tunavyoyaendesha kwenye uchumi wetu ni lazima tuyabadilishe haraka sana. Kwa kuanzia nashauri tuanze na mawili makubwa lakini ni myepesi sana serikali kuyatekeleza. Yataanza juonesha athari chanya mara moja (positive results).

1) "Peg" Kigingi.

Kwa haraka sana tuiwekee vigingi (peg) Shillingi yetu ili tuifungamanishe na pesa za nje zinazitumika kwa wingi kwenye biashara za kimataifa. Tunaweza juweka vigingi (pegs) kwenye sarafu nyingi tu duniani. Ingawa duniani huko ilizoweleka sana kuweka kigingi kwenye US Dollar peke yake, lakini dunia ya leo na mambo yanavyobadilika kwa haraka, si kazima kuweka kigingi kwenye sarafu (currency) moja tu.

Kwa kufanya hivyo kwenye biashara yetu kwa miaka mingi usoni hakutakuwa na mifumuko (inflation) zabghafla kwa bidhaa zetu kama ilivyo sasa.

Wafanya biashara na serikali wstsweza kupanga bajeti zao za mapato na matumizi kwa ufanisi zaidi.

Tutawavuta wawekezaji wengi wakubwa sana ambao kwa sasa uwekezaji wao wote unadhaminiwa kwa sarafu za nchi wanazowekeza kuwa na vigingi.

Ni vigumu kuwsvuta Tanzania. Wawekezaji wenye mitaji mikubwa kama hatuna dhamana ya uwekezaji wao kubaki na thamani ile ile ndani ya muda wa kurudisha mitaji yao (ROI), ambao mara nyingi huwa kati ya miaka 2 mpaka 5. Na dhamananrahusi ninkuwa nansarafu isyopanda na kushuka, yqani iwe pegged. Mfano, kuna nchi duniani huko leo miaka 40 mpaka 50 sarafu zao na.zingine zimebaki kiwango kile kile (stable).

Wakulima wetu watakuwa na uhakika wa bei za mazao yao wakati wote.

Walaji, wananchi walio wengi, watakuwa na uhakika wa kufanya bajeti nzuri za matumizi yetu kwa kipato chetu.

Sarafu yetu itakuwepo kwenye soko la kimataifa na tunaweza kusafiri nayo na kuibadilisha kwa thamani inayojukina bila tatizo lolote (convertible), siyo kama ilivyo sasa. Mpaka inaitwa *pesa ya madafu".


2) "Same rate taxation on everything".

Kodi zetu za mapato kwa serikali tuzibadili ziwe na kiwango kimoja tu cha kupigia mahesabu ya kodi. Siyo kama ilivyo sasa, kila kitu na namna yake ya mahesabu na vitu vinaongezeka kila siku. Hii ya kodi kuwa na viwango vingi vya namna nyingi tofauti kunafanya mianya ya rushwa iwe mingi sana na wizi wa ujwepaji kodi unaongezeka.

Hayo mawili kwa sasa yanatosha kabisa kuanzia, ni mambo yaliyopo duniani huko.

Mama na Mwigulu huu ni ushauri muhimu sana.

Nawasilisha na nakaribisha maswali.


Hivi kweli dada yangu hii akili nzuri huwaa ndo unaitumia kutetea DP? Ni nini kinakupofusha?
 
Hivi kweli dada yangu hii akili nzuri huwaa ndo unaitumia kutetea DP? Ni nini kinakupofusha?
Unachoongelea nini kuhusu DP World?

Mimi sitetei chochote bali naunga mkono makubaliano yaliyoingiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai.
 
Ahsante bibi mtaalamu wa uchumi wa kiislam mbobezi wakisikia ushauri wako niite mjinga nipo siti ya nyuma huku. Unamjua mwigulu wewe?
 
Unachoongelea nini kuhusu DP World?

Mimi sitetei chochote bali naunga mkono makubaliano yaliyoingiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai.
Ongezea na unatetea pia dini yako islamu
 
Umetoa ushauri mzuri
Ila kwenye kuwa na sarafu imara itumike mbinu gan Ili kuweka vigingi na sarafu yetu isiwe inayumba kama dela
Dhahabu yetu na mali asili tulizonazo Tanzania zinatosha kabisa kuwa ni dhamana ya sarafu, tena siyo kwa kuiwekea vigingi tu bali hata bila vigingi tunaweza kuifanya sarafu yetu ikawa na thamani kubwa kuliko ilivyo sasa na iakawa "convertible" Kimataifa.

Tena bila vigingi tunaweza kuanza kwa haraka sana, tunaweza kuanza na nchi za Afrika mashariki kwa kuiwekea dhamana ya dhahabu ya kutokukushuka thamani Shillingi yetu, na kwa muda mchache sana itajipandisha chati yenyewe na khamia nchi za sadec.

Nawashangaa sana wachumi wetu, uchumi tunao lakini tunaukalia.


Naweza ku-challenge na mchumi yeyote hapa, kuwa Tanzania tunawea kuifanya shillingi yetu iwe pesa ya kibiashara Afrika Mashariki ndani ya miezi mitatu tu. Ni uamuzi tu.
 
Interesting subject...
Binafsi nafikiri hii mipango ya kurudisha wizara ya Mipango..hili liwe sehemu ya agenda...
Kuwe na watu wa mipango na watendaji......

Kuhusu peg...nimeshangaa Sana inflation inatusumbua kisa dollars wakati kumbe tunge peg Kwa Euro ni currency stable zaidi kuliko dollars...
Wazo lako la Ku peg Kwa currency nyingi zaidi ni better...
Na alieharibu utaratibu wa serikali kununua Dhahabu alituuumiza zaidi..
Tuwe na reserve ya Dhahabu ya kutosha Ku offset hizi inflation kila mara zikijitokeza..
kwa dhahabu tuliyonayo Tanzania, tena kwa kununuwa ile ya wachimbaji wadogo tu na kuiweka reserve, tutakuwa hatuna haja hata ya pegging, tutaifanya Tanzania Shilling iwe convertible currency tena kwa kuanzia kwa hapahapa Afrika Mashariki tu, kwengine huko itajipeleka yenyewe Automatically".

Ni very simple, ni kuistabilize rate yetu kwa Afrika Mashariki na kuruhusu Shillingi iweze kutoka mipakani, kwisha kazi.

Tena kimya kimya, kila anaekuja kununuwa vitu Tanzania na pesa zake kama za Kenya, anakuta rate ileile kwa wauza pesa. Akija benki zetu hapa anaikuta labda imebadilika vijisenti tu na money changers.


Nashangaa kwanini hatufanyi hivyo, benki za Afrika zikianza kuitumia shillingi, tutajiingizia pesa za bure kwa commission za transfer charges, na hivi siku hizi tunahamisha pesa kwa njia ya simu, ndiyo kabisa, tukiwa stable, Afrika Mashariki nzima wanaofanya biashara watakuwa wanatumia shillingi zetu tu.
 
Unachoongelea nini kuhusu DP World?

Mimi sitetei chochote bali naunga mkono makubaliano yaliyoingiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai.

And that is where your problem is, hauoni mapungufu kwenye Mkataba? Can this address your common sense/logic/soul and give a proper un influenced answer?

Hauoni cha kuboresha kwenye mkataba?
 
And that is where your problem is, hauoni mapungufu kwenye Mkataba? Can this address your common sense/logic/soul and give a proper un influenced answer?

Hauoni cha kuboresha kwenye mkataba?
Huo mkataba mnaouongolea uko wapi? Mimi sijauona. Au IGA (Intergovernmental Agreement) ndiyo mnauita mkataba?

Hebu nifahamishe tuelimishane kidogo.
 
Baby wangu umeongea point sana leo, and this is why i love you..
 
Back
Top Bottom