Naamini sijakosea kukuita Mwenyekiti mpya wa CCM, leo siku moja kabla ya uthibitisho wako. Naamini utakuwa ndiye tena kwa kura zoote, ni suala la muda tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nikueleze kuwa wako waliokuwa watumishi ndani ya CCM na hasa katika shule zilizokuwa chini ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM ambao wako hoi kimaisha, na wengine wameshakufa ili hali haki zao hawajapata. Wengi hawajipwa haki zao za NSSF, MISHAHARA NA VIINUA MGONGO hadi katika uzee wao.
Hawa nao ni watoto wako kama Mama na Kiongozi katika Chama. Wewe ndiye wakufuta machozi yao na dhiki yao kwani naamini Mungu amekuleta kwa kusudi.
Chonde chonde Mheshiwa Mama Mwenyekiti, wakumbuke watu hawa kwani wametoa mchango wao kwa chama na taifa na sasa wanaugulia kwa njaa na dhiki za maisha ili hali haki zao zinajulikana.