Mama Samia Suluhu wakumbuke watumishi wa CCM wanaoteseka kwa dhiki haswa wale wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM

Naamini sijakosea kukuita Mwenyekiti mpya wa CCM, leo siku moja kabla ya uthibitisho wako. Naamini utakuwa ndiye tena kwa kura zoote, ni suala la muda tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nikueleze kuwa wako waliokuwa watumishi ndani ya CCM na hasa katika shule zilizokuwa chini ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM ambao wako hoi kimaisha, na wengine wameshakufa ili hali haki zao hawajapata. Wengi hawajipwa haki zao za NSSF, MISHAHARA NA VIINUA MGONGO hadi katika uzee wao.

Hawa nao ni watoto wako kama Mama na Kiongozi katika Chama. Wewe ndiye wakufuta machozi yao na dhiki yao kwani naamini Mungu amekuleta kwa kusudi.

Chonde chonde Mheshiwa Mama Mwenyekiti, wakumbuke watu hawa kwani wametoa mchango wao kwa chama na taifa na sasa wanaugulia kwa njaa na dhiki za maisha ili hali haki zao zinajulikana.
Kwani hawa siyo wazalendo?
 
Kwani hawa siyo wazalendo kwa chama chao?
 
Hapa hazungumziwi Raisi ila Mwenyekiti wa ccm ndugu mataga!
Hivi vitega uchumi vilivyoporwa kutoka kwa watanzania, kama viwanja vya michezo, majengo mbali mbali, vilivyojengwa kwa nguvu na kodi za watanzania, havisaidii kutatua hizo kero za hao wazee?
 
Naamini sijakosea kukuita Mwenyekiti mpya wa CCM, leo siku moja kabla ya uthibitisho wako. Naamini utakuwa ndiye tena kwa kura zoote, ni suala la muda tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nikueleze kuwa wako waliokuwa watumishi ndani ya CCM na hasa katika shule zilizokuwa chini ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM ambao wako hoi kimaisha, na wengine wameshakufa ili hali haki zao hawajapata. Wengi hawajipwa haki zao za NSSF, MISHAHARA NA VIINUA MGONGO hadi katika uzee wao.

Hawa nao ni watoto wako kama Mama na Kiongozi katika Chama. Wewe ndiye wakufuta machozi yao na dhiki yao kwani naamini Mungu amekuleta kwa kusudi.

Chonde chonde Mheshiwa Mama Mwenyekiti, wakumbuke watu hawa kwani wametoa mchango wao kwa chama na taifa na sasa wanaugulia kwa njaa na dhiki za maisha ili hali haki zao zinajulikana.
Naamini wewe au aliyekutuma ni moja wapo ya wale walikuwa wananufaika na tozo za mapango ya majengo ya chama ila baada ya kukatiwa ulaji sasa mnakuja na gia hiyo tegeshi.

Wakati mwenyekiti akiwa bado hai kwanini hamjawahi kuwasilisha ombi hilo likashughulikiwa kuliko kuleta hapa kwenye jukwaa la kisiasa tena kwenye itikadi tofauti? Je, utamaduni wenu wa kumaliza masuala ya kichama kwa vikao vyan ndani ulikufa?

Je, mwenyekiti ndio hushughukia kero za malipo na sio katibu mkuu?

Katibu mkuu wenu aliwabana ilivyo mkamwekea NONGWA hadi kumchongea akatolewa kiajabuajabu kwenye nafasi hiyo lakini hakuna lolote mlilolifanya tangu mumwondoe.

Tangu mwezi wa pili hakuna katibu mkuu na tangu tarehe 17 Machi 2021 hakuna mwenyekeiti hivyo mambo yote aliyekuwa anashughulikia ni makamu mwenyekiti.

Mnakoelekea mali zote za chama chenu zitarudi tena kwenye mikono ya wachache wenye fedha au kuporwa. Mlitengezewa utaratibu mzuri wa kujiingizia kipato ili kuepuka utegemezi wa ruzuku na michango toka kwa majiri lakini ubaya wenu ni uchoyo, wizi na ubinafsi ulikithiri hata kuambukiza watendaji wa serikali. Kuna haja gani suala hilo kuletwa hapa wakati makamu mwenyekiti na mweka hazina wa chama chenu alikuwepo? Unafiki mkubwa huo
 
awasaidie kwa pesa za ccm au kwa kodi za watanzania wote?
Kodi za watanzania zilishatumika kujenga viwanja vya michezo na majengo ya maofisi na mengine yanayotumika kwa shughuli za biashara. Watumie hizo pesa kutoka kwenye hivyo vitega uchumi kutatua kero za hao wazee. Ifike mahala rasilimali hizi zirudishwe serikalini kwa wananchi, vyama vyote vijitegemee.
 
Naamini sijakosea kukuita Mwenyekiti mpya wa CCM, leo siku moja kabla ya uthibitisho wako. Naamini utakuwa ndiye tena kwa kura zoote, ni suala la muda tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nikueleze kuwa wako waliokuwa watumishi ndani ya CCM na hasa katika shule zilizokuwa chini ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM ambao wako hoi kimaisha, na wengine wameshakufa ili hali haki zao hawajapata. Wengi hawajipwa haki zao za NSSF, MISHAHARA NA VIINUA MGONGO hadi katika uzee wao.

Hawa nao ni watoto wako kama Mama na Kiongozi katika Chama. Wewe ndiye wakufuta machozi yao na dhiki yao kwani naamini Mungu amekuleta kwa kusudi.

Chonde chonde Mheshiwa Mama Mwenyekiti, wakumbuke watu hawa kwani wametoa mchango wao kwa chama na taifa na sasa wanaugulia kwa njaa na dhiki za maisha ili hali haki zao zinajulikana.
Waachane na huo mfumo wa zamani wa kiujamaa. Ushapitwa na wakati.... Hayo ni mambo ya China na North Korea.
 
Back
Top Bottom