Hata kama uongozi mtamu, kwa stahili hii - Ningekua mimi ningerudisha mpira kwa kipa.
Uongozi umeishatiwa doa..na vile ni mama, sidhani kama atatoka salama kiafya.
Sema mama naye jamani, hii shida alijitakia mwenyewe,achana akome:
1.Wizi uchaguzi serikali za mitaa mwaka jana - Alisupport kabisaa
2.Utekaji na upoteaji wa waziwazi.Bora hata Kikwete kipindi cha mgomo wa madaktari, yule Dr.kiongozi wao, walimjeruhi..lakini hawakuua - Ulimboka.Yupo anaendelea na mishe zake.
Magufuli alistua kwa Lissu - hakufa, BenSanane ndo hakurudi kabisa..
List ya mama ni wengi sana, tena wengine watu ambao hawana madhara kabisa, mtu kama yule Kijana Soka..hivi kweli,??Mzee Kibao,Polepole, Yule dogo aliyechana picha, Mdude...yaani watu wa chini kabisa au wasiweza kuwa wapinzani wa kweli...Polepole kidogo tu..Mama either alijisahau, alidanganywa, UKISHAURIWA JIONGEZE....au alifikiri Urais ni kama Umungu vile, kwa karne hii sio kivile.
3.Wizi wa waziwazi uchaguzi mkuu, uonevu, maneno ya kejeli.
4.Ugomvi wake ni CCM wenzake.Aliwapiga chenga la macho.
Nashauri ndugu zake wa karibu wamsaidie na wawe karibu naye, wampe ukweli - hao ndo watu wake kwenye shida na raha.Akijiaminisha washauri wake - watamdidimiza halafu wao watakaa pembeni.Kama sasa anavyosurubiwa - hawezi waona, wapo kwenye viyoyozi tu.
5.Kwa mazingira yalivyo, reaction baada ya matokeo, kuna vitu angepiga chinj.Mfano kwa jinsi hali ya ajira zilivyo ngumu, vijana wenye ajira za hovyohovyo walivozagaa halafa anateua au kufanya mazingira ya ndugu zake wa karibu kupata vitengo nyeti..ni kujitafutia lawama tu.Hivi yule Wanu kweli kwa siasa za MAN to MAN..za jukwaani bila kubebwa, na figisu ambatanishi angeweza toboa hata kuwa DIWANI kweli???
Mama kayazua..sasa anakula matunda.Awe makini akiendelea kujitangaza kama chura kiziwi..atapata tabu sana.