JITU BANDIA
JF-Expert Member
- Feb 5, 2023
- 2,868
- 6,453
NAKAZIAMkuu picha ya Mama akicheza kigodoro inahusu ili tuamini zaidi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NAKAZIAMkuu picha ya Mama akicheza kigodoro inahusu ili tuamini zaidi
Mliodhani Robert Heriel Mtibeli anamzungumzia mama yake mmeendaa 😂😂😂👍
Hiiiiiiiii bhagsehiiii
🙊🙈😅😅😅kwahiyo mwanangu umetuita vilaza sio?
Robert Heriel Mtibeli Je Mama yako akienda kukata kigodoro akilipwa hiyo hela si anananua chakula ili ule ushibe ?😎
[emoji847][emoji847][emoji847]Ugali nakula lakini kushiba nitashibaje wakati kila nikila filamu zake akicheza zinapita kichwani mwangu
Khanga moko...ndembendembe....
Nenda kwa mjomba mwambie kuhusu dada yake pengine anaweza msikiliza na akabadilika.
Huu nadhan ni ujumbe kwa wazazi wa pwani huko,wana tabia za ajabu sana
Swali. Jadili dhima ya Mwandishi huyu kwa kurasa zisizo pungua mbili. Enzi hizo ukipata C ya Kiswahili basi wewe ni bonge la mtaa la mtaalam.
Kaka video iko wapi.!?MAMA SASA NIMEKUA, ACHA KUCHEZA VIGODORO HUKU UNATIKIZA MAKALIO.
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli
Nimechoka. Acha niseme tuu. Niwe huru. Mama gani huyu, Bora kutokuwa na mama kuliko kuwa na Mama wa hovyo kama mama huyu. Oooh! Mama ni Mama, sijui Taikon unalaana, mmelogwa ninyi sio bure.
Ni bora niwe na laana kuliko kuwa na Mama kama huyu.
Bora angekufa, au angekuwa kichaa ningeshukuru Mungu. Sijui kwa nini Mungu alinipa Mama wa hovyo kama huyu. Natamani siku moja niambiwe huyu sio mama yako. Nitafurahi sana.
Hakuna jambo baya duniani kama kuzaliwa na limama lichawi au Mama wa aina ya huyu wangu. Mama wa hovyo.
Najua Watu humu ni wanafiki, hawawezi kusema mambo bayana. Lakini mimi nitasema.
Unafikiri mimi najisikiaje kumuona Mama yangu akicheza kigodoro huku akikata mauno na kutikiza matako bila haya, najisikiaje? Ati huyu ndio Mama yangu. Haki ya nani ninabahati mbaya mno.
Mama anacheza chura huku akivua nguo mpaka nguo za ndani zaonekana. Inafikia hatua anabambiwa mpaka na vijana wadogo ati ndio raha ya kigodoro. Kigodoro gani, Upumbavu tuu.
Yaani Washikaji zangu wa kijiweni wamkamatie Mama yangu kwenye vigoma na vigodoro alafu ninyi muone nina Mama. Mama gani? Upuuzi tuu.
Najua na huwezi kunilaani kwa chochote na siwezi na sitokuja kukuheshimu. Kwanza matendo yako yenyewe yalishanilaani kitambo sana. Mimi wakuona aibu zako? Mimi wakuona uhuni wako? Mimi wakuona uchafu wako? Mimi huyu nione mpaka nguo zako za ndani alafu unitishie Laana kweli? Hivi utanilaani mara ngapi zaidi ya mambo hayo wewe mama wa hovyo?.
Nimechoka kutiwa aibu! Unafikiri ninajisikia unavyobadilisha Wanaume, najisikiaje? Najua hujali na ndio maana hata mimi sitajali kukutolea maneno ya hivyo. Siwezi kuwa na heshima na busara kwa Mama Mpumbavu ati kwa kile kiitwacho heshima ya Wazazi.
Heshima ya wazazi ni kuzaa? Mbona hata wanyama Wanazaa, panya anazaa, mbwa anazaa, nguruwe, mbuzi mee wote Wanazaa. Heshima yao ni kuzaa nakuuliza?
Kuzaa ni silika ya kiumbe. Haihusiani na heshima. Heshima inajengwa na malezi na makuzi. Tabia njema na utu wema ndio huleta heshima.
Sasa wewe umenizaa au nimekuzaa alafu hapohapo unadai heshima ambayo haikustahili.
Mimi sio mwanao nilishakuambiaga. Nawe sio Mama yangu hilo unalijua. Mimi siwezi kuwa na Mama kama wewe. Na wewe huwezi kuwa na mtoto kama mimi.
Lazima nifanye uchunguzi kuwa huenda siku unajifungua ulibadlishiwa mtoto. Lazima nifuatilie mpaka nitajua ukweli.
Mama gani? Hovyo kabisa!
Najua kuna wamama wa hovyo kama wewe maelfu kwa maelfu Duniani. Unganeni nyote mniombee dua mbaya ili nipatwe na mabaya. Lakini kwa vile Mungu hasikilizi Watu wa hovyo mtagongana mwamba.
Mimi sio mwanao. Tayari nimekua, vigodoro vyako vimenidhalilisha vyakutosha.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Siku ukija hapa Buza kwa Mpalange nijuze. Hasa siku za weekend kama leo Jumamosi. Utajionea kila kitu bayana.Kaka video iko wapi.!?
Tutaamini vp maneno yako