Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,133
- 12,361
Kwa hiyo mama zao wakiuza juice na mboga mboga ndio maisha ya wasanii yanakuwa magumu?Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .
Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.
Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.
This industry is all about shit.
Hata kama ni maisha magumu, si ni ya mama zao?Kwahiyo kuuza mboga mboga na juice ndio ugumu was maisha kwa tafsiri Yako sio!!?
Kwani wewe tafsiri ya maisha magumu na rahisi ni ipi!!?
Wewe naona ndio una matatizo man!
Yaaani inasaidia sana.Na inampa afya ya akili kukaa bila kazi sio vizuri
Hatari !Halafu unakuta àna mabody guards anawalipa kumlinda, kwanini asimpe màma yàke hela?
Huu ni upunguani ndo maana wanalaaniwa na kuanza kusaga wenzao kama huyo martha.
Una uhakika huyo mama anaokota makopo?Kipato cha mtoto kinaamua mama au mzazi afanye kazi gani.
Sio asifanye kazi bali afanye kazi gani kulingana na kipato cha mtoto wake.
Mama kakusomesha kwa kuokota makopo. Umefanikiwa na unapesa unamuacha aendelee kufanya kazi yake ya kuokota makopo, kisa ana uzoefu nayo?
Upumbavu mkubwa!
Ukiwa na pesa harafu hauna ubunifu hata wa kutafutia mama yako aina ya kazi/biashara, hiyo sio pesa halali.
Kama umesoma kwa utulivu usingeuliza hilo swali.Una uhakika huyo mama anaokota makopo?
Hapana Kuna kazi mara mbili ikiwa Mungu amekubarikia wewe let's say umekuwa C.E.O wa kampuni kubwa unalipwa vzr mamako na babako walikusomesha Kwa kuokota machupa... Kuuza Genge na kazi nyengine ndogondogo tunategemea ukivuka daraja uvuke na ulikuwa nao ulipokuwa kwenye shida .... Wafanye kazi lkn kidogo zenye kuwapumzisha na staha....Mbona kawaida Mzee,wajitafutia utaomba watoto mpaka lini au ww unataka wakajiuze.
Umiza kichwa kuhusu maisha yakoWasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .
Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.
Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.
This industry is all about shit.
hahahahahahahahahahaahMapema yote hii umeamka na maisha ya Watu kichwani mwako? Sidhani kama Leo utapata nafasi ya kutafakari maisha yako na hatima ya familia yako!
Kuna wazazi huwa hawapendi kuwa wategemezi hata we uwe na mishe zako unamtumia pesa bado utamkuta anafanya biashara zake ambazo we unaona zinamuumiza ila ye ameshazoea na anaona anatengeneza pesa inayokidhi mahitaji yake bila kukutegemea, siku ukiona kakuomba pesa ujue hali ngumu kweli unatakiwa ujiongeze uitume hata ndani ya sekunde 1.
Kiuhalisia maisha ni magumu sana mtu akikutegemea kwa 100% kuna muda unaweza kukwama, juzi kati nilikua na angalia clip flan za hawa truckers wa USA nikaona kuna mzee kazeeka sana bado anaendesha malori anasema udereva kanza 1972 hadi leo bado anaendesha gari za mizigo ila kibongo bongo utakuta huyo mzee mwenye umri kama wake hafanyi kazi anasumbua watoto hata kama afya yake ni nzuri.
Kuwa tegemezi ni chanzo cha ongezeko la umaskini kila mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kile anachoweza.