Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .

Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.

Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.


This industry is all about shit.
Kwa hiyo mama zao wakiuza juice na mboga mboga ndio maisha ya wasanii yanakuwa magumu?

Au mtu akiwa msanii inatakiwa mama yake auze nini, magari?
 
Kwahiyo kuuza mboga mboga na juice ndio ugumu was maisha kwa tafsiri Yako sio!!?

Kwani wewe tafsiri ya maisha magumu na rahisi ni ipi!!?

Wewe naona ndio una matatizo man!
Hata kama ni maisha magumu, si ni ya mama zao?

Kwa hiyo wawalazimishe mama zao nao wawe wasanii?

Unaweza kumpangia maisha mkeo tu, siyo mama yako.
 
Ndo shida ya Utajiri "Mweusi" lazima mmoja kwenye familia yako ateseke!
 
...
 

Attachments

  • Screenshot_20241102-135058.png
    Screenshot_20241102-135058.png
    411.3 KB · Views: 1
Inawezakana wanatunzwa vizuri lakini sisi wenye mama zetu wanyakyusa tunawajua ni watata na wanapenda kujishughulisha ata kama anapata kila kitu na ukimforce aache shughuli zake atakwambia usiletee tena vipesa vyako yaan wana jeuri sijui ya dunia gani
 
Kipato cha mtoto kinaamua mama au mzazi afanye kazi gani.
Sio asifanye kazi bali afanye kazi gani kulingana na kipato cha mtoto wake.

Mama kakusomesha kwa kuokota makopo. Umefanikiwa na unapesa unamuacha aendelee kufanya kazi yake ya kuokota makopo, kisa ana uzoefu nayo?
Upumbavu mkubwa!
Ukiwa na pesa harafu hauna ubunifu hata wa kutafutia mama yako aina ya kazi/biashara, hiyo sio pesa halali.
Una uhakika huyo mama anaokota makopo?
 
Mbona kawaida Mzee,wajitafutia utaomba watoto mpaka lini au ww unataka wakajiuze.
Hapana Kuna kazi mara mbili ikiwa Mungu amekubarikia wewe let's say umekuwa C.E.O wa kampuni kubwa unalipwa vzr mamako na babako walikusomesha Kwa kuokota machupa... Kuuza Genge na kazi nyengine ndogondogo tunategemea ukivuka daraja uvuke na ulikuwa nao ulipokuwa kwenye shida .... Wafanye kazi lkn kidogo zenye kuwapumzisha na staha....
 
Bora muuza mboga mboga, ila muokota makopo anaweza kuwa mwehu ama akili zisiwe sawa kabisa

Siwezi kuwa na kipato cha uhakika halafu nikaruhusu mama Yangu akaokota makopo, aingie majalalani afungue makopo yenye mikojo eti kisa anatafuta... UONGO😭😭😭

siku ya msiba CV yake inasomwaje?😭😭😭
 
Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .

Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.

Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.


This industry is all about shit.
Umiza kichwa kuhusu maisha yako
 
Wazazi lazima wafanye kazi wangali Bado na nguvu. Maisha ya mtoto siyo ya mzazi. Kila mmoja ana maisha yake. Mwenye uhitaji wa lazima wa kuhitaji msaada Kwa mwenzake atafuata utaratibu
 
Kuna wazazi huwa hawapendi kuwa wategemezi hata we uwe na mishe zako unamtumia pesa bado utamkuta anafanya biashara zake ambazo we unaona zinamuumiza ila ye ameshazoea na anaona anatengeneza pesa inayokidhi mahitaji yake bila kukutegemea, siku ukiona kakuomba pesa ujue hali ngumu kweli unatakiwa ujiongeze uitume hata ndani ya sekunde 1.

Kiuhalisia maisha ni magumu sana mtu akikutegemea kwa 100% kuna muda unaweza kukwama, juzi kati nilikua na angalia clip flan za hawa truckers wa USA nikaona kuna mzee kazeeka sana bado anaendesha malori anasema udereva kanza 1972 hadi leo bado anaendesha gari za mizigo ila kibongo bongo utakuta huyo mzee mwenye umri kama wake hafanyi kazi anasumbua watoto hata kama afya yake ni nzuri.

Kuwa tegemezi ni chanzo cha ongezeko la umaskini kila mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kile anachoweza.

Vipi kuhusu uboreshwaji wa Biashara? Kila mtu anapenda upgrade; ama?
 
Mbona ni maisha ya kawaida ya kiTanzania , ulitak aache asubr tuu apew wakt watoto nao wanasak future zAo
 
Back
Top Bottom