Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .

Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.

Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.


This industry is all about shit.
 
Namtumia hii thread asome
 
Kuna wazazi huwa hawapendi kuwa wategemezi hata we uwe na mishe zako unamtumia pesa bado utamkuta anafanya biashara zake ambazo we unaona zinamuumiza ila ye ameshazoea na anaona anatengeneza pesa inayokidhi mahitaji yake bila kukutegemea, siku ukiona kakuomba pesa ujue hali ngumu kweli unatakiwa ujiongeze uitume hata ndani ya sekunde 1.

Kiuhalisia maisha ni magumu sana mtu akikutegemea kwa 100% kuna muda unaweza kukwama, juzi kati nilikua na angalia clip flan za hawa truckers wa USA nikaona kuna mzee kazeeka sana bado anaendesha malori anasema udereva kanza 1972 hadi leo bado anaendesha gari za mizigo ila kibongo bongo utakuta huyo mzee mwenye umri kama wake hafanyi kazi anasumbua watoto hata kama afya yake ni nzuri.

Kuwa tegemezi ni chanzo cha ongezeko la umaskini kila mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kile anachoweza.
 
Humu jamii forum ni matajiri Sana,, usidharau mboga mboga... Nalima mboga mboga eneo ni heka na nusu unazijua Chinese wewe, Kuna msusa zile sukuma wiki matembele na bamia kwa siku nafunga hesabu inayoelewka ... Acha hao kina mama wafanye kazi!!!! Zaidi watoto wao wawaboreshee manzingira wauze mboga kwa level kubwa zaidi ya hapo.v
 
Ulitaka wakae bila kufanya kazi halafu wale nini? Watoto wao warithi nini?
Hata kama mtoto wako ni tajiri kiasi gani kufanya kazi ni lazima.
Kipato cha mtoto kinaamua mama au mzazi afanye kazi gani.
Sio asifanye kazi bali afanye kazi gani kulingana na kipato cha mtoto wake.

Mama kakusomesha kwa kuokota makopo. Umefanikiwa na unapesa unamuacha aendelee kufanya kazi yake ya kuokota makopo, kisa ana uzoefu nayo?
Upumbavu mkubwa!
Ukiwa na pesa harafu hauna ubunifu hata wa kutafutia mama yako aina ya kazi/biashara, hiyo sio pesa halali.
 
Back
Top Bottom