Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Mama wa Rayvany anauza mbogamboga na Mama wa Martha anauza Juice. Maisha ya wasanii ni magumu sana

Mapema yote hii umeamka na maisha ya Watu kichwani mwako? Sidhani kama Leo utapa nafasi ya kutafakari maisha yako na hatima ya familia yako!
Wao si ndio wanawake maisha yao tuyajue mitandaoni? Sada endelea na Show Off harafu ukibroke uone kama tutaacha kukusema.

Kama unayaonesha hadharani inakuwaje usitake.kusemwa hadharani?
 
Humu jamii forum ni matajiri Sana,, usidharau mboga mboga... Nalima mboga mboga eneo ni heka na nusu unazijua Chinese wewe, Kuna msusa zile sukuma wiki matembele na bamia kwa siku nafunga hesabu inayoelewka ... Acha hao kina mama wafanye kazi!!!! Zaidi watoto wao wawaboreshee manzingira wauze mboga kwa level kubwa zaidi ya hapo.v
Uko sahihi. Wa kuwaboreshea ni watoto.
Wawawekee mazingira mazuri ya kuuza vitu fresh kulingana na dunia ya sasa.
 
Mama wa Rayvanny ni mlokole . Huwa hataki pesa za mwanae sababu anaamini ni pesa ambazo zimepatikana kwa njia za kishetani na hazina upako ndani yake.

Anauishi mstari wa Biblia unaosema ; "Heri walio maskini wa Roho maana ufalme wa mbinguni ni wao."
 
Hapo umemaliza Mkuu! 👏👏👏
 
Kipato cha mtoto kinaamua mama au mzazi afanye kazi gani.
Sio asifanye kazi bali afanye kazi gani kulingana na kipato cha mtoto wake.

Mama kakusomesha kwa kuokota makopo. Umefanikiwa na unapesa unamuacha aendelee kufanya kazi yake ya kuokota makopo, kisa ana uzoefu nayo?
Upumbavu mkubwa!
Ukiwa na pesa harafu hauna ubunifu hata wa kutafutia mama yako aina ya kazi/biashara, hiyo sio pesa halali.
Kuuza mboga sokoni kuna tatizo gani??
 
Bimkubwa ana watoto wanne wakiume wote tunajiweza. Ila kila siku jioni anapika mikate anauza ambapo faida yake kwa siku ni kama 6000. 6000Tsh ndio faida yake kwa siku pesa ambayo anaiweza kuipata bila kufanya kazi,ila anaskia raha kuifanya ile kazi yake na kuzalisha kipato chake hata kama kidogo.
 
Humu jamii forum ni matajiri Sana,, usidharau mboga mboga... Nalima mboga mboga eneo ni heka na nusu unazijua Chinese wewe, Kuna msusa zile sukuma wiki matembele na bamia kwa siku nafunga hesabu inayoelewka ... Acha hao kina mama wafanye kazi!!!! Zaidi watoto wao wawaboreshee manzingira wauze mboga kwa level kubwa zaidi ya hapo.v
Afu watu hawajui, Bustani za mboga zina hela balaa, nilishawahi fanya,
Ila mie walikua wanakuja bustanini wenyewe walanguzi, pesa nayopata hadi mwenyewe siamini.

Ni biashara nzuri yenye hela hatarii, mchicha, tembele, pitiku, sukuma wiki, mnafu, Chinese, spinach, etc
 
Kuna wazazi huwa hawapendi kuwa wategemezi hata we uwe na mishe zako unamtumia pesa bado utamkuta anafanya biashara zake ambazo we unaona zinamuumiza ila ye ameshazoea na anaona anatengeneza pesa inayokidhi mahitaji yake bila kukutegemea, siku ukiona kakuomba pesa ujue hali ngumu kweli unatakiwa ujiongeze uitume hata ndani ya sekunde 1.

Kiuhalisia maisha ni magumu sana mtu akikutegemea kwa 100% kuna muda unaweza kukwama, juzi kati nilikua na angalia clip flan za hawa truckers wa USA nikaona kuna mzee kazeeka sana bado anaendesha malori anasema udereva kanza 1972 hadi leo bado anaendesha gari za mizigo ila kibongo bongo utakuta huyo mzee mwenye umri kama wake hafanyi kazi anasumbua watoto hata kama afya yake ni nzuri.

Kuwa tegemezi ni chanzo cha ongezeko la umaskini kila mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kile anachoweza.
umenena mkuu
 
Uko sahihi. Wa kuwaboreshea ni watoto.
Wawawekee mazingira mazuri ya kuuza vitu fresh kulingana na dunia ya sasa.
Si lazima mtoto aboreshe, mama anaingiza pesa kila siku hapo hizo pesa zitumike kuboresha na mtoto ampe mama idea na jina lake aliingiza kwenye biashara ya mama mambo yanaenda..... Unajua mboga mboga kufunga faida ya 20000 ni kawaida!!
 
Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .

Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.

Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.

This industry is all about shit.
Si kila mzazi hupenda kumtegemea mwanae akiwa na nguvu.Wengine ni hulka yao kufanya kazi teache hizo mindset
 
Afu watu hawajui, Bustani za mboga zina hela balaa, nilishawahi fanya,
Ila mie walikua wanakuja bustanini wenyewe walanguzi, pesa nayopata hadi mwenyewe siamini.

Ni biashara nzuri yenye hela hatarii, mchicha, tembele, pitiku, sukuma wiki, mnafu, Chinese, spinach, etc
Watu hawaelewi tu... Bustani Ina hela mdogo wangu.,... Wamekalili mpaka wafungue maduka Kodi kubwa wakae kupiga picha hapo. Wakati chinese, spinach ,sukuma wiki unavuna miezi mitatu na ukipanda ni siku 21 tu unaanza kuchukua maokoto.
 
Wasanii wa Tz ukiachana na showoff zao, Ila kiufupi wana maisha magumu Sana .

Mama wa Rayvanny yupo mbeya sokoni anauza Mboga za majani za reja reja.

Na mama yake Martha anaokota machupa na kuuza juice.

This industry is all about shit.
Kufanya kazi ni baraka, kufanya kazi ni lazima

Tangu kuumbwa kwa dunia Mungu alimwamrisha binadamu afanye kazi!

Na ndio maana alimpa Bustani ailime na kuitunza!

Kazi ni lazima haijalishi una pesa ngapi unless una afya isiyo njema au umri mkubwa
 
Kuna wazazi wanapenda kazi ili kulinda identities zao. Kuwapa pesa sio kigezo cha kuacha kazi zao.

Ila kuna wazazi ambao watoto hawajali kabisa kama wapo na pengine wanahitaji ukaribu wao.

Mara nyingi watoto wanakuwa busy hasa na mapenzi ya kutambulika, kuliko kuangalia wametokea wapi.

Diamond hamsahau mama yake na nahisi kama ana tofauti kubwa na wasanii wengi sana
 
Vipi kuhusu baba yake?
 
Watu hawaelewi tu... Bustani Ina hela mdogo wangu.,... Wamekalili mpaka wafungue maduka Kodi kubwa wakae kupiga picha hapo. Wakati chinese, spinach ,sukuma wiki unavuna miezi mitatu na ukipanda ni siku 21 tu unaanza kuchukua maokoto.
Labda wanaidharau jinsi ilivyo kazi enyewe, ila wangejua maokoto yako hapo wasingesema.

Wawaache wamama wa watu wajitafutie pesa zao wenyewe.
 
Humu jamii forum ni matajiri Sana,, usidharau mboga mboga... Nalima mboga mboga eneo ni heka na nusu unazijua Chinese wewe, Kuna msusa zile sukuma wiki matembele na bamia kwa siku nafunga hesabu inayoelewka ... Acha hao kina mama wafanye kazi!!!! Zaidi watoto wao wawaboreshee manzingira wauze mboga kwa level kubwa zaidi ya hapo.v
nafikiri tatizo sio biashara ya mbogamboga shida hawa wasanii wanatabia ya kuigiza maisha na kutengeneza picha flani kwa watu kwamba maisha wameyapatia kumbe sio ualisia jambo ambalo ndio usani wenyewe na watu hawaelewi
 
Back
Top Bottom