Waziri
Dkt. Gwajima D kuna hii familia ya kuitazama inahitaji msaada wa kiuchumi na kijamii. Mama wa watoto nane, Belita Deus, ambaye mumewe katoroka.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Wilaya ya Malinyi, Mkaguzi wa Polisi Michael Rasha, ameguswa na hali ya mama wa watoto nane, Belita Deus (37), ambaye alitorokwa na mumewe kutokana na ugumu wa maisha.
Mkaguzi Rasha, akiwa katika jukumu lake la kutoa elimu katika kijiji na kata ya Kilosa Mpepo, Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, alipokea ujumbe kutoka kwa mama huyo akiomba msaada wa kutafutiwa mumewe ambaye ametoroka na kumtelekeza pamoja na watoto.
Baada ya kupokea wito huo, Rasha alifika nyumbani kwa Belita na kuelezwa changamoto alizonazo baada ya mume wake kumtoroka. Ameeleza kuwa maisha yamekuwa magumu sana na anakabiliwa na tatizo la makazi, kwani anakaa kwenye kibanda alichopewa na msamaria ambaye sasa anakitaka. Pia, amekosa mahitaji muhimu kwa ajili yake na watoto wake na hawezi kuwaendeleza kielimu.
Belita amesema njia pekee inayomfanya aishi ni kufanya vibarua vya kulima na usafi kwenye nyumba za watu ili apate pesa za kusukuma maisha. Mtoto wake mkubwa ana miaka 14 na alitakiwa kuwa darasa la sita, huku mtoto mdogo akiwa na miezi mitano tu.
Mkaguzi Rasha amempatia Belita kilo 20 za unga, mche wa sabuni, na fedha kidogo ya kujikimu ili kumfariji. Hata hivyo, mama huyo anahitaji msaada zaidi kutoka kwa wasamaria wema walioguswa na hali yake.
Picha:
Michael Rasha