Mama yake mpenzi wangu hataki Mgeni kwake baada ya kusikia Mshenga anaenda kupeleka Ujumbe wangu

Mama yake mpenzi wangu hataki Mgeni kwake baada ya kusikia Mshenga anaenda kupeleka Ujumbe wangu

Kasinja jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2017
Posts
1,069
Reaction score
1,958
Nina mpenzi wangu ambaye tumependana kwa miezi 10 sasa, kaja kwetu Msoma kututembelea kutoka kwao Arusha ikiwa ni njia ya kujuana kiundani alikuja akakaa week 1 hotelini

Baada ya kumshawishi aache kazi ili nimuoe, hii ni kutokana na kazi alokuwa anafanya ya counter kwenye Lounge fulani Dar es Salaam, kuona kazi ya namna ile isinge mpendeza Mwanamke anayetakiwa kuwa mke wa mtu, nimamuachisha nikampa millioni 2 na nusu mtaji aanze biashara nyingine alafu nitakuwa namsapoti kwa mambo mengine.

Ndugu zake wawili waliafiki kukubaliana na suala na mipango yangu kumuoa, ila hawakujua kama kaacha kazi. Baadae walipojua hasa ana dada yake ambaye anezalia nyumbani, wakamaind sana kwakuwa ndo alikuwa ana wasapot kwa mambo ya hapa na pale.

Sasa Mpango wa kwenda kwao ukaanza na nakumbuka mwanzoni walikubali ila walivyosikia kaacha kazi wakaja juu kwamba hatutaki Mgeni yeyote hapa hakuna cha mshenga wala nini.

Msichana kanijia anamapendekezo matatu:
Moja: Aende tena kumuomba mama anweleweshe kwa Kina, Maana mama yake kawa Mbogo , na ukizingatia mpenzi wangu katuma watu kadhaa wa Kumbembelezea wakiwapo wajomba na baba mdogo zake mama kagoma hataki jambo hilo mtoto wake kuolewa kuwa ni Upuuzi

Pili: Ama achukue ile 2.5 nimuongezee 5 ifike 3 afungue duka ndo aende kumweleza mama kuwa sikuacha kazi blindly nilikuwa na mpango huu

Tatu: Kasema wakigoma atalazimisha tuoane bila ridhaa ya mzazi


Je, njia ipi ya kumshawish Mama mtu akubali mshenga kufika kwao maana nataka kufuata utaratibu?
 
Mmh Sijaelewa, ila mumwambie mama binti hakuacha kazi ila alifukuzwa kazi.
 
Unawezaje kumpa mtu hela ya mtaji wa biashara ambayo huna wazo nayo.

Nadhani kabla ya kuwa na mtaji mtu anatakiwa kuwa na hilo wazo la biashara.

Nahitimisha kwa kukuita wewe kilaza
 
Wamepanga deal wakupige hela. Hapo inabidi utulie kimya usiende kupeleka mshenga wala nini wasubiri wakuulize wenyewe. Na akikuuliza mbona kimya mwambie nimeona kwenu hamunihitaji najifikiria kama niendelee na mipango ya kukuoa au lah. Utaona kesho yake tu mama mkwe anakuita mpeleke posa
 
Pole sana, cha Muhim chunguza sana dhamira ya Mwanamke huyo isije kuwa wanakuchota

Pili kama mnachumbia jaribuni kuficha financial position zenu au Vyeo
 
Mchumba anapigwa mimba tu mbna hata huyo mshenga ataitwa yeye
 
Usipoteze muda hakuna ndoa hapo ukweni washakukataa unataka uforce upendo kwa kutumia pesa?
 
Pole sana, cha Muhim chunguza sana dhamira ya Mwanamke huyo isije kuwa wanakuchota

Pili kama mnachumbia jaribuni kuficha financial position zenu au Vyeo
Hii ndo principle yangu, until it's permanent. Hatakiwi kujua kazi wala mshahara wangu.
Inaonekana mzee alijimwambafy. Hapo ataombwa mtaji wa mama soon.
Na yeye apotezee tu
 
si ndo fresh endelea kujilia ikiwezekana jaza mimba ilimradi nyie mnapendana...hio budget ya mahari fanyieni mambo vipaumbele
 
Mi nimesoma kichwa habari tu...jibu ni moja tu mpe mimba na mama ake akikuuliza kwanini umempa mimba,mpe tena mimba
 
Back
Top Bottom