Mama yake mpenzi wangu hataki Mgeni kwake baada ya kusikia Mshenga anaenda kupeleka Ujumbe wangu

Mama yake mpenzi wangu hataki Mgeni kwake baada ya kusikia Mshenga anaenda kupeleka Ujumbe wangu

we endelea kuishi nae huko ukweni wapotezee kwa sasa.. endelea kuyapanga maisha yako na mwanamke wako mpaka watakapoanza kuwatafuta wenyewe. ukijipendekeza sana hata kwenye swala la mali watakukomoa.

nakusihi bro uweni usihangaike nao tena, nia yako ya kumwachisha kazi ni njema, hakikisha tu mnayajenga maisha yenu kwa jinsi mnavyotaka nyie na sivyo wanavyotaka ukweni.

huyo mwanamke anakupenda na una uwezo wa kumwambia kitu akakusikiliza. sasa ukikubali kupelekeshwa na watu wa kwao utapoteza cheo chako kwa huyo mwanamke. narudia tena usihangaike na ukweni kwa sasa we jijenge kiuchumi kwanza.

narudia tena kaka, kwa sasa ukweni wape break, wapotezee, jenga maisha na huyo mwanamke.
 
kabla ya kumpa huo mtaji kwanza nakushaur chukua hela kwanza harafu mpe mimba akizaa sasa ndo mpe hela ya mtaji
 
Hapo bila ridhaa, msifanye.....
 
Dalili zote ni unaenda kupigwa pesa hamna mke hapo stuka...kasinja wafwa
 
Nina mpenzi wangu ambaye tumependana kwa miezi 10 sasa, kaja kwetu Msoma kututembelea kutoka kwao Arusha ikiwa ni njia ya kujuana kiundani alikuja akakaa week 1 hotelini

Baada ya kumshawishi aache kazi ili nimuoe, hii ni kutokana na kazi alokuwa anafanya ya counter kwenye Lounge fulani Dar es Salaam, kuona kazi ya namna ile isinge mpendeza Mwanamke anayetakiwa kuwa mke wa mtu, nimamuachisha nikampa millioni 2 na nusu mtaji aanze biashara nyingine alafu nitakuwa namsapoti kwa mambo mengine.

Ndugu zake wawili waliafiki kukubaliana na suala na mipango yangu kumuoa, ila hawakujua kama kaacha kazi. Baadae walipojua hasa ana dada yake ambaye anezalia nyumbani, wakamaind sana kwakuwa ndo alikuwa ana wasapot kwa mambo ya hapa na pale.

Sasa Mpango wa kwenda kwao ukaanza na nakumbuka mwanzoni walikubali ila walivyosikia kaacha kazi wakaja juu kwamba hatutaki Mgeni yeyote hapa hakuna cha mshenga wala nini.

Msichana kanijia anamapendekezo matatu:
Moja: Aende tena kumuomba mama anweleweshe kwa Kina, Maana mama yake kawa Mbogo , na ukizingatia mpenzi wangu katuma watu kadhaa wa Kumbembelezea wakiwapo wajomba na baba mdogo zake mama kagoma hataki jambo hilo mtoto wake kuolewa kuwa ni Upuuzi

Pili: Ama achukue ile 2.5 nimuongezee 5 ifike 3 afungue duka ndo aende kumweleza mama kuwa sikuacha kazi blindly nilikuwa na mpango huu

Tatu: Kasema wakigoma atalazimisha tuoane bila ridhaa ya mzazi


Je, njia ipi ya kumshawish Mama mtu akubali mshenga kufika kwao maana nataka kufuata utaratibu?
Ushauri wa Mr Kind

Nisiseme umeshachemka, ngoja niseme umeteleza kidogo yawezekana ni umri mdogo au kukosa watu wa karibu wa kukushauri au haukutaka kuwashirikisha

Mchumba wako na wewe nyote mmefanya kosa na uwezo wenu wa kufikiri unakaribiana sana

Kitendo cha kuacha kazi kabla ya kuanzisha biashara au kabla ya nyie kuoana ilikuwa si sahihi sana na kitendo cha kumpa mtaji wakati hujulikani kwao hapo tunaita kukurupuka au wadau hapo juu wamesema kujimwambafai. Yaani unataka binti aamini unampeeenda! Unamaheeeela! Ndiomaana amepata ujasiri wa kusema uongeze laki 5 zifike million 3 kana kwamba hizo milion2.5 hazitoshi kufungua biashara!? Watu wanafungua biashara hadi ya elfu 50 sembuse 2.5M!?

Kitu kingine Mama mkwe huyo na hao shemeji zako ni waswahili. Yaani kifupi unaoa uswahilini sasa kama wewe ni wa ushuani jua uko uswahilini kwetu sasa.

Mama mstaarabu hamzuii binti kuolewa kwa namna yoyote ile badala yake kama ameona kasoro kwa kijana, anamsihi binti yake asifanye haraka! Anamshauri nakumshauri nakumshauri!

Binti akionyesha msimamo, Mama hana namna zaidi ya kumruhusu afanye kilicho ndani ya moyo wake lakini kwa tahadhari.

Namna nyingine huwa nikuchelewesha matukio. Kwa mfano, badala ya kwenda na mshenga angeomba uende kwanza peke yako (au na rafiki zako) kwa matembezi ya kawaida wakufahamu kama hujawahi kufika

Unachoweza kufanya ni nini?

Moja, kwa vile umeshampa hela na unampenda, fungueni hiyo biashara na maisha yaendelee (fanya Kama umetoa sadaka tu)

Sitisha issue za mshenga kwanza, endelea na maisha ya zamani kwanza hadi biashara isimame vizuri

Mbili, Kama unahisi pesa zitapotea na biashara ikafa, binti arudi kazini Kama inawezekana na Kama haiwezekani, arudi aishi na mama yake kwanza watizamane usoni miezi kadhaa waone

Tatu, fuata moyo wako unachoona ni sahihi kufanya
 
Back
Top Bottom