CHAPTER 13
ile nimenyanyuka naenda kunywa maji uso kwa uso na NAA tena round hii akiwa kabeba mtoto moyo ulipiga paaaaah kushituka na akili ikanijia fast kuwa inawezekana Naa ndio MAMA SOMOE mwenyewe ambae alikuwa anaongea na mke wa mganga siku ya jana.
Ndani ya mda mfupi nilipatwa na maswali kama yote hivi
nilijiuliza
1. NAA ATAREACT VIPI BAADA YA KUONANA NA MIMI ?
2. LAKINI IMEKUWAJE ANA MTOTO ?
3. MTOTO KAZAA NA NANI ?
4. VIPI KUHUSU SHULE ?
INAENDELEAAAA....
Daaah kuna vitu sikia tu nilipata mshituko sio wa nchi hii kwa mtu wa kawaida hawezi kunielewa nilishtuka vipi ila just imagine unakutana na Ex wako ambae muliachana katika mazingira ambayo sio mazuri kabisa alafu siku ya siku munakutana wewe ukiwa ndo umepigika zaidi yake.
ile kutazamana macho kwa macho ilitufanya sisi wote wawili tushangaane. akaingia ndani ila nikamwambia samahani Naa naomba tuongee kidogo kama hautowaza.
lengo la kutaka kuongea nae kwanza nilitaka kujua yule mtoto wa nani isije kuwa ni mtoto wangu alafu baadae akaja kuwa kiongozi mkubwa maisha wakala watu wengine nijipendekeze mapema ili baadae nikizeeka nile mafao yangu ya uzeeni.
akaingia ndani akatoka nikamuagizia ukitoka ndani rudi na maji ya kunywa mimi nakusubiri tuongee.
akaitikia sawa lakini mda wote alikuwa na hofu hatari. akaingia ndani mtoto yule nadhani alimuachia yule mke wa mganga. mimi na yeye tukasogea sehemu ya mbali kidogo na pale kuna mti fulani hivi.
maongezi yakaanza nikamuuliza za siku nyingi.
akajibu " nzuri tu"
za shule "
"salama pia"
nikabidi sasa nimuulize " za shule nzuri vipi na nakuoana umekuja na mtoto wa kike umri kama miaka miwili kasoro hivi"
Naa alikaa kimya kwa mda bila kunipa jibu lolote lile " baada ya mda sasa ndo akaanza kunipa mkasa mzima yule mtoto ni wa nani ?
aliniambia tu kuwa yule mtoto ni wa yule jamaa wa mbezi mwisho alikuwa namfata kipindi kile dar mwana anaitwa Benjamin.
wakati siku ile nimpandisha gari yeye alirudi mpaka kwao mkoa X na akurudi shule aliamini kuwa Benjamin atakuja tu mkoa x na watakuja dar pamoja maana maisha yake na ya mama yake yalimchosha sana.
yule benjamini alikaa kama mwezi mmoja hivi akaenda mkoa X wakafanya yao na Naa, Naa akapata mimba ya Mtoto wake Somoe.
mzozo ukawa mkubwa kwa sababu mama yake Naa akutaka Benjamin alete huduma za somoe tu baada ya mtoto kuzaliwa alilolitaka mama yake Naa ni Benjamin amuoe Naa kama hataki kuoa basi kesi iende mbele zaidi serikalini.
maana nao alipata mimba wakati bado anasoma kwahiyo Benjamin baada ya kuona hivyo na anaogopa kwenda kunyea debe jamaa akamuoa Naa lakini before ajamuoa ikabidi Benjamin abadilishe dini. jamaa akatoka dini yake ya mwanzo akaamia dini ya kina Naa.
akamchukua Naa na mtoto wake wakaja zao kuishi dar es salaam. maisha yalikuwa magumu sana katika ndoa yao.
nikamuuliza "why sasa haukunitafuta labda ulidhani siwezi kukusaidia au ulinitafsiri kama mtu mbaya kwako"
akajibu " hapana , ali wewe sio mtu mbaya kwangu ila maisha yalinichanganya sana lakini hayakunichanganya mimi tu ila mpaka baba mtoto wangu ambaye aliyekuwa mume wangu yalimchanganya pia alishawahi kuniambia kuwa kuna siku alitamani achukue kila kilicho chake usiku tukiwa tumelala na atutelekeze maana aliisi kama mwanamke mimi nina nuksi hivi"
wakati naa ananieleza maneno ayo mda uo alikuwa anatokwa na machozi tu.
" Doooh, sasa kwanini upo mkoa X mda huu na haupo kwa mume wako Dar es salaam"
" tulishaachanaga zamani alinipa taraka , unajua alibadili dini kwa ajiri ya ndoa lakini ndugu zake baada ya kujua kuwa kabadili dini waliingilia kati na wakataka kumtenga akaona bora aniache tu"
"pole sana ndo maisha Naa yote ya yote mungu ndo mpangaji hauwezi kujua mungu alikuepusha na nini baada ya kuachana na Benjamin"
Naa alilia sana. ikabidi sasa hapa mkoa X unaishi wapi na unafanya mishe gani
akanijibu " bado naishi kwa mama nafanya kazi ya mama ntilie unajua sasa hivi nishakuwa mkubwa na siwezi kumtazama mama tu kama miaka za zamani now, napambana mwenyewe mtoto apate sabuni, chakula na mahitaji mengine maana baba mtu hana habari kabisa na mtoto wake na hata siku mmoja haijawahi kutokea kunipigia simu hata kwa bahati mbaya".
Daaah nilisiktika sana japo kuwa na mimi ni jambazi nilimteka mtoto wa watu ila Benjamin ni jambazi zaidi yangu, na kuanzia siku nikapa sitowalaumu tena wanawake wanao kataa kuwakutanisha watoto zao na baba zangu wana maumivu makubwa sana yanawasumbua na pengine labda akimuona mzazi mwenzie inakuwa kama kidonda kukitia msumali wa moto.
tuliongea ongea mengi sana. tukarudi wote pamoja mpaka pale kwa mganga yeye Naa alikaa kama siku mbili hivi akaondoka zake ilibidi nimwambie mjomba anikopeshe pesa kiasi kadhaa tukifika Dar nitakupa pesa zako alinipa pesa nikampa Naa akaondoka zake.
ostadh baada ya siku kadhaa alikaa sawa mganga akasema kuwa kama tunataka kupata mali za kule shimoni basi kabla ya kwenda shimoni tupite pale kwake kwa ajiri ya kinga.
tuliitikia tutakuja tu lakini nadhani kila mtu ndani ya nafsi yake hakuna aliyetamani kurudi kule shimoni hata kwa bahati mbaya maana sio kwa mauza uza ya kule shimoni.
tukarudi mpaka mjini nafika home tu mimi na uncle mama anakipigia simu ananiitaji niende kwa sister ana mazungumzo na mimi.
nikaingia zangu kuoga nikala kabisa nikadandia gari mpaka keko kwa sister siku hii ilikuwa ni ya kitofauti sana. kwa sababu mama nilimkuta akiwa mnyonge sana kwa kweli hii siku siwezi kuisahau hata kidogo katika maisha yangu alinipa maneno yani acha tu
aliniambia kuwa kwanza anajua kila kitu kama licha ya kufanya kazi sokoni lakini hata pesa ya kujilipia chuo sina ilo la pesa nimepeleka wapi na nimefanyia nini hataki kulijua ila cha muhimu natakiwa kujua kuwa mimi sio mtoto tena ni mtu mzima na nisitarajie hata siku mmoja kama atakuja mtu ataniambia kuwa nishakuwa mkubwa niachane kabisa na matukio ya ajabu ajabu.
lakini pia nimsamehe sana kuna siku alishawahi kuniambia bora nife ili hapumzike yale maneno yalikuwa ni ya hasira tu, ni kweli naweza nikafa na yeye akazaa mtoto wengine lakini ukweli ni kwamba hawezi kuzaa mtoto mkubwa mwenye umri kama wangu atazaa mtoto ambae atatakiwa atunzwe upya wakati mimi ni mtu mzima na kesho kutwa tu anategemea msaada kutoka kwangu.
Mama alichukua bahasha ya kaki akanipa ndani ilikuwa na pesa kiasi fulani hivi akaniambia hiyo ni pesa za ada ya chuo na hostel na matumizi yako mengine itakayo baki hiyo ndo pesa yangu ya mwisho kubwa kukupa kwenye maisha yangu.
ukiichezea na hiyo basi unatakiwa kujua kuwa umechezea teyali maisha yako na sitokuwa na msaada na wewe.
Daaah maneno ya mama yaliniumiza kichwa hatari sana pale lakini pia yaliniumiza kichwa zaidi baada ya sister kunipigia simu baada ya kufika kwa uncle na kuniambia kuwa pesa aliyonipa mama ndo akiba yake yote hata nauli ya kurudi mkoa X anapokaa yeye kampa yeye siku hii niliona love ya mama mzazi niliamini mtu pekee anayetamani kuona nikifanikiwa bila kuniwekea kiwango cha mafanikio ni mama yangu mzazi.
Marafiki wanaweza kuwakatamani nifanikiwe lakini kuna kiwango cha mafanikio wameniwekea nikipitiza tu watachukia
niliapply chuo na nikalipa kila kitu maisha chuo yakaanza.
MWISHO.