CHAPTER 7
marafiki zangu wawili walikuwa wanabet sana
kuna rafiki yangu mmoja akauliza vipi mbona una mawazo sana ikabdi nimwambie tu kilichonitokea
Akaniambia "Daaah wewe MSE#@₹E ni jambazi alafu umeyakanyaga yani umejipiga kisu cha kiuno wewe mwenyewe sasa hapo itabidi tubet tu".
nikamwambia " sasa tunafanyaje nitengenezee mkeka"
akaniuliza " kwani haujui kubet "
nikamwambia " mimi sijui " .
akanitengenezea mikeka miwili mkeka wa kwanza anakitengenezea mikeka miwili mkeka wa kwanza ulikuwa wa elfu 20 mwengine wa elfu 10.
Mkeka wa elfu 20 mapema tu ukachanika. ukabaki wa mkeka wa pili wa elfu 10 nao niliubettia team moja ya kwanza dakika 40 za kwanza tu teyali ilikuwa ishafungwa goal tatu.
mda uo jasho linanitoka ikabidi nizime simu nilale kwanza.
INAENDELEAAA...
lakini sio kulala tu kwanza nilitoa simu yenyewe betri na line zote mbili nikaziweka pembeni.
nikaona acha nitie line mmoja nilikuwa na salio kama la buku lakini sijajiunga nimpigie Cosmas. mwanangu wa kule Sinza.
Sijui mawazo au mapepe ya usingizi. nilitaka kununua mda wa maongezi wa mitandao yote kwa mfano dakika za AIRTEL KWENDA MITANDAO MINGINE si nikakosea kununua muda wa maongezi kwenye simu yangu nikajikuta nishajiunga midakika kibao ya buku ya AIRTEL KWENDA AIRTEL alafu kwenye simu yangu namba ya airtel zipo kama mbili hivi.
na niliyetaka kumpigia ni Cosmas yeye anatumia mtandao wa VODACOM
nikapiga simu ( Customer care ).
mtandao husika kuomba kama naweza saidiwa kwa namna moja ama kama vipi wanibadilishie kifurushi au wanirudishie vocha yangu.
Mtu wa customer care akaniuliza bwana Ali
"unaweza rudisha UNGA uliosaga na kuwa MAHINDI ?"
ikabidi nikate simu haraka sana maana niliona jamaa anataka kunichefua nimjibu ovyo wanifungue line. nikaona sio riziki acha nitie line nyingine ambayo nilitumia katika kubet nikatoa battery nikaweka line ile nawasha tu simu nakutana na message ya mkeka wa elfu 10 nao umechanika.
Nb: kutumia pesa ya ada kubeti, hilo ni kosa daraja la kwanza lakini pia
usithubutu kutumia ada unayopewa na mzazi wako kufanya ufuska(ile pesa huwa na laana lile jasho tuliloambiwa tutalikula ndio lipo kwa ile pesa) ukiitumia kinyume na maelekezo kuirudsha n ngumu kama kufika zanzibar kwa miguu
kitendo cha kuchukua hata buku tu kwenye elfu 10 basi ile pesa iliyobaki inakwambia punguza buku nyingine tu si utairudisha utasubiri wewe utateseka sana kuirudisha.
asubuhi ilivyofika tu nikazidi kuchanganyikiwa pesa sina na shule natakiwa niende.
Shule nikaenda kama kawaida watu wanaodaiwa ada wakirudishwa na mimi narudi naenda kuchill ghetto
hapo kumbuka nimevuta kama siku kadhaa hivi nimechelewesha kulipa ada na kuna walimu anamjua sister vizuri tu sasa sikujua kama alimipgia simu akampanga kuwa mdogo wako ajalipa ada .
kuna siku mama akaja Dar es Salaam kumsalimia dada. sasa ikabidi aje shule kujua maendeleo yangu, akaenda shule siku ambayo mimi sijaenda shule. kwa kawaida yangu kipindi hiko nilikuwa shule naenda kwa week mara 3 tu au mara 2
ilikuwa jumatatu , alhamisi na ijumaa siendi shule. mimi kipindi hiko nilikuwa naishi ghetto alafu mama akaja hajanipa taarifa yoyote kama kaja Dar es salaam.
Sasa alhamisi ndo siku aliyoenda shule .akaenda mpaka kwa mwalimu wangu wa darasa.
mwalimu wangu wa darasa akasema nina deni la ada laki laki nne na nusu na deni jengine la pesa ya mitihani mama alichanganyikiwa vibaya sana.
Usiku saa 1 usiku nipo ghetto napigiwa simu na mama akaniuliza uko wapi
nikamjibu "nipo ghetto kurasini huku nasoma"
akaniambia "njoo keko haraka sana"
Nilivyopigiwa simu usiku tu ,nikaingia na hofu machale yakanicheza nikajua tu kwa vile napigiwa simu usiku alafu naambiwa njoo keko uko usalama 4×4 -16 .ikajiandaa fresh mpaka keko
,ile nafika tu mama alinipiga kofi hilo sio la nchi hii.
swali la kwanza " wewe una siku ngapi haujaenda shule na pesa ya ada umepeleka wapi"
nikamwambia " sijaenda jana tu nilikuwa naumwa "
" na pesa ya ada umepeleka wapi"
" ada nimelipa"
"ada haujalipa "
nikamwambia aah nilikuwa nimechelewa tu risiti ipo ghetto kule kulipa na pesa ya mtihani elfu 50 iko wapi ... daah ndo nikashtuka kumbe ukiachana na msala wa ada niliokuwa napambana nao kuna inshu nyingine ya pesa ya mtihani "
"nikamwambia mama nshalipa sijapeleka risiti tu"
mama akaongea sana alinimwagia matusi kama yote hivi yani hii siku ndo niliziona hasira za mama zikoje yani alifoka mpaka ikafikia hatua sasa namuona kama presha imepanda hivi jasho linamtoka anahema juu juu.
yale maneno yote aliyoniambia na matusi juu hayakuniumiza kivile lakini aliposema kauli ya " Bora ufe nipumzke nitazaa mtoto mwengine" daaah hii kauli ilinikata maini vibaya sana.
sister akaingilia kesi akamtuliza mama akaniuliza
" ada umelipa au haujalipa"
na mimi msimamu wangu ni ule ule " ada nimelipa risiti ya bank ipo ghetto kule"
sister akaniambia " Sio kesi nenda ndani kalale kesho asubuhi tunaongezana mpaka uko unaposoma kuifata risiti kisha tutaenda pamoja shule"
Daaah ilikuwa afadhali kwa upande fulani lakini pia sio afadhali siku hiyo sikupata usingizi kabisa ndo niliaza kuelewa ile kauli ya kwanini watu wazima wanasima sipati usingizi.
mpaka inafika saa 11 alfajiri naona kama kausingizi kanakuja kuja hivi.
Saa 1 sister anakuja kuniamsha chai teyali kitu nilichokutana nacho ukimbini sikikutarajia kabisa yani. kumbe ile safari ya kwenda kuchukua risiti sio ya watu watatu yani mimi , sister na mama .
sister alimkodi jamaa fulani hivi mnyanyua vyuma jitu la miraba 12 kifua tako eti tuongozane nae ili nisikimbie njiani.
yule jamaa alikuwa acheki kabisa aliniambia kauli mmoja ya kunitisha " kuwa mdogo wangu uko njiani ukikimbia nikikukamata cha kwanza nakuvunja kiuno mse#€e wewe"
Nikaona sasa SHABANI KAONEKA NIMEYAKANYAGA
ITAENDELEAAAA...