Mama yangu na kaka yangu ni wachoyo sana, wanafunga friji wafanyakazi wasile, lakini ni washika dini sana

Mama yangu na kaka yangu ni wachoyo sana, wanafunga friji wafanyakazi wasile, lakini ni washika dini sana

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Mama yangu anaishi na kaka wa kwanza. Hawa watu ni washika dini sana, lakini ni wachoyo sana wa chakula kiasi kwamba Wamefunga friji na makufuli ili wafanyakazi wasipate nafasi ya kula vyakula kadha wa kadha.

Nimeshawasema kwa tabia yao ya kuwabagua wafanyakazi, lakini hawakomi.

Yaani hadi nashindwa kuelewa hawa watu hata hizo ibada wanazozifanya ni za kazi Gani?

Tuwapende watu wanaotutumikia.
 
Kule kwenye dini wamejificha tu,na ni asilimia kubwa sana ya wanaojifanya wako deep sana na dini ilaukichunguza mambo yao ni ya ajabu na ndiyo yanayosababisha hata watu kupuuza kufuatilia kwenda Makanisani/Misikitini
 
Katika maisha yangu kuna vitu nilivyogundua, wapo watu wanashika dini saana lakini vipo vitu/dhambi za asili zinazowadrive ni ngumu kuviacha hata uwe padree au mchungaji, mfano kiburi, hasira, uchoyo,tamaa,ufuska n.k kama hipohipo tu hata kama ukiwa deep kwenye dini kiasi gani bado huwezi kuviacha, ndio maana makanisani kwetu mpaka wachungaji wanagombana n.k
 
Katika vitu nilivyojisemea enzi za ubachela ni kutokuoa mwanamama aloshika “dini”
Wengi wa walioshika dini mara nyingi tabia zao wameziweka pembeni kwa ajili ya matumizi ya baadae
Kwangu mwanamke bora ni yule niliyemkuta kama ni mchoyo au mnywaji ama vyovyoye ilimradi najua rangi yake ni either nichague kuishi nae au laa ila siyo mshika dini unakua obsessed na maombi/ kunena kwakw lakini siku unaweka ndani unakuta kile ulichokidhania sicho. Ni heri aupate wokovu/aanze kuswali swala 5 akiwa ndani kwangu ila siyo nikamuokote ananena kwa lugha au ana swala 5
 
Wengne wanafungiaga Hadi TV kwenye kabati. Wafanyakazi wasiangalie, chanzo cha yote haya ni umasikini + roho mbaya
Ni kweli umaskini hasa ndio swala. Kwenye hali ya uchumi bembelezi inabidi chakula kiliwe kwa mpango rasmi nyakati za kifungua kinywa, lunch na supper tu. Kuruhusu vyakula vichukuliwe kiholela nyakati zozote itavuruga bajeti.
Ila kwa vitu kama maji ya kunywa ndio changamoto!
 
Kule kwenye dini wamejificha tu,na ni asilimia kubwa sana ya wanaojifanya wako deep sana na dini ilaukichunguza mambo yao ni ya ajabu na ndiyo yanayosababisha hata watu kupuuza kufuatilia kwenda Makanisani/Misikitini
Kwanini hatuna upendo wa dhati?
 
Ni kweli umaskini hasa ndio swala. Kwenye hali ya uchumi bembelezi inabidi chakula kiliwe kwa mpango rasmi nyakati za kifungua kinywa, lunch na supper tu. Kuruhusu vyakula vichukuliwe kiholela nyakati zozote itavuruga bajeti.
Ila kwa vitu kama maji ya kunywa ndio changamoto!
Hapo nyumbani wanaona Bora vyakula vimwagwe kuliko viliwe na wafanyakazi
 
Back
Top Bottom