Mambo 05 ya kujifunza maishani kutoka kwa mitume na manabii wa uongo nchini Tanzania

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
1: Uwe msiri na usiwe unapatikana kirahisi wakati wote au kuwa adimu( do not be too available).
Huwezi kumkuta nabii wa uongo anatembeatembea hovyo au anapatikana kirahisi. Watu wanatafuta kitu adimu sio kinachopatikana kila mahali.

2: Usijibujibu tuhuma. Usiongee au kujitetea unaposhambuliwa maana unawapa maadui points za kukushambulia zaidi.
Hawa mabingwa wanatuhumiwa misikitini,makanisani, baa, sokoni, kwenye mitandao na vyombo vya usafiri nakini wao wako kimya wanapiga pesa tu na kufocus kwenye mambo yao. Mfano kanisa ninaposali kila akisimama muhubiri anawazungumzia hadi kero.

3: Jifunze kutumia wanawake kuendesha mambo yako. Wanawake wengi ni waoga, alafu ni viumbe ambavyo ni rahisi kuvitawala. Hata ukifungua ofisi yenye wanawake wezi, hawawezi kukupiga ufirisike, huwa wanadokoa kwa hofu kuliko vidume.
Pia ukiwasifia huwa hawakubali kushindwa. Pia ni machawa wazuri wenye uwezo mkubwa wa kukuletea mafanikio. Moja ya siri ya mafanikio ya mitume na manabii ni mbinu bora za kucheza na akili za wakina mama. Hata Yesu masponsa wake wakubwa walikuwa wake za watu na wanawake wengi.

4: Kaa mkao wa kitaalam. Muda wote umaintain professional posture. Huwezi kujibrand kuwa wewe ni mtu flani mkubwa alafu unakaa kizembe. Huchani nywele, meno ya njano, shati limepauka, Ukitembea shape inatawanyika hovyo. Jifunze (diplomatic walk). Tembea kimamlaka. Vaa vizuri, jali afya na tumia muda mwingi kuboresha namna unavyoongea.
Hata paulo alionekana kama tajiri hadi Feliki akamuomba rushwa. Hakuwa mzembemzembe alikaa kitaalam.

5: Kuwa jasiri hata kama unaogopa igiza ujasiri. Watu wanapenda kuwa wafuasi wa mtu jasiri anayejiamini.
Hawa jamaa ni majasiri kupitiliza. Kumuaminisha mtu uongo ukiwa muoga au unaongea kimasihara rahisi kukudaka. Viongozi wengi wa dini hasa za mifumo kama Sabato,Katoriki,KKKT na dini kubwa duniani hawajiamini. Maana juu yao kuna watu wanaoweza kuathili maisha yao. Ndio maana wengi hawana mvuto kuliko hata mwinjilisti tu std 7 anayeamini kaitwa na Mungu moja kwa moja. Yesu alivuta watu wengi kwa sababu alijiamini sana na alikuwa na kauli za mamlaka kuliko mtu yeyote israel. Hii kitu hawa wajomba wamecopy vizuri kuliko hata watumishi wa Mungu halali. Na ndio chanzo cha wao kuwa na mvuto ukiacha backup za kafara za kishirikina.

Ni hayo tu...
Niwatakie Sabato njema.
 
Maisha yana usiri sana. Sasa hapo kwenye meno ya njano unawasema watu wa Arusha.
 
Na uijue Biblia kiukweli kweli. Si unakuwa hoya hoya. Na kuijua huko, ujue kuitumia.
 
Hata mtume Mohammad alikua tapel ayejiamini uarabuni nzima..............ndo maana wakamuamini...tapel mudy
Sijui kuhusu utapeli maana hakuna rejea hiyo.
Ila najua kama Yesu na yeye alisaidiwa sana na Mwanamke Khadīja bint Khuwaylid, mwarabu mwenye asili ya kikristo. Alikuwa boss wake baadae mkewe. Ndiye aliyesaidia kifanikisha utume wake kwa kumpeleka kwa Uncle wake Waraqa ibn Naufal aliyemtabiria utume. Huyu Uncle alikuwa mkristo.

Story hii inapatikana kwenye hadithi za Sahih Bukhari.
 
Na uijue Biblia kiukweli kweli. Si unakuwa hoya hoya. Na kuijua huko, ujue kuitumia.
Wanasoma sana. Ila wanachambua cream tu. Ndio maana wanaweza kuhubiri mwaka mzima kila siku maana wanatafuta zile sehemu zinazogusa watu, sio za kuleta ligi na mabishano.
 
Maisha yana usiri sana. Sasa hapo kwenye meno ya njano unawasema watu wa Arusha.
Wale hawana meno ya njano. Wanameno yaliyoungua kwa sababu ya madini kupitiliza kwenye maji yao.
Namaanisha njano matokeo ya uchafu au kukoswa elimu ya kutosha ya kinywa.

Wale ni watu wema, sina ugomvi nao.
 
Kwa hiyo hizi mbinu watu wenye ujasiri wakitumia kuanzisha huduma watatoboa sio...
 
Back
Top Bottom