Mambo 05 ya kujifunza maishani kutoka kwa mitume na manabii wa uongo nchini Tanzania

Mambo 05 ya kujifunza maishani kutoka kwa mitume na manabii wa uongo nchini Tanzania

Hao wote wanabebwa na nguvu ya kafara wanazomtolea shetani ndie uwaletea watu kujaza makanisa Yao.
 
kama mtu anaujasiri wakusema mbele yawatu elfu moja kuwa amefufua misukure na anakuja nao hadi kanisani kuwaonyesha hao waumini wake lakini wengi wakiwa niwanawake

mtuhuyo muacheni apige hela mana kafika kiwango chajuu chauongo nawatu wameamini
 
Sijui kuhusu utapeli maana hakuna rejea hiyo.
Ila najua kama Yesu na yeye alisaidiwa sana na Mwanamke Khadīja bint Khuwaylid, mwarabu mwenye asili ya kikristo. Alikuwa boss wake baadae mkewe. Ndiye aliyesaidia kifanikisha utume wake kwa kumpeleka kwa Uncle wake Waraqa ibn Naufal aliyemtabiria utume. Huyu Uncle alikuwa mkristo.

Story hii inapatikana kwenye hadithi za Sahih Bukhari.
Huu ni uthibitisho uislam ulianzishwa na Wakatoliki ili kuwacontrol waarabu
 
1: Uwe msiri na usiwe unapatikana kirahisi wakati wote au kuwa adimu( do not be too available).
Huwezi kumkuta nabii wa uongo anatembeatembea hovyo au anapatikana kirahisi. Watu wanatafuta kitu adimu sio kinachopatikana kila mahali.

2: Usijibujibu tuhuma. Usiongee au kujitetea unaposhambuliwa maana unawapa maadui points za kukushambulia zaidi.
Hawa mabingwa wanatuhumiwa misikitini,makanisani, baa, sokoni, kwenye mitandao na vyombo vya usafiri nakini wao wako kimya wanapiga pesa tu na kufocus kwenye mambo yao. Mfano kanisa ninaposali kila akisimama muhubiri anawazungumzia hadi kero.

3: Jifunze kutumia wanawake kuendesha mambo yako. Wanawake wengi ni waoga, alafu ni viumbe ambavyo ni rahisi kuvitawala. Hata ukifungua ofisi yenye wanawake wezi, hawawezi kukupiga ufirisike, huwa wanadokoa kwa hofu kuliko vidume.
Pia ukiwasifia huwa hawakubali kushindwa. Pia ni machawa wazuri wenye uwezo mkubwa wa kukuletea mafanikio. Moja ya siri ya mafanikio ya mitume na manabii ni mbinu bora za kucheza na akili za wakina mama. Hata Yesu masponsa wake wakubwa walikuwa wake za watu na wanawake wengi.

4: Kaa mkao wa kitaalam. Muda wote umaintain professional posture. Huwezi kujibrand kuwa wewe ni mtu flani mkubwa alafu unakaa kizembe. Huchani nywele, meno ya njano, shati limepauka, Ukitembea shape inatawanyika hovyo. Jifunze (diplomatic walk). Tembea kimamlaka. Vaa vizuri, jali afya na tumia muda mwingi kuboresha namna unavyoongea.
Hata paulo alionekana kama tajiri hadi Feliki akamuomba rushwa. Hakuwa mzembemzembe alikaa kitaalam.

5: Kuwa jasiri hata kama unaogopa igiza ujasiri. Watu wanapenda kuwa wafuasi wa mtu jasiri anayejiamini.
Hawa jamaa ni majasiri kupitiliza. Kumuaminisha mtu uongo ukiwa muoga au unaongea kimasihara rahisi kukudaka. Viongozi wengi wa dini hasa za mifumo kama Sabato,Katoriki,KKKT na dini kubwa duniani hawajiamini. Maana juu yao kuna watu wanaoweza kuathili maisha yao. Ndio maana wengi hawana mvuto kuliko hata mwinjilisti tu std 7 anayeamini kaitwa na Mungu moja kwa moja. Yesu alivuta watu wengi kwa sababu alijiamini sana na alikuwa na kauli za mamlaka kuliko mtu yeyote israel. Hii kitu hawa wajomba wamecopy vizuri kuliko hata watumishi wa Mungu halali. Na ndio chanzo cha wao kuwa na mvuto ukiacha backup za kafara za kishirikina.

Ni hayo tu...
Niwatakie Sabato njema.
🤣🤣🤣usiondoke,,,,ngoja waje
 
kama mtu anaujasiri wakusema mbele yawatu elfu moja kuwa amefufua misukure na anakuja nao hadi kanisani kuwaonyesha hao waumini wake lakini wengi wakiwa niwanawake

mtuhuyo muacheni apige hela mana kafika kiwango chajuu chauongo nawatu wameamini
Uongo ukiusema kwa ujasiri na ukaupitilizisha (exaggeration), na ukausema kwa kujirudiarudia watu wasiofikiri sana ni rahisi kukuamini. Na hawa ndio wengi kwenye jamii.

Hata Wayahudi walipotaka kumfanyia fujo Paulo huko asia, waliwatafuta watu kama hawa kufanikisha mission yao.
 
Huu ni uthibitisho uislam ulianzishwa na Wakatoliki ili kuwacontrol waarabu
Hakuna uhakika kwa hiyo nadharia. Kwa sababu wakristo waliokuwepo middle east wengi hawakuwa wakatoriki walikuwa ni Jacobian na Nestorian na makao makuu yao yalikuwa iraq, hawa walienda hadi india na mashariki mwa china. Na hawa waliinfluence mambo mengi sana kwenye uislam. Hata misikiti shape yao ilikuwa ndio shape ya makanisa ya hao jamaa.
 
Kwa hiyo hizi mbinu watu wenye ujasiri wakitumia kuanzisha huduma watatoboa sio...
Ukiwa na ujasiri wa roho mtakatifu na ukawa unetumwa na Mungu hakuna wa kukuzuia. Sema wale wajomba kama ni ujasiri wa gizani pia huwa unachuja over time.
Ila ujasiri yote kwa yote ni muhimu sana ili watu wakuamini na kukufuata kama mtatuzi wa mambo yao yanayowasumbua.
 
Mmmmh kuna walakini mahali ebu atoe muongozo
Hakuna walakini. Masponsor wakubwa wa Yesu walikuwa ni wanawake. Ndio maana watu wa kwanza kufuka kaburini walikuwa ni wakina mama. Walimuamini Yesu kuliko hata mitume 12.

Luka 8:3
na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao.
 
Back
Top Bottom