Mambo 10 magumu kwa wanafunzi wa 'short course' wanaosoma VETA Kama huyawezi usiende; tafuta njia nyingine ya kusoma

Mambo 10 magumu kwa wanafunzi wa 'short course' wanaosoma VETA Kama huyawezi usiende; tafuta njia nyingine ya kusoma

pCpCp RICH THINKER

Senior Member
Joined
Apr 5, 2021
Posts
121
Reaction score
103
Una mpango wa kusoma Short Course V.E.T.A ? Na ni mtu mwenye majukumu yako?!
Basi, tambua:

1. Utalazimishwa kuvaa sare. Hauko tayari kuvaa sare mazingira yako ni magumu. Hakuna cha 'bring-bring' wala nini!

2. Utanyoa Kama mtoto, kama mwanafunzi haswaa. Kama unauchebe, uchebe wako utaambiwa 'kakate ndevu' na kama mke wako anaupenda 'mustachi'; rafiki yangu utaambiwa “chagua V.E.T.A ama mkeo”.

3. Usilete habari za 'udigrii', 'u-pHD', uzamili wala u-astashahada. Jifanye hujui, jifanye darasa la saba hata Kama una shahada ya uzamivu. “Don't outshine your teachers”.

4. Utapaswa kujibu Kama madesa ya Mwalimu yanavyo sema na si vinginevyo. Ujuaji hautakiwi, hata kwa mambo unayojua ya mtaa, tulia; ' aliye na kisu ndio anaamua keki aikate vipi'

5. Hutaruhusiwa kufuga rasi, a.k.a 'dread', kunyoa kidugu, kufuga kucha n.k Hiyo ni ishara ya uhuni. Wadada wote wasuke twende kilioni ama wanyoe ama nywele fupi fupi.

6. Utasalimia watu na stafu wote, hata kama unawazidi umri Salam kwa mwanafunzi ni moja tu nayo ni “shikamoo”; usile mambo ya “za saizi!” na salamu unazozijua wewe! Hutaki tafuta chuo chako.

7. Hutaruhusiwa kutumia simu ukiwa darasani. “Simu utazima ukiwa darasani, na ukikamatwa nayo siku utakayoichukua siifahamu!”

8. Utapewa adhabu kama kawaida, kuzibua mifereji kumwagia maji, ikiwezekana kung'oa visiki, ukizingua. Kwa ufupi unaambiwa “ukiingia humu hata kama una pHD; unaiacha getini”

9. Habari za ujuaji na ‘harakati za hovyo’ hazitakiwi kwa sababu “hujalazimishwa kuja V.E.T.A”

10. Ukikiuka kati ya hayo tisa, maana yake uko tayari kufukuzwa hatakama unafadhiliwa na Ofisi ya waziri mkuu
 
Hiyo ya tisa imefanya watu wawe wanaangalia tu mambo hata huku kwenye jamii yani hamna kuuliza ubongo umeendaliwa hivyo toka tunasoma ukijifanya kujua tu unasepa shule yaani sisi bana
 
Ni VETA ya wapi yenye hayo masharti? Ni kweli wanasisitiza nidhamu ila sio kama ulivyowasilisha. Kwa kozi fupi sare yao ni tisheti na ovaroli kama mtu anaingia karakana.

Hayo masharti ya kunyoa ni kwa wanafunzi wa kozi ndefu tena wanaokaa bweni.

Na kuhusu kutokuonesha uewelewa na kiwango cha elimu au ujuzi alionao mtu si kweli kabisa iwe kwa kozi fupi au ndefu.

Kuhusu salamu umetupiga mno hakuna hicho kitu.

Itoshe kusema tu umetupiga hakuna ukweli wa wasilisho lako.
 
Ila hawa jamaa wanapenda sana kunyenyekewa, ukivikuta vile videmu vya pale mapokezi vinaongea kama vile wao ndiyo wana ufunguo wa Mafanikio yako na wanaamini kila anayeenda VETA amepigika na maisha ya mtaani na amefeli maisha kwahiyo wao ndiyo kila kitu katika ukombozi wako.

Yalinikuta miaka kadhaa ya nyuma wakati nafuatilia kozi ya Udereva ila kwa mapokezi yao ikabidi niende kwenye chuo kingine ambacho kina heshimu pesa ya mteja.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Ni upuuzi mtupu kum treat mfanyakz kama bado yuko primary skul
 
Back
Top Bottom