Mambo 10 makubwa ya Rais wa awamu ya tano wa Tanzania

Mambo 10 makubwa ya Rais wa awamu ya tano wa Tanzania

Nakuona ngumbalu katika ubora wako
Huelewi kuwa data ni zao la tafiti?nani alikuambia utafiti ni mpaka uufanye wewe mwenyewe?..Mkuu unakwama wapi?
Mbona umehamaki mkuu mimi nimeuliza maswali ulitakiwa ujibu tu.
 
Ungeenda kwenye website ya CCM ungepata mengi zaidi ya 10 (amani ipo, wafanyabiashara wako poua, watumishi wako vizuri, wakulima wako happy), Uchumi nao unakuwa, mazingira ya kidemokrasia ndiyo poooa kbs.

"tusiwe kama nyumbu, mwanasiasa akikuambia nje kuna giza usiamini"
Hayo ni baadhi hata hivyo
 
Mbona umehamaki mkuu mimi nimeuliza maswali ulitakiwa ujibu tu.
Swali ulilouliza halina uhusiano na nilichoandika ndiyo maana nimekujibu tofauti na ulivyotaka..ulipaswa uishambulie hoja uliyoiona dhaifu kwa kutumia hoja yako uliyoona ina nguvu zaidi
Unaniuliza elimu yangu "so what" ..logically hii ni fallacy "argumentum ad hominem"..na ndiyo tatizo kubwa tullilonalo wengi.
Kama umeichukia hoja onesha ubaya wake kwa hoja na siyo dharau au kejeli kwa mtoa hoja.
 
Tumekuwa Taifa la hovyo hovyo sana! Majitu yanajipendekeza mpaka kero!
Mwalimu Nyerere Hydroelectric Power ni kujipendekeza. Asilimia 70 ya Watanzania kusema rushwa imepungua ni uongo au kujipendekeza?
Barabara ya njia nane inayojengwa ni kujipendekeza?
Elimu bure ni kujipendekeza?
Uboreshwaji wa elimu ni kujipendekeza?...Hivi unaelewa kujipendekeza.
Hoja yako hapo sasa ni ipi?......jenga hoja ya kupinga hayo mambo kumi siyo kusema " Najipendekeza"...ofcourse najipendekeza kuonesha uhalisia kama unavyosemwa na unavyoonekana ..wewe unafanyaje?
 
Sasa ulitaka hayo ayafanye nani wakati hazina anayo yeye na ndo mwenye mamlaka?
Yaani unamsifia mtu kwakua anatimiza wajibu wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumbani kwako ukiwa msanii kiasi hiki basi waweza pachikwa jina - Mzee wa fix kaja kamfungulieni geti.
 
Kwenye ukoo wa walaki wa upareni hakuna kilaza namna hii!
Hiyo ndiyo hoja yako ya msingi au una hoja nyingine?...nawafahamu sana hamuwezi kujenga hoja mnaishia kwenye personal attacks.
Teh..teh..teh....kwani nimeandika masuala ya ukoo hapo?...au hujaielewa post vizuri?...kama umeielewa na hili ndilo jibu uliloona linafaa basi kuna haja ya kukubali kukaa chini na kujifunza kujenga na kubomoa hoja ya mtu " critical thinking and argumentation"..naweza nikakusaidia ukihitaji.
 
Nyumbani kwako ukiwa msanii kiasi hiki basi waweza pachikwa jina - Mzee wa fix kaja kamfungulieni geti.
Ha..ha..haa...kijana jifunze kutofautisha maoni na uhalisia kwanza ndiyo uje kujenga hoja yako hapa.
 
Hiyo ndiyo hoja yako ya msingi au una hoja nyingine?...nawafahamu sana hamuwezi kujenga hoja mnaishia kwenye personal attacks.
Teh..teh..teh....kwani nimeandika masuala ya ukoo hapo?...au hujaielewa post vizuri?...kama umeielewa na hili ndilo jibu uliloona linafaa basi kuna haja ya kukubali kukaa chini na kujifunza kujenga na kubomoa hoja ya mtu " critical thinking and argumentation"..naweza nikakusaidia ukihitaji.
Nimekupuuza kwa propaganda zako dhaifu,nawajua walaki ndio maana nasema itakuwa tu umejiita hivyo ila sio mwana ukoo huo,Walaki wako smart sana upstairs!
 
"3.Uboreshwaji wa Demokrasia pamoja na hali ya kisiasa na uwepo wa vyama vya upinzani Prof Ahmed Mohhidin,mtaalamu wa siasa za kikanda amenukuliwa akisema "ushindani katika siasa Tanzania ni jambo lililozoeleka tangu uchaguzi wa vyama vingi vya kisiasa wa mwaka 1995.Na maandiko lukuki ya wanasayansi wa siasa wamekuwa walionesha licha ya kuwepo kwa uchaguzi zenye ushindani Nchini bado uimara wa demokrasia Nchini Tanzania umeonekana kuwa na nguvu zaidi ukilinganisha na Nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki."

Unadanganya kwa manufaa ya nani?Eti kwamba demokrasia imeimarika awamu hii,huu ni uongo wa mchana kabisa!Ungeweka na hapa utafiti wako,Tanzania imekuwa nchi ya ngapi kwa uhuru wa kujieleza na kupata habari africa ukilinganisha na awamu iliyopita!Kuna report(imo humu JF kutoka taasis moja ya kimataifa) inaonesha tumeshuka sana kwenye nyanja hiyo awamu hii!
Hii paragraph ni propaganda tupu na hakuna ukweli hata kidogo!
Sheria kali kama za takwimu na cyber ambazo zimeletwa awamu hii,zote hizi zimetafsiriwa kama namna ya kuminya uhuru wa kujieleza kwa wananchi!

Ndio maana ninasema unafanya propaganda kwa hoja za uongo,hii sio haiba ya Walaki!
 
Nimekupuuza kwa propaganda zako dhaifu,nawajua walaki ndio maana nasema itakuwa tu umejiita hivyo ila sio mwana ukoo huo,Walaki wako smart sana upstairs!
Hiyo ndiyo hoja yako ndugu yangu?..kama ni propaganda ipinge kwa hoja basi achana na maneno ya mipasho hayabadilishi ukweli kuwa katika utawala wa Magufuli kuna ujenzi wa barabara nane ,Mwalimu Nyerere Hydro-electric power,elimu ya sekondari bure ,ongezeko la vituo vya Afya n.k.
Yakatae hayo kwa hoja nitakueleza vizuri tu.
 
Bome-e,
Hujaona nimequote mtaalamu wa siasa za kikanda alivyoielezea siasa ya Nchi hii hapo?Hivi unaelewa maana ya propaganda kweli? Na kama ni uongo prove hoja hiyo ni uongo kwa kuonesha wataalamu wengine walioonesha hoja hiyo siyo sahihi.

Walaki hapo hawaingii ndugu yangu kwa sababu hoja haipo kwao ,jenga hoja yako taratibu bila kuingiza attacks itaeleweka tu.
 
Kwenye democracy index kuna makundi manne!
1.Full democracy
2.Flawed democracy
3.Hybrid democracy
4.Authoritan democracy

Hapo tuko kwenye kundi la 3,yaani tukiteleza zaidi tunaangukia kundi la 4 kwa akina North Korea!
Tumefika hapo kwasababu ya wanasiasa wanaoshika hatamu kuweka sheria kuwabana wakosoaji wao,kuwabambikizia kesi na kuwasweka rumande!

Awamu ya 5 imerudi nyuma kwenye demokrasia ukilinganisha na awamu iliyopita!
Sasa nashangaa unaposema JPM amefanikiwa kuimarisha demokrasia,shame!
 
Bome-e,
Naam.. hapa twende taratibu umekuja vizuri sasa
Kumbuka hayo makundi yamegawanywa kwa vigezo ambavyo vimewekwa na na social structure fulani inayotaka kuendeleza "status quo"..ukifanya critical discourse analysis utagundua hata hivyo vigezo ni pendeleo za watu fulanifulani tu " vested interest".

Democracy ni context bound hatuwezi kuielezea African democracy kwa context ya ulaya.Tukitumia context ya ulaya ni sahihi kusema "Hakuna demokrasia Afrika" jambo ambalo ni sawa na kusema hakuna ustaarabu wa kujisimamia katika Afrika na hivyo Afrika inahitaji kutawaliwa.
Kiuhalisia African Democracy ni tofauti sana na Demokrasia ya Nchi za ulaya.
 
Back
Top Bottom