Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,662
- 27,112
Si kweli maana makundi yanayoangaliwa ni haya ambayo pia sisi yamo kwenye katiba,so si sahihi kusema ni utamaduni wa nchi nyingine!Kama tumeamua kuiishi katiba yetu ya JMT basi lazima tukubali pia yaliyomo laasivyo katiba haifai kama inabakia kama maandishi! Makundi hayo niNaam.. hapa twende taratibu umekuja vizuri sasa
Kumbuka hayo makundi yamegawanywa kwa vigezo ambavyo vimewekwa na na social structure fulani inayotaka kuendeleza "status quo"..ukifanya critical discourse analysis utagundua hata hivyo vigezo ni pendeleo za watu fulanifulani tu " vested interest".
Democracy ni context bound hatuwezi kuielezea African democracy kwa context ya ulaya.Tukitumia context ya ulaya ni sahihi kusema "Hakuna demokrasia Afrika" jambo ambalo ni sawa na kusema hakuna ustaarabu wa kujisimamia katika Afrika na hivyo Afrika inahitaji kutawaliwa.
Kiuhalisia African Democracy ni tofauti sana na Demokrasia ya Nchi za ulaya.
-Muundo na utendaji wa serikali
-Mchakato wa uchaguzi wa viongozi
-Shughuli za kisiasa
-Haki za kiraia
Ukiangalia kwa makundi hayo ambayo ndiyo yanatumika ni wazi hatuna pakukwepea maana makundi yote hayo yanatambulika na katiba yetu!
Hata huyo porofesa uliyemtaja,unadhani ametumia vigezo gani kusema kuwa Tanzania imekuwa na demokrasia toka 1995?Vigezo ni hivyo hivyo!
Pia ninashangazwa kwenye hoja nyingine unatumia international data kujustify hoja zako lakini kwenye hili la democracy,unakuja na sababu za kiutamaduni kukwepa data hizo hizo kwa vigezo hivyo hivyo vya kimataifa!
Halafu kwanini data hizo hizo zilimbeba JK?Na kwanini data hizo hizo zinamuangusha JPM?
Hili ndio swali la msingi kwenye hoja yako namba 3!