Hichi ndio kipindi ambacho WATANZANIA wanapaswa kuzitumia akili zao vyema kuliko kipindi chocchote cha maisha yao....ndicho kipindi ambacho fikra zao zinatakiwa kuchunguza mambo kwa kina na kuyafanyia maamuzi makini kwa ajili ya kipindi cha miaka mitano ijayo....Maamuzi magumu na makini katika kipindi hiki yanatakiwa yachochewe na mateso makali tuliyopitia kwa kipindi cha miaka mitano....Lazima tutambue kuwa mateso na machungu tuliyopitia kwa kipindi cha miaka mitano hayawezi kuzimwa sahani za pilau, vipande vya khanga, posho za vikao vya kampeni wala lifti za magari ya wanasiasa bali kwa kufanya maamuzi sahihi kwa kumchagua mtu sahihi ambaye atatufuta machozi na kutufanya tusahau yote yaliyopita huku tukiganga yajayo kwa matumaini makuu....matatizo ya huduma duni za afya tulizopitia kwa kipindi cha miaka mitano vinatosha kutupa somo la namna ya kufanya maamuzi.....huduma mbovu za usafirishaji katika kila Nyanja ,hapa namaanisha kuanzia majini, nchi kavu , na angani zilizotokana viongozi wetu wabovu kutokujali maslahi ya wengi pia vitupe somo la namna kiongozi bora anapaswa kuwa....kashfa kubwa kubwa zinazowakabili viongozi wa umma za ubadhilifu wa mali za umma na wizi wa fedha za umma pia vinapaswa vituamshe akili kuwa tunataka kiongozi wa aina gani.....lazima tukumbuke kuwa uongozi kamwe haununuliwi......mtu yoyote anayetumia fedha au mali kuwania uongozi tunapaswa kumuogopa na kumkwepa kama ukoma...ni dhahiri shahiri kuwa mtu huyo hatufai...kiongozi wa umma ni wa makundi yote ya kijamii, hapo wapo wenye nacho na wasio nacho, wapo weusi kwa weupe, wapo pia na walemavu sasa mtu kama huyu anapotumia fedha au mali inamaanisha kuwa atajenga matabaka katika jamii yetu kwa atatakiwa kulipa fadhila kwa wale wote waliochangia kuingia kwa madarakani, na hapo ndipo hatari inapoanzia kwani hatakuwa tena kiongozi wa umma bali ni kiongozi wa UMATI......Hichi ndio kipindi ambacho hatupaswi kupumbazwa na kauli tamu za wanasiasa waongo, hatupaswi kuacha akili zetu zichezewe na wanasiasa walaghai , lazima tukumbuke kuwa hatima za mustakabali wa maisha yetu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kinategemea na maamuzi ya leo......MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU ZIBARIKI AKILI ZA WATANZANIA.........AMEN......