Mambo 10 niliyoyaona leo Simba vs Al Ahly Tripoli

Mambo 10 niliyoyaona leo Simba vs Al Ahly Tripoli

Niliwai kusema hapa kwamba Simba walisajili cheap labour ivyo wasitegemee mafanikio kwa hao cheap labour, walienda kuokoteza wachezaji wa bei nafuu, kwenye vilabu vya kawaida ambavyo vingine ata kucheza hatua ya makundi shirikisho avijawai, watawezaje kuhimili mikiki mikiki ya vilabu vyenye wachezaji Wenye uzoefu mechi za kimataifa? Matokeo yake kocha anakwenda na game plan ya kulinda na wachezaji 8 dk zote 90!
Tena analinda dhidi ya timu ya kawaida kama iyo ya tripoli, ni aibu!
No shoot on target ata Moja ndani ya dk 90, No chance created ata Moja, Mpira walikuwa wakiugusa wanakaa nao si zaidi ya dk Moja washanyang'anywa, Kina ahoa, mutale, Debora, barua walikuwa kama vile na wao ni mabeki ilikuwa ni zero performance!
Sijui wewe na kocha wa simba ni nani tumwamini?
 
1. Kama Simba ingefungwa leo lawama angebeba kocha wetu, kocha kabisa una taaluma zako umeaminiwa kufundisha klabu kubwa kama Simba unadiriki kumnyanyua na kumuingiza Valentine Mashaka akawasumbue waarabu kweli? Fahdu umeniudh sana.

2. Wanasimba lazima tukubali wapo wachezaji katika timu yetu ni wa kucheza ligi kuu, kombe la Mapinduzi na kombe la Azam lakini sio kombe Shirikisho, Mashaka na Balua ni mojawapo.

3. Wale waarabu wala sio wa kuiihami, Kibu Dennis alipoingia ndio ameichangamsha sana timu

4. Kipa wa Simba ni 100 kwa 100

5. Upangaji wa timu leo haukuwa mzuri kabisa, viungo Joshua na Balua kama ndio anawategemea Basi ajiandae kufukuzwa

6. Kama tungecheza na timu zenye uwezo mzuri leo tungekula hata bao 6 pale tripoli

7. Jean Charles Ahoua kwa uchezaji ule hatuwezi kutoboa kabisa kabisa

8. Ateba ni striker mzuri mno ila kwa viungo hawa akina Mutale sasa hv tutalalamika

9 Yaani Mukwala akae benchi halafu Mashaka aingie, we kocha mbona unanitia mashaka namna hii.Mashaka hata hajui alikuwa anafanya nini

10. Che Malone Fondoh kama anajiamini kwa namna ile basi kuna cku tutakuja kulia.

Soma Pia: FT: Al Ahly Tripoli 0-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Tripoli International Stadium | 15/09/2024
Nilisinzia kwenye sofa dakika ya 82 Kama sikosei nimeyapata matokeo Jf saa saba usiku..

Kuna moja che Malone alifanya tackling na akamwangusha kwa gwara mchezaji wa tripoli ndani ya 18 wachezaji wa tripoli wakamzonga refa Sanaa refa hakuyumbishwa..
 
Kwakweli kumtoa ateba na kuingia mashaka ni shida hii. Pia kuanza kwa balua na kumuacha awesu awesu na penyewe ni kufeli .
 
Back
Top Bottom