Mambo 10 Niliyoyaona Simba Ikidhalilishwa kwa Mara ya Tano Mfululizo na Yanga

Mambo 10 Niliyoyaona Simba Ikidhalilishwa kwa Mara ya Tano Mfululizo na Yanga

Matokeo mazuri ya Yanga yanatokana na timu kuaandaliwa kwa muda, si kama Simba inayotegemea kujengwa kwa msimu mmoja.
 
Kinachosikitisha ni siku 6 zote wamekula buyu kuwa hawana lolote kuhusu mechi mpaka 7 ndio wanatangaza kucheza?. Tena mechi amabayo inaamua nani awe bingwa?, lengo lao lilikuwa ni nini? Yanga asipate mapato? Hivi kwenye mechi ya simba na yanga kina watu wanawazaga mapato zaidi ya pointi 3?.
 
Simba tatizo ni management na mashabiki mbumbumbu
We fikiria huwa wanagoma kukiri kama YANGA ana quality wao kila siku eti GSM anaharibu ligi, ila wao wakija wanapigwa kama Ngoma
Simba imetengeneza pesa nyingi Sana kwenye michuano ya kimataifa na ni TIMU kubwa kabisa Afrika.
 
Oya kushinda mmeshinda na hongereni kwa hilo. Ila suala la kulazimisha eti Mashabiki wa Simba wakiri sijui Yanga ina quality HILO HALIPO. Wewe ulionao lini Iran, Urusi au China ikakiri uwezo wa Marekani? Au ulionao lini Israeli, Uingereza,na Marekani wamekiri uwezo wa hizo nchi nilizozitaja?

Au nikuulize swali jingine. Wakati Simba ikifanya vyema ikiwa na akina Chama na Miquissine wa kwanza, au ile Simba ya akina Okwi iliyompiga Yanga 5-0. Ni lini wewe binafsi ulikiri kuwa Simba hizo zilikuwa bora kwa Yanga?
Bado kimataifa Simba ni kubwa kulinganisha na yanga.
 
Back
Top Bottom