Mambo 10 ya kisayansi yanayothibitisha kuwa VVU sio chanzo UKIMWI

Mambo 10 ya kisayansi yanayothibitisha kuwa VVU sio chanzo UKIMWI

Nimependa sana ufafanuzi wa mleta mada..ila kuna mamabo kadhaa naona bado yanahitaji maelezo zaidi

Kwanza ni vema ukatuambia una maana gani unaposema kwamba,kwa kuwa T-Cells zinazalishwa nyingi na kwa hiyo kiasi kidogo kinachoathiriwa na vvu haliwezi kuwa tatizo kubwa? Je,unatambua kuwa T-Cell zipo aina tofauti tofauti na ziko recruited kwa specific functions? Na je,unatambua kuwa si aina zote za T-Cells zinazoshambuliwa na HIV?

Tutumie mfano huu: nchi yetu ina majeshi kadhaa..ina polisi,ina magereza,ina jeshi la ulinzi nk..nk.. Pia kuna usalama wa taifa..vikosi vyote hivi ni vya ulinzi na usalama wa nchi..na kila jeshi lina utaratibu wake wa utendaji kutegemea aina ya mafunzo wanayopata na aina ya adui wanayefundishwa kukabiliana naye..sasa kwa mfano,tunaweza kusema,vikosi vyote hivi vina askari laki 2 kwa ujumla wake..Halafu let's say JWTZ is only 5%..Sasa kwa kuwa JWTZ ni sehemu ndogo miongoni mwa vikosi vyote vya ulinzi na usalama..je,tuseme hata kama likiondolewa tutabaki salama kwa kuwa wao ni just 5%?

Unaposema HIV haina uwezo wa kuua T-Cells unamanisha nini? Inafahamika kuwa HIV akiingia ndani ya T-Cell (specifically CD4) anacomand ile cell kutumia rasilimali ilizonazo kutengeneza nakala nyingi za HIV..na kwa kufanya hivyo maisha ya ile cell yanakuwa mafupi,yaani cell inakufa haraka..na hivyo ndivyo kinga inapokuwa inapungua..je,kwa njia hii ni kwanini HIV asihesabike kuwa sababu mojawapo ya Upungufu wa Kinga Mwilini(UKIMWI)?

Hebu fafanua kidogo..

Nimekupata mkuu, T-Cells zimeganyika katika makundi mengi, lakini kwa upana wake zimekuwa grouped katika makundi makuu mawili,yaani Killer T-cells and Helper T-cells. Na ni kweli sio T-Cells zote hushambuliwa na HIV.
[h=1]Lakini ngoja tugusie kwa ukaribu zaidi hizi Helper T-cells ambazo ndiyo target ya HIV.[/h]T-helper cell: Ni aina ya T-Cell ambayo inazipa msaada seli nyingine kuweza kureact na kutambua kitisho na hatimaye kuzalisha protini ijulikanayo kwa jina la Cytokines ambayo hutumika kuzichochea T- cells na B -cells.

Sasa kutokana na maelezo ya hawa Defendant wa HIV/AIDS hypothesis, ni kwamba HIV anashambulia hizi T-helper Cells na kusababisha mwili kuwa dhaifu katika kujilinda na maambukizi. Kumbuka T-helper Cells zimecontain CD4 katika surface zake. Kwahiyo T-helper cells zinapoharibiwa automatically CD4 pia zinaharibiwa. Na ndiyo hapo tunasema kuwa mgonjwa anakuwa na CD4 chini ya 200.

Sasa tukirejea kwenye hiyo fact No:1 ni kwamba hizi T-helper cells huzalishwa kwa wingi mwilini na HIV ina uwezo wa kuathiri T-helper Cell moja kwa 1000, sasa iweje HIV isababishe kushuka kwa mfumo mzima wa kinga hali ya kuwa kitu kinacho play part kubwa katika mfumo wa kinga bado kiko katika ubora wake?
Hivyo basi HIV si sababu ya UKIMWI kuna kitu kingine ambacho kinahusika katika kushusha mfumo mzima wa kinga katika mwili wa binadamu na sio HIV.

Katika mfano wa majeshi uliyotoa naomba kabla sijakujibu nikuulize swali;
Assume mlango wa grill una komeo 2 juu na chini, na komeo zote zimefungwa kwa kufuli za solex ambazo ni imara, je kuvunja kufuli moja ya komeo kutakufanya uweze kuufungua mlango na kuingia ndani?

Sasa nakuja kwenye jibu lako, kwa kupitia kwenye mfano wako, kwanza ungetoa mfano wa jwtz pekee igekuwa vizuri zaidi, usihusishe majeshi mengine maana hayo sio target ya adui, hapa tunazungumzia T-helper Cell huyu ndiye adui kwa HIV na si seli nyinginezo.

Inaamaana ulipaswa kutoa mfano wa jeshi la ulinzi kama JWTZ, yaani hiko kikosi cha askari laki 2 wawe JWTZ ili kuleta maana halisi ya mfano wako.

Then katika hao askari laki 2, tutoe 5% ya askari, kwa mfano huu efficient ya jeshi itapungua kidogo, maana ni asilimia ndogo tu ya askari wamezulika.

Sasa tuje kwa kesi ya UKIMWI, idadi ndogo ya T-Helper Cell inayozulika kutokana na HIV haisababishi mfumo mzima wa kinga ku break down isipokuwa efficient ya ulinzi itapungua.

Na hili liko wazi kwa mara ya kwanza HIV anapofanya infection, mtu hukumbwa na mafua makali then kinga inakuwa generated na mchezo unakuwa umeishia hapo (GAME IS OVER. HIV IS NO MORE).

Mafua haya makali ni dalili ya kutetereka kwa mfumo wako wa kinga na si kuwa breakdown katika stage ya kusababusha magonjwa zaidi ya 20.
 
Mkuu @poverty eliminator naomba usinipoteze.
Hapa unamaanisha T-Cells au T-helper cells?

Maana mwanzo wa topic umesema T-seli(T-Cells), na sasa unasema T-helper cells..inaweza kutupa shida kuelewa. Kwa kuwa 5% ya T-Cells si sawa na 5% ya T-helper cells! Na hata mfano wa jeshi niliotoa hapo juu nilikuwa sahihi maana tulikuwa tunazungumzia jeshi la T-Cells;ambamo kuna vikosi kama T-helper cells(CD4+),Cytotoxic T Cells(CD8+),Memory T Cells,Supressor T Cells nk..nk.. ndo maana nikasema ikiwa vikosi vya T-helper cells ni 5% ya vikosi vyote vya T-cells na vikaondolewa,je kinga itabaki vile vile?

Na kuhusu makomeo mawili yenye makufuli..hiyo ni simple logic! Kwanini yamewekwa mawili? Does it mean kwamba,
makomeo 2 = komeo 1? Kwamba ukiondoa moja likabaki moja,ulinzi utakuwa sawa,then kwanini yamewekwa mawili?!!
 
Mrimi,
Kaka najua umeshanielewa, ila ni vizuri ulivyouliza maana itawasaidia wengine wasioelewa, Ok! ngoja nikuweke sawa, T-Cell aina ya T-Helper Cell ndiyo target ya HIV.

Yap! inawezekana huo mfano ukawa ni simple logic but unapotoa mfano wa majeshi wa JWTZ na majeshi mengine hakuna logic pia, kama nivyokwambiia target ni T-Cell aina ya T-helper Cell....yaan kwa mfano wako target inatakiwa iwe JWTZ maana ndo walinda mipaka ya nchi..thats why nikakwambia base kwenye JWTZ hapo mfano wako utakuwa na logic zaidi.
 
poverty eliminator,
Huenda wewe huelewi point yangu iko wapi au pengine mimi ndo sikuelewi. Look,article yako imeanza kwa maelezo mengi juu ya uhusiano wa T-Cells na UKIMWI. umesema kwa siku mwili unatengeneza 5% ya

T-cells..na ktk hizo,ni 1/1000 ya T-cells ndizo zinaathirika na HIV..na tunakubaliana pia kwamba,T-cells ni broad term..kwa maana kwamba ktk hizo kuna % fulani(ambayo hujatuambia!) ya cells ambazo ni T-helper,ambazo hasa ndiyo target ya HIV.

Sasa shida yangu ni: hizi takwimu za 5% na 1/1000, ni za T-cells kwa ujumla wake au unamanishisha T-helper pekee?
 
Huenda wewe huelewi point yangu iko wapi au pengine mimi ndo sikuelewi..
Look,article yako imeanza kwa maelezo mengi juu ya uhusiano wa T-Cells na UKIMWI..umesema kwa siku mwili unatengeneza 5% ya T-cells..na ktk hizo,ni 1/1000 ya T-cells ndizo zinaathirika na HIV..na tunakubaliana pia kwamba,T-cells ni broad term..kwa maana kwamba ktk hizo kuna % fulani(ambayo hujatuambia!) ya cells ambazo ni T-helper,ambazo hasa ndiyo target ya HIV..

Sasa shida yangu ni: hizi takwimu za 5% na 1/1000, ni za T-cells kwa ujumla wake au unamanishisha T-helper pekee?
Mkuu Mrimi naona hatuwezi kufikia conclusion, nimekuwekea reference hapo chini, ingia usome zaidi then nadhani utapata information nyingi zaidi ya hizi na kupata majibu ya maswali mengi ambayo unaona yana utata.
 
It is all about money, there is tons of dollars in keeping this this alive and kicking!!!

True dat, uwepo wa UKIMWI miaka 30 (miaka 3) umewafanya watu kumiliki villas na luxury cars, UKIMWI ni Dollor billion industry. Kuna watu hawapo tayari kuona hii biashara inaondoka. Na kitu cha kusikitisha zaidi kuna baadhi ya waafrika kwa kujua ama kutokujua wameingia kwenye mtego wa hii biashara, wanaangamiza waafrika wenzao kwa maslahi ya viwanda vya madawa, condoms na HIV blood test kit kutoka nchi za magharibi. Its so sad.
 
Mkuu Mrimi naona hatuwezi kufikia conclusion, nimekuwekea reference hapo chini, ingia usome zaidi then nadhani utapata information nyingi zaidi ya hizi na kupata majibu ya maswali mengi ambayo unaona yana utata.

Kwani mkuu ugumu uko wapi?
Nilitaka kujua tu kuwa takwimu hizo ni za nini hasa..T-cells kwa ujumla wake au ni za T helper pekee? Na pengine % ya T-helper miongoni mwa wenzake. Usikate tamaa mkuu mi nahitaji kujua tu..
 
Ukimwi ipo kijana.

Hakuna aliyesema UKIMWI haupo kaka, jaribu kusoma kabla huja comment, tunachosema ni kwamba HIV sio sababu ya Upungufu wa kinga kwenye mwili wa binadamu (UKIMWI). UKIMWI upo na umekosa dawa kwa miaka 30 sababu ya wrong target ya research.
AIDS Research has not failed to find a cure…. AIDS research has failed because it never found the cause!
 
It is all about money, there is tons of dollars in keeping this this alive and kicking!!!

True dat, but nashauri tukiwa kama waafrika (mimi na wewe) tusome, tudadisi na tufatilie mambo kwenye ulimwengu, tusiishi kama tupo kwenye chupa. Then we can make permanent decision for permanent emotion.
 
Kwani mkuu ugumu uko wapi?
Nilitaka kujua tu kuwa takwimu hizo ni za nini hasa..T-cells kwa ujumla wake au ni za T helper pekee? Na pengine % ya T-helper miongoni mwa wenzake. Usikate tamaa mkuu mi nahitaji kujua tu..

Yap! najua unataka kujua thats why niliweka reference kwa watu wenye uwezo wa kudadisi kama wewe, ili upate more inforrmation ambazo zinaweza kukufanya ufikie right conclusion...Go for it...i believe ur smart utafikia conclusion.
 
Huenda wewe huelewi point yangu iko wapi au pengine mimi ndo sikuelewi..
Look,article yako imeanza kwa maelezo mengi juu ya uhusiano wa T-Cells na UKIMWI..umesema kwa siku mwili unatengeneza 5% ya T-cells..na ktk hizo,ni 1/1000 ya T-cells ndizo zinaathirika na HIV..na tunakubaliana pia kwamba,T-cells ni broad term..kwa maana kwamba ktk hizo kuna % fulani(ambayo hujatuambia!) ya cells ambazo ni T-helper,ambazo hasa ndiyo target ya HIV..

Sasa shida yangu ni: hizi takwimu za 5% na 1/1000, ni za T-cells kwa ujumla wake au unamanishisha T-helper pekee?

Mkuu uko sahihi kwamba hajakuelewa swali lako,nimeipata vizuri maana ya swali lako,ni kweli kwamba amezungumzia T-cells in general bila ku specify.Lakini mjadala kati ya wewe na yeye kuhusu jambo hili umeibuka kwa sababu moja tu ambayo ni kuhusu HIV kuua T-helper cells.Inawezekana ni kwasababu amejibu kwa haraka,lakini akija tena nina uhakika utakuja kivingine.

Jibu sahihi linaloendana na uhalisia ni hili hapa chini:

Ni kwamba HIV haui T-cell yoyote anayo infect(hapa nazungumzia hata hiyo ambayo inaaminika ndio target yake,yaani T-helper cells).Hapa swali lako linakua halina maana tena.Kutokana na chanzo alichotumia mleta mada,kuna maneno yamepishana kidogo na yake kiasi cha kuleta mkanganyiko huu kati ya wewe na mleta mada.Chanzo kinasema kwamba "HIV does not kill T-cells it infects(T-helper cells),Robert Gallo and other AIDS researcher used T-cells(general) to grow the virus because HIV lives compatibly with T-cells".

Je,unajua kwa nini Dr.Peter Duesbsrg alipata mshtuko aliposikia Robert Gallo anasema kwamba HIV anaua T-cells(T-helper cell)?

Hata wewe ukisikia mtu anasema Bifidus bacteria anasababisha kifo kwa binadamu yeyote aliyenaye najua utashtuka pia,hii ni kwa sababu haiendani na mafundisho na tafiti ulizopitia/kujifunza ukiwa shuleni na tafiti zako binafsi,na pia unajua kwamba kila mtu anao bifidus bacteria,hivyo lazima ushangae utakaposikia hivyo.

Basi Dr.Peter Duesberg naye ni vivyo hivyo, Peter ni very intelligent virologist mwenye vey high/good reputation,si rahisi kukurupuka na kuhoji swal hili bila data na hoja za msingi.Kina Gallo wenyewe wanamtambua huyu jamaa kwa uwezo wake,huyu jamaa alifanya vitu ambavyo kina Gallo walishindwa kuhusu virus na akapewa Nobel prize ya vitu hivyo.

Hivyo Peter Duesberg sio wa kubeza.Ukifuatilia historia ya utafiti wa kina Gallo na wenzake kuhusu HIV ndio utaelewa vizuri kwa nini HIV haui T cell yoyote,achilia mbali T helper cell pekee,HIV haui T cell yoyote.Retrovirus yeyote hana uwezo wa kuua T cell yoyote,"to infect does not mean to kill".So HIV does not kill T-helper cell it infect, for this case.

Kilichowafanya wewe na yeye muanze kujadili hili ni kuhusu HIV kuua T helper cell.Chanzo kinasema hivi;"HIV does not infect enough T cells(T helper cells) to cause AIDS",narudia,to infect does not mean to kill.

Chanzo kinaendelea kusema;"even if HIV kill T helper cells,it can't kill enough T cells(T helper cells) to cause AIDS",yaani hapa maana yake si kwamba chanzo kimekubali kwamba HIV anaua T helper cells,la hasha,ila chanzo kinataka kuonesha kwamba HIV si sababu kabisa ya AIDS hata kama HIV atapewa uwezo wa kichawi kuua T helper cells bado hana uwezo wa kusababisha AIDS kwa kuwa kiwango cha HIV kwenye T helper cell ni kidogo mno(1/1000).Penye ukweli siku uongo hujitenga.

Halafu pamoja na mjadala huu kati ya wewe na yeye,lakini umesahau kuzungumzia point za msingi alizoziweka yeye ambazo kama point hizi ni kweli basi mjadala wote huu unaofanya kati ya wewe na yeye wa HIV kuua T helper cells hauna maana tena.Point hizo ni;

1.HIV is harmless after antibody immunity.HIV hufubaa na kupoteaa kabisa baada ya kushambuliwa na kinga ya mwili.Na ndio maana kwenye majaribio ya maabara ya Robert Gallo baada ya kuchukua blood kutoka kwa AIDS patient,hakufanikiwa kukuta HIV kwenye T cells(T helper cells) sio kwamba Gallo alikuwa incompetent,la hasha,bali huo ndio ukweli kwamba hakukuta HIV kwenye T cells(T helper cells),ni antibodies ambazo ndizo ziliweza kuonekana,na hizo antibodies zenyewe ni controvesial kama utafuatilia vizuri historia hii ya ugunduzi.

Na ndio maana Gallo baada ya kushindwa kupata HIV kwenye damu aliiba lab data kutoka kwa Luc Montaigner wa France mpaka ikaleta mgogoro kugombania patent na marais wote wawili Reagan na Jacques Chirac waliingilia kati kutatua.Na hata wewe unajua kwamba vipimo vinapima antibodies against HIV.Sasa kama una antibodies maana yake tayari HIV is under control.

Mainstream wamempa HIV uwezo wa kichawi wa kujibadili ili asiweze kudhulika na kinga ya mwili,mimi huwa nacheka sana ninaposikia madaktari wanasema hivyo.Fuatilia utajua tu.

2.Kiasi kidogo sana cha T cells(T helper cell) kinaweza kuathiriwa na HIV.Kuathiriwa haina maana ya kuuawa/kufa.

Ukiniambia nikupe uthibitisho kwamba HIV haui T cell yoyote nitakanchofanya ni kukupa mifano ya watu ambao wamepimwa HIV+ lakini wanaishi kwa miaka zaidi ya 20 bila kula ARVs.Watu hawa wapo wengi sana,na ukichunguza sana utakuta kwamba wanaokufa ni wale wanaotumia ARVs,maana ARVs ndizo husababisha AIDS kwa wale wanaozitumia.

Sitaelezea kisayansi kwanini HIV haui T cell yoyote kwa kuwa kina Gallo na Duesberg wote walishafanya haya,ni juhudi zako tu kufuatilia.

Hebu msikilize kwa makini sana hapa chini Prof.Luc Montaigner mgunduzi wa HIV kwenye hii video ya takribani saa 1,sikiliza kwa makini sana,usiruke point yoyote.Hapo ndipo utakapoelewa kwamba HIV/AIDS ni mchezo wanaochezewa wale walio gizani tu.

Nimekupa link hii ya mtu aliye upande wa mainstream,sasa nikikupa link ya mtu anayepinga ndio nitapigilia msumali wa mwisho kwenye jeneza la HIV/AIDS na ugonjwa huu usitiliwe kabisa maana kwa kuwa ni feki kupindukia.

 
Deception,
Thanks! Mkuu Deception kwa ufafanuzi mzuri, nafurahi kuona mwafrika mwenzangu especially mtanzania ukiwa unafatilia mambo na kudadisi kwa kina. Na umetoa mfano wa huyo Co-Founder wa HIV (Luc Montagnier). Kwenye AIDS Conference ambayo ilifanyika San Francesco, Marekani mwaka 1990 alikiri wazi kwamba HIV is Harmless. Hii ilikuwa nia miaka 3 mbele baada ya Dr.Peter Duesberg kutoa chapisho lake la utafiti wa kansa na kusema kwamba HIV sio sababu ya magonjwa yote yaani kansa na ukimwi.

Kwa kuongezea hapo watu wengi hususani sisi waafrika hatufahamu CV's za hawa Opponents wa HIV/AIDS hypothesis. Dr.Peter Duesberg ni mtu wa kwanza ku map genetic structre ya retrovirus kikiwemo kirusi hicho cha HIV. Ni mtu ambaye ame deal na retrovirus kwa miaka mingi, so ni mtu ambaye anajua weakness na strength ya retroviruses.
Pia ni mtu wa kwanza kugundua genes ambazo zinasababisha ugonjwa wa kansa.

Pia kuna mtu anaitwa Dr.Kally Mullis, huyu ana Nobel Prize kwasababu ya invention aliyofanya katika ulimwengu wa sayansi. Huyu ndiye aliye invent technlogy ya PCR (Polymerase Chain Reaction). Hii ni moja ya technology ambayo vipimo vya UKIMWI inavitumia.
Hao ni baaadhi tu ya reputed scientists ambao wame question hii hypthesis ya HIV/AIDS.
 
Aisee huu ugonjwa una big controversy, nimefatilia kwa ukaribu historia ya huu ugonjwa na kusoma vitabu zaidi ya 10, articles nyingi na kuangaliia documentary nyingi. Nimefatilia facts za hawa waanzalishi wa hii nadhariia ya HIV/AIDS (Defendants) na pia nimefatilia facts za wanaopinga hii nadharia (Denialists). Kitu ambacho nimegundua ni kwamba hawa waanzilishi wa nadharia ya HIV/AIDS ni watu ambao wanakimbia fact za sayansi na kwenda kwenye imagination zaidi. Sasa ukiona Scientist anakimbia uwanja wake wa nyumbani (Scientific Ground) ujue kuna problem.

Na kitu cha kushangaza kama dunia inapambana na adui mmoja ambaye ni UKIMWI, why tunagombania fito????
Na kwanini tunakataa mawazo mbadala hali ya kuwa tunataka ku solve tatizo? waanzalishi wa nadharia ya HIV/AIDS wameshindwa kupata chanjo na dawa huu ni mwaka 30 sasa. Na wakati marekani wanautangazia ulimwengu kwamba kuna kirusi kinaitwa HIV kinasababisha ugonjwa wa ukimwi wali promise chanjo ingepatikana ndani ya miaka 2.

Me binafsi naamini kam ukimwi ungekuwa unasababishwa na kirusi na ungekuwa ugonjwa wa kuambukizwa, kutoka mwaka 1984 mpaka miaka ya tisini 96 au 98 kinga au dawa ya huu ugonjwa ingekuwa imeshapatikana.
Maana ukifatilia history of medicine kwenye huu ulimwengu, magonjwa yote ambayo yalikuwa ya kuambukiza na ambayo yalikuwa yakisababishwa na virusi yaliweza kudhibitiwa kwa chanjo tu na antibiotics, hiyo ni success story of medicine, isipokuwa magonjwa ambayo si ya kuambukiza kama Kansa na magonjwa mengine, haya yameshindwa kuwa controlled kwa chanjo na antibiotics. Sasa why Ukimwi? je ukimwi ni kansa mpya????

Mm nadhani huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote.....this is time to rethink again HIV/AIDS hypothesis.
 
Inachangaya kiasi..najikuta naelewa nikisoma zaidi nasahau nilichoelewa mwanzo..
naomba mnijuze kwaufupi kinachoua watu ninini hasa mpaka kufananishwa na ukimwi?..

Kinachoua watu hakifanani katika nchi maskini na zilizoendelea, na ndiyo maana takwimu za ukimwi amerika na ulaya hazifanani na afrika...takwimu zinaonesha wagonjwa wengi wa ukimwi wako afrika especially kusini mwa jangwa la sahara.

Sababu ya UKIMWI kwa nchi maskini zikiwemo nchi nyingi za afrika ni; utapiamlo, matumizi yaliyopitiliza ya antibiotics, magonjwa kama malaria na tb na mitindo mibaya ya maisha. Avrs pia inachangia sana kusababisha ukimwi, ina haribu organ muhimu kwenye miili ya watanzania wengi tu.


Kwa nchi zilizoendelea sababu ni matumizi ya madawa ya kulevya ambayo watu huyatumia kama sehemu ya starehe;
mfano wa madawa hayo ni; HEROIN, COCAINE, POPPERS, BARBITUATES, SPEED, PCP na LSD.
 
poverty eliminator,

Kwann asilimia kubwa ya wenye ukimwi wana HIV+..
na kwann ukishiriki tendo na mwenye virusi baada ya muda unakua na dalili zenye kufanana na mwenye ukimwi?..

ili tusipate ukimwi nini kifanyike?..

Kuna ukweli kwamba virusi vyaukimwi viantofautiana kati yamtu mmoja na mwingine?..
 
Kwann asilimia kubwa ya wenye ukimwi wana HIV+..
na kwann ukishiriki tendo na mwenye virusi baada ya muda unakua na dalili zenye kufanana na mwenye ukimwi?..

ili tusipate ukimwi nini kifanyike?..

Kuna ukweli kwamba virusi vyaukimwi viantofautiana kati yamtu mmoja na mwingine?..

Thanks! kk kwa maswali yako. Nikianza na swali lako la kwanza, kama nimekuelewa ni kwamba kuwa na HIV+ kwa wagonjwa wengi wa Ukimwi kunakufanya uamini HIV ndo sababu ya UKIMWI, nadhani niko sawa hapo.

Kumbuka Ushahidi wa hypothesis isemayo HIV ni sababu ya UKIMWI umeegemea juu ya uhusiano (correlation) tu. Sababu virusi wa HIV hupatikana katika wagonjwa wengi wa UKIMWI, hivyo ikadhaniwa huenda HIV husababisha UKIMWI.

Lakini logic ya hii hypothesis ina walakini mkubwa sana kwa sababu uhusiano (correlation) hauwezi kuthibitisha Usababisho (Causation).

Sasa basi kama HIV haina mahusiano na UKIMWI, ni rahisi kupata watu wenye UKIMWI bila kuwa na HIV na watu wenye afya ambao wanaishi na HIV lakini kamwe hawauguwi UKIMWI.

Hakuna siri katika hili, katika bara la Afrika utafiti umeonyesha zaidi ya asilimia 65% ya wagonjwa wa UKIMWI hawana HIV. Huku kwetu Afrika positive results hazina umuhimu kwa ajili ya kuripoti wagonjwa wa UKIMWI; dalili za kuugua muda mrefu zinatosha.

Tuje kwenye swali lako la 2.
Umeuliza ni kwanini ukishiriki tendo na mwenye virusi baada ya muda unakua na dalili zenye kufanana na mwenye ukimwi?

Huo muda ambao unasema kutoka kushiriki tendo na mgonjwa wa ukimwi mpaka kuanza kuugua huwa unaweza kufika hata miaka 20.Sasa kwa kipindi cha miaka 20, unakula diet mbovu, unaugua malaria mara kwa mara, unakula madawa feki, unakula vyakula feki, unafanya ngono mara 60 kwa wiki, je mfumo wako wakinga utabaki vipi salama?

Pili tuseme imetokea umefanya ngono na mtu mwenye kirusi, miaka 10 bdaye unakuja kuugua ukimwi, hiki kipindi cha kati kuna mambo mengi yanatokea, fikiria kwa kipindi hiki cha miaka imetokea umeenda kucheki afya, baada ya kupimwa ukakutwa upo positive, kinachofuata ni wewe kupanic, kuwa na msongo wa mawazo na kukimbilia kula ARV's (Baadhi ya watu hujiua), sasa hapo ndipo unaanza kudevelop dalili za ugonjwa wa ukimwi, yaan unapata ukimwi by medical prescription na stress tu.

Nije kwenye swali lako la 3, kwa mtazamo wangu sidhani kama waafrika tunahitaji ARV's ili kupambana na UKIMWI. Hivyo kila mtu anatakiwa ku play part yake. Sisi kama waafrika na watanzania tunapaswa kubadili mitindo ya maisha (Mfano: Huwezi kunywa pombe kila siku huku ukiwa unakula diet mbovu na kufanya ngono mara 50 kwa wiki ukabaki salama).

Hapa ni pagumu sana, na ndiyo maana nowdays watanzania wengi tunaugua visukari, figo zinafeli, upungufu wa nguvu za kiume na magonjwa ya ajabu ajabu, bad lifestyle inatuangamiza.

Kwa upande wa tume ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS) ijikite kwenye kuelimisha watu kupitia television na radio. Maisha ambayo tunaishi ni hatarishi kuliko kuwa na michepuko (Simaanishi uwe na michepuko). TACAIDS wajikite kuwaelimisha watu wale vizuri na kufanya mazoezi.

Kwa upande wa serikali kama serikali, iongeze nguvu kwa taasisi kama TFDA kuwa na uwezo wa kudhibiti madawa na vyakula feki kabla havijaangia sokoni. Ni mara ngapi TFDA imekamata madawa na vyakula feki? Na je ni madawa na vyakula feki kiasi gani vimeingia sokoni na kuaathiri mamilioni ya watanzania?

Nikija kwenye swali lako la mwisho, hakuna kitu kama hicho, kutokana na hizo facts za kisayansi UKIMWI hausababishwi na kirusi na wala hauambukizwi (It is not both a viral epidermiology and infectious disease).

Kwahiyo hakuna kitu kinachoitwa kirusi cha UKIMWI. So swali lako litakuwa halina tija hapa.
Mwisho, watanzania tukiwemo mimi na wewe tunapaswa kujua mitindo ya maisha ambayo tunaishi, vyakula ambavyo tunakula, madawa ya hospitali ambayo tunatumia, malaria, tb na mazingira yanayotuzunguka ni vitu hatarishi kwa asilimia 100% kuliko hata kirusi cha HIV.
 
Back
Top Bottom