Mambo 10 yanayothibitisha kwamba Mungu yupo

Mambo 10 yanayothibitisha kwamba Mungu yupo

Wapi Mungu kamuhitaji binaadamu kwa lolote? Kwamba kwa sababu wewe unasema hayupo basi yeye huko ajioneshe kwa watu kuwa yupo ili wewe uthibitishe uwepo wake ili iweje sasa?
Huyo Mungu hayupo.

Ni wewe tu unahangaika kufosi aonekane yupo.
Ipo hivi mkuu, suala la Mungu ni la imani na si bahati mbaya bali ndio alivyotaka hivyo kuwepo wasioamini haiwezi kuwa ajabu ni lazima iwe hivyo maan kuamini ni hiari.
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.

Sasa tutahakikisha vipi na kuthibitisha vipi kwamba imani yako ina ukweli?
 
Nani kasema nataka kuthibitisha? Au umekariri tu kusema thibitisha ila hujui hata huo uthibitisho wa kuthibitisha huyo Mungu unapaswa uweje?
Sema unapaswa uweje? Nahitaji kujua.
 
Mnahangaika sana kumwelezea, kumtetea na kumuongelea Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe, kujitetea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe, Yeye kama yeye kwamba yupo.

Ni ninyi tu mnahangaika kufosi aonekane yupo, Kumbe hayupo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe yupo kama ana huo uwezo.

Sio ninyi mumuhangaikie kumuelezea uwepo wake.
 
Kwa lugha rahisi

👉🏾Kuna vielelezo na hoja mbalimbali ambazo zimekuwa zikijaribu kuthibitisha uwepo wa Mungu. Ingawa uthibitisho wa moja kwa moja wa Mungu ni jambo linalozungumziwa kwa mitazamo ya imani na siyo masuala ya kisayansi, baadhi ya hoja zinazotumika kuunga mkono wazo la uwepo wa Mungu ni pamoja na:

👉🏾Dhana ya uumbaji (Cosmological Argument)
Hoja hii inadai kwamba kila kitu kinachoonekana kuwa na mwanzo kinahitaji sababu. Dunia na ulimwengu wetu unaonekana kuanza, hivyo lazima kuwepo na kitu cha nje ambacho kilianzisha kila kitu, na hicho kinaitwa Mungu. Hii ni hoja ya kimsingi ambayo inatolewa na wanatheolojia wengi kwa kusema kuwa Mungu ndiye chanzo cha ulimwengu.
😊 embryonic similarities between different creatures

👉🏾Hoja ya Design (Teleological Argument)
Hoja hii inadai kwamba ulimwengu na maisha yanayoendelea ni ushahidi wa mpango maalum au uundaji. Mfumo wa asili, kama vile miundo ya wanyama, mimea, na mazingira, inaonekana kuwa na mpango maalum unaowezesha maisha kuendelea. Wanaamini kwamba haya ni matokeo ya akili ya kimungu inayoshughulikia uumbaji.

👉🏾Hoja ya Maadili (Moral Argument)
Hoja hii inasema kuwa kuwa na maadili na hisia za haki ni dalili ya uwepo wa Mungu. Kwa mfano, watu wanahisi kuwa kuna mambo fulani ni sahihi na mengine ni mabaya, na hii inahitaji msingi wa kimaadili wa nje, ambao ni Mungu. Hoja hii inathibitisha kwamba uwepo wa maadili ya kimungu unaeleza mifumo ya tabia za kibinadamu.

👉🏾Hoja ya Uzoefu wa Kibinafsi
Watu wengi wanasema kuwa uzoefu wao wa kibinafsi na Mungu unawaonyesha kuwa Mungu yupo. Hii inaweza kuwa katika hali ya maombi, mawasiliano ya kiroho, au hata wakati wa mateso ambapo mtu anapata hisia ya kuwa Mungu anakuwepo na anakupa nguvu.

👉🏾Hoja ya Uthibitisho wa Vitabu Vitakatifu.
Vitabu vitakatifu kama Biblia, Qur'ani, na vitabu vingine vya dini vinasema kuwa Mungu yupo na mara nyingi huonekana kama vyanzo vya kweli kwa waumini. Wengi wanasema kwamba unabii, miujiza, na mafundisho katika vitabu hivi ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu.

👉🏾Hoja ya Ulimwengu wa Asili
Mfumo wa asili, kama vile ulimwengu wa mimea na wanyama, unaonekana kuwa na ufanisi mkubwa. Hakuna maelezo ya kisayansi ambayo yanaweza kufafanua kwa kamili kwa nini na jinsi ulimwengu huu ulivyo na utaratibu mzuri, kwa hivyo wanatheolojia wengine wanatambua hii kama ishara ya kuwepo kwa Mungu.

👉🏾Hoja ya Uthibitisho wa Historia na Miujiza.
Katika historia, kuna matukio na miujiza mbalimbali ambayo watu wanadhani ni ushahidi wa uwepo wa nguvu ya kimungu. Hii ni pamoja na matukio ya ajabu yanayoshuhudiwa na jamii na waumini, kama vile uponyaji wa ajabu au mabadiliko ya kimazingira yaliyoonekana kama matokeo ya maombi.
Mfano mwenyewe nimewahi kushuhudia , miaka ya 2006 na 2007 ,Tosamaganga Iringa kulitokea ukame na mvua hazikunyeshwa watu wakaombwa kusali kwa imani zao , Msikitini,Makanisani, na hata wale wazee wakimila masaa machache mvua zilinyesha balaaaa, (SO THERE IS SUPERNATURAL POWER GOVERN THE WORLD)

amini Mungu yupo ,puuza halafu ukamkute utameza ulimi nakuambia🙏
 
Unahisi kwa nini napaswa kuamini na sio kujua?
Sijasema unapaswa kuamini maana kuamini ni hiari ndio maana huwa nasema huwezi kumlazimisha mtu kuamini. Ila kuamini ni sehemu ya maisha yetu binaadamu sidhani kama kuna binaadamu asiye amini.

Halafu kujua wala sio kinyume cha kuamini, hata tunayoyaamini tunayajua sijui kwa nini mnalikuza hili neno kujua.
 
Mnahangaika sana kumwelezea, kumtetea na kumuongelea Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe, kujitetea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe, Yeye kama yeye kwamba yupo.

Ni ninyi tu mnahangaika kufosi aonekane yupo, Kumbe hayupo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe yupo kama ana huo uwezo.

Sio ninyi mumuhangaikie kumuelezea uwepo wake.
Ok bora wewe umeweka wazi kwamba kumbe sababu ya kusema hakuna Mungu ni kwa kuwa haonekani ndio maana mnasema hayupo.
 
Biblia inaeleza mambo mengi kuhusu Mungu. Na Biblia imeandikwa na wanadamu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, ukisoma Biblia utajua habari za Mungu na unaweza kuwaelezea wengine wasiomjua Mungu.
Biblia ni madai sio ushahidi.
 
Ok bora wewe umeweka wazi kwamba kumbe sababu ya kusema hakuna Mungu ni kwa kuwa haonekani ndio maana mnasema hayupo.
Sio haonekani tu.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Maana kuna vitu havionekani ila vipo, mfano upepo.

Mungu ni dhana ya kutungwa na kufikirika tu mliyo jitungia huko vichwani mwenu.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Mungu ni jina uchwara tu mlilo jitungia.
 
Biblia inaeleza mambo mengi kuhusu Mungu. Na Biblia imeandikwa na wanadamu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, ukisoma Biblia utajua habari za Mungu na unaweza kuwaelezea wengine wasiomjua Mungu.
Kutumia Biblia kusema kwamba ndio uthibitisho wa uwepo wa Mungu ni sawa na kutumia hekaya za vitabuni kusema kwamba ndio uthibitisho wa uwepo wa Abunuwasi.
 
Mwalimu wangu wa falsafa wakati anatufundisha metaphysics alituambia kuwa " we know God through negation and affirmation". Kuwa ukisema Mungu hayupo hicho ni kinini unachosema hakipo?. Once you negates about God you prove His existence. Mujwahuzi the PhD .
Unafahamu kwamba huko Japan kuna dini inayoamini Mungu anayeitwa Erick???

Unajua huyu Erick ni Mungu wa aina gani kwa mafundisho ya dini hiyo?

Ngoja nikuelezee kwa ufupi.

Huyu Erick ni maarufu kwa jina kamili la Erick God eater. Yani ni Penguin wa kimiujiza ambaye kazi yake ni kula Mungu na Miungu.

Umeelewa tunakoelekea??

Kwasababu Erick God eater ana kusudio moja tu la kula Mungu na Miungu basi hoja itayofuata ni kuwa Mungu wako alikwisha liwa na huyu Erick so kimsingi hayupo.

Otherwise uthibitishe Erick God eater hayupo.

Namimi hapo nitakuuliza Kuwa "ukisema Mungu Erick hayupo hicho ni kinini unachosema hakipo"
 
Okay

Nikikuambia kuwa nina vidole 10 kwenye mikono yote miwili, unaweza kuniamini bila hata kuhoji swali.

Lakini nikikuambia mbali na hivyo vidole 10, nina vidole viwili vya ziada kwenye kila mkono.

Pengine utashangaa na huwenda ukaamini labda i'm just born different.

Lakini nikaja na hii

Nikasema nina macho matatu kwenye paji la uso na kwenye kisogo so nauwezo wa kuona vision zote katika nyuzi 360.

Halafu nikakutumia na hii picha kama uthibitisho

View attachment 3188949

Je utakuwa satisfied na huo uthibitisho?

Bila shaka hautorudhika na ushahidi wa aina hiyo na utaomba ushahidi mwingine.

Kwa hiyo kadri unavyozidi kuelezea vitu ambavyo sio vya kawaida ndivyo jinsi ambavyo utahitaji kutoa uthibitisho mkubwa zaidi ku prove madai hayo.

The more extraordinary the claim, the more extraordinary the evidence that is required to demonstrate it.
Hujaeleza huo uthibitisho unatakiwa uweje ili sasa pengine hao wanaojaribu kuthibitisha waweze kujua huo uthibitisho unatakiwa uweje ili wajue wathibitishe kwa aina gani, kinyume na hivyo hakuna kitakachokubaliwa kama uthibitisho na madai ya kwamba hakuna uthibitisho yataendelea kuwepo.

Maana nilichogundua kwenye hili suala la uthibitisho ni kwamba hakuna idea hata huo uthibitisho unafananaje kitu kinachofanya ni ngumu kuweza kukubali kuwa huu ni uthibitisho.

Japo najua kinachomfanya atheist kupinga uwepo wa Mungu sio kutokuwepo kwa uthibitisho maana ingekuwa hivyo basi kusingetokea atheist kuja kuwa muamini Mungu hali ya kwamba bado uthibitisho hakuna.
 
Sio haonekani tu.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Maana kuna vitu havionekani ila vipo, mfano upepo.

Mungu ni dhana ya kutungwa na kufikirika tu mliyo jitungia huko vichwani mwenu.

Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.

Mungu ni jina uchwara tu mlilo jitungia.
Umesema mwenyewe mara kadhaa kuwa kama Mungu yupo aje ajisemee mwenyewe na kama kweli yupo ajitokeze, wakati wewe unasema kwa uhakika kuwa Mungu hayupo kuna wenye kusema hakuna namna ya kujua kuwa huyo Mungu yupo au hayupo, sasa unadhani wewe umewezaje kujua kuwa hayupo kwa uhakika?
 
Hujaeleza huo uthibitisho unatakiwa uweje ili sasa pengine hao wanaojaribu kuthibitisha waweze kujua huo uthibitisho unatakiwa uweje ili wajue wathibitishe kwa aina gani, kinyume na hivyo hakuna kitakachokubaliwa kama uthibitisho na madai ya kwamba hakuna uthibitisho yataendelea kuwepo.

Maana nilichogundua kwenye hili suala la uthibitisho ni kwamba hakuna idea hata huo uthibitisho unafananaje kitu kinachofanya ni ngumu kuweza kukubali kuwa huu ni uthibitisho.

Japo najua kinachomfanya atheist kupinga uwepo wa Mungu sio kutokuwepo kwa uthibitisho maana ingekuwa hivyo basi kusingetokea atheist kuja kuwa muamini Mungu hali ya kwamba bado uthibitisho hakuna.
Hivi nikikuambia kuwa katikati ya jua kuna chupa ya chai ya kimaajabu isiyoonekana inafanya rotation kulizunguka jua kila siku.

Halafu nikakuuliza unahitaji uthibitisho wa namna gani unaoweza kutimiza haja yako ya kukufanya ukubaliane na maelezo hayo.

Utanipa jibu gani?

Niambie namimi nijifunze.
 
Umesema mwenyewe mara kadhaa kuwa kama Mungu yupo aje ajisemee mwenyewe na kama kweli yupo ajitokeze, wakati wewe unasema kwa uhakika kuwa Mungu hayupo kuna wenye kusema hakuna namna ya kujua kuwa huyo Mungu yupo au hayupo, sasa unadhani wewe umewezaje kujua kuwa hayupo kwa uhakika?
Madai ya uwepo wa Mungu yametoka kwenu nyie waamini huyo Mungu.

Nyie waamini Mungu ndio mnapaswa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo.

Mkishindwa kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo, Ni kwamba madai yenu ni ya uongo.

Na huyo Mungu mnayedai yupo, HAYUPO.
 
Relax Mungu yupo
 
Back
Top Bottom