Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Huyo Mungu hayupo.Wapi Mungu kamuhitaji binaadamu kwa lolote? Kwamba kwa sababu wewe unasema hayupo basi yeye huko ajioneshe kwa watu kuwa yupo ili wewe uthibitishe uwepo wake ili iweje sasa?
Kuamini unaweza kuamini hata uongo.Ipo hivi mkuu, suala la Mungu ni la imani na si bahati mbaya bali ndio alivyotaka hivyo kuwepo wasioamini haiwezi kuwa ajabu ni lazima iwe hivyo maan kuamini ni hiari.
Sema unapaswa uweje? Nahitaji kujua.Nani kasema nataka kuthibitisha? Au umekariri tu kusema thibitisha ila hujui hata huo uthibitisho wa kuthibitisha huyo Mungu unapaswa uweje?
Sijasema unapaswa kuamini maana kuamini ni hiari ndio maana huwa nasema huwezi kumlazimisha mtu kuamini. Ila kuamini ni sehemu ya maisha yetu binaadamu sidhani kama kuna binaadamu asiye amini.Unahisi kwa nini napaswa kuamini na sio kujua?
Ok bora wewe umeweka wazi kwamba kumbe sababu ya kusema hakuna Mungu ni kwa kuwa haonekani ndio maana mnasema hayupo.Mnahangaika sana kumwelezea, kumtetea na kumuongelea Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe, kujitetea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe, Yeye kama yeye kwamba yupo.
Ni ninyi tu mnahangaika kufosi aonekane yupo, Kumbe hayupo.
Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe yupo kama ana huo uwezo.
Sio ninyi mumuhangaikie kumuelezea uwepo wake.
Biblia ni madai sio ushahidi.Biblia inaeleza mambo mengi kuhusu Mungu. Na Biblia imeandikwa na wanadamu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, ukisoma Biblia utajua habari za Mungu na unaweza kuwaelezea wengine wasiomjua Mungu.
Sio haonekani tu.Ok bora wewe umeweka wazi kwamba kumbe sababu ya kusema hakuna Mungu ni kwa kuwa haonekani ndio maana mnasema hayupo.
Kutumia Biblia kusema kwamba ndio uthibitisho wa uwepo wa Mungu ni sawa na kutumia hekaya za vitabuni kusema kwamba ndio uthibitisho wa uwepo wa Abunuwasi.Biblia inaeleza mambo mengi kuhusu Mungu. Na Biblia imeandikwa na wanadamu wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, ukisoma Biblia utajua habari za Mungu na unaweza kuwaelezea wengine wasiomjua Mungu.
Unafahamu kwamba huko Japan kuna dini inayoamini Mungu anayeitwa Erick???Mwalimu wangu wa falsafa wakati anatufundisha metaphysics alituambia kuwa " we know God through negation and affirmation". Kuwa ukisema Mungu hayupo hicho ni kinini unachosema hakipo?. Once you negates about God you prove His existence. Mujwahuzi the PhD .
Hujaeleza huo uthibitisho unatakiwa uweje ili sasa pengine hao wanaojaribu kuthibitisha waweze kujua huo uthibitisho unatakiwa uweje ili wajue wathibitishe kwa aina gani, kinyume na hivyo hakuna kitakachokubaliwa kama uthibitisho na madai ya kwamba hakuna uthibitisho yataendelea kuwepo.Okay
Nikikuambia kuwa nina vidole 10 kwenye mikono yote miwili, unaweza kuniamini bila hata kuhoji swali.
Lakini nikikuambia mbali na hivyo vidole 10, nina vidole viwili vya ziada kwenye kila mkono.
Pengine utashangaa na huwenda ukaamini labda i'm just born different.
Lakini nikaja na hii
Nikasema nina macho matatu kwenye paji la uso na kwenye kisogo so nauwezo wa kuona vision zote katika nyuzi 360.
Halafu nikakutumia na hii picha kama uthibitisho
View attachment 3188949
Je utakuwa satisfied na huo uthibitisho?
Bila shaka hautorudhika na ushahidi wa aina hiyo na utaomba ushahidi mwingine.
Kwa hiyo kadri unavyozidi kuelezea vitu ambavyo sio vya kawaida ndivyo jinsi ambavyo utahitaji kutoa uthibitisho mkubwa zaidi ku prove madai hayo.
The more extraordinary the claim, the more extraordinary the evidence that is required to demonstrate it.
Umesema mwenyewe mara kadhaa kuwa kama Mungu yupo aje ajisemee mwenyewe na kama kweli yupo ajitokeze, wakati wewe unasema kwa uhakika kuwa Mungu hayupo kuna wenye kusema hakuna namna ya kujua kuwa huyo Mungu yupo au hayupo, sasa unadhani wewe umewezaje kujua kuwa hayupo kwa uhakika?Sio haonekani tu.
Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.
Maana kuna vitu havionekani ila vipo, mfano upepo.
Mungu ni dhana ya kutungwa na kufikirika tu mliyo jitungia huko vichwani mwenu.
Mungu hayupo kwa namna yoyote ile.
Mungu ni jina uchwara tu mlilo jitungia.
Hivi nikikuambia kuwa katikati ya jua kuna chupa ya chai ya kimaajabu isiyoonekana inafanya rotation kulizunguka jua kila siku.Hujaeleza huo uthibitisho unatakiwa uweje ili sasa pengine hao wanaojaribu kuthibitisha waweze kujua huo uthibitisho unatakiwa uweje ili wajue wathibitishe kwa aina gani, kinyume na hivyo hakuna kitakachokubaliwa kama uthibitisho na madai ya kwamba hakuna uthibitisho yataendelea kuwepo.
Maana nilichogundua kwenye hili suala la uthibitisho ni kwamba hakuna idea hata huo uthibitisho unafananaje kitu kinachofanya ni ngumu kuweza kukubali kuwa huu ni uthibitisho.
Japo najua kinachomfanya atheist kupinga uwepo wa Mungu sio kutokuwepo kwa uthibitisho maana ingekuwa hivyo basi kusingetokea atheist kuja kuwa muamini Mungu hali ya kwamba bado uthibitisho hakuna.
Madai ya uwepo wa Mungu yametoka kwenu nyie waamini huyo Mungu.Umesema mwenyewe mara kadhaa kuwa kama Mungu yupo aje ajisemee mwenyewe na kama kweli yupo ajitokeze, wakati wewe unasema kwa uhakika kuwa Mungu hayupo kuna wenye kusema hakuna namna ya kujua kuwa huyo Mungu yupo au hayupo, sasa unadhani wewe umewezaje kujua kuwa hayupo kwa uhakika?
Hapana si kweli ... kama atahitaji chanzo ata kuwa sio Mungu tenaHiyo inaonesha kwamba hata Mungu naye anahitaji chanzo
Relax Mungu yupoMadai ya uwepo wa Mungu yametoka kwenu nyie waamini huyo Mungu.
Nyie waamini Mungu ndio mnapaswa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo.
Mkishindwa kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo, Ni kwamba madai yenu ni ya uongo.
Na huyo Mungu mnayedai yupo, HAYUPO.
Kama kutakuwa na exception kwenye kanuni yako basi tunaweza kuelezea hivyo hivyo ulimwengu kwa kuweka exception hiyo hiyo.Hapana si kweli ... kama atahitaji chanzo ata kuwa sio Mungu tena
Kama huongozwi na Mungu hii huezi elewaKama kutakuwa na exception kwenye kanuni yako basi tunaweza kuelezea hivyo hivyo ulimwengu kwa kuweka exception hiyo hiyo.