Mambo 12 niliyoyaona leo Simba Vs Coastal Union

Mambo 12 niliyoyaona leo Simba Vs Coastal Union

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
1. Kocha Fahdu na Jean Charles Ahoua ndio walioiua Simba leo, Ahoua yuko slow, mchoyo na hajui kupiga faulo, kila nikitoa maoni mnatukana leo mmeona

2. Jean Charles Ahoua kama ndio MVP ligi ya kwao basi Ditram Nchimbi ana uwezo wa kucheza soka Ivory Coast

3. Kama Simba ingecheza na timu nzuri leo tungeongea mengine jioni wala sio sare

4. Uchezaji wa timu uko slow sanaaaa tofauti na Simba ile ya kasi

5. Joshua Mutale mpelekeni Ken Gold huko

6. Augustine Okajepha nakubali ni kiungo wa maana kabisa

7. Hivi chasambi na Karabaka hata leo mechi mbovu kabisa mmeshindwa kuwapanga?

8. Leonel Ateba Mbida anashindwa kufunga kwa sababu Ahoua mbinafsi sana

9. Kila mchezaji leo alikuwa anacheza kivyake wala hakukuwa na mfumo wowote

10. Mikoani kugumu sana, kocha wetu anaweza kudondosha point kizembe kabisa kama hatobadilika na mbinu zake za mwaka 1970.

11 Mwisho wa yote Simba haina mafia nje ya uwanja, leo wametegwa na wakategeka, mpango ulianzia Dodoma na bado wataendelea kutupiga pini

12. Nina uhakika tutashika nafasi ya 2 tena msimu huu kwa kocha huyu mchovu.

Soma Pia: FT: Simba SC 2-2 Costal Union | NBC Premier League | KMC Complex | 4 Octoba, 2024
 
Naunga mkono 100% namba 8......

Katampigisha sana shoti kocha hako katoto....na Balua...
 
Refa kawaokoa ilibidi ziwe 3, kapuliza filimbi wakati coastal anakaribia kufunga
 
Timu haijajengwa ikakakaa sawa, bado nafasi lukuki zinahitaji kusajili wachezaji wenye viwango vinavyoendana na timu.

Unasare na coastal union wakati huo huo unatarajia kuwa bingwa wa ligi!!
 
Tatizo la SIMBA ni kivimmba kichwa kwa wachezsji. Wanasifiwa hadi wanajisahau. Hawana Spirit force ya kupigania timu. Watazame yanga walivyo na spirit, na wakifika karbu na goli ndo hatari zaidi .
Leo yamekuwa hayo tena? Si mlikuwa mnasema Yanga ya kagoli kamoja hakuna kitu pale!
 
Back
Top Bottom