Mambo 15 niliyoyaona Simba ikiiangamiza Fountain Gate leo

Kwa moto ambao simba wameanza nao, nawaona kabisa wakijihakikishia kushika nafasi ya 3
 
ila sio fountain gate kuwa na kikosi nusu. sababu foreign players wote awakucheza. sema na kocha wa fountain gate ni tapeli. kipa mfupi. hii simba ni mbovu. sema najua wapi mwisho wenu Tripoli 13 September,

Huyo kipa si ndiyo alikuwa Ihefu, kuna ile mechi alikaza sana akaja kuwazawadia goli baada ya kumpasia mpira Mayele akiwa nyuma yake. Ni kipa mzuri na anajiamini sana, sijaona ufupi wake kumsumbua.
 
Kama vital o tu
“SIMBA WAMEIFUNGA FOUNTAIN GATE FC B MAANA WACHEZAJI WA KIKOSI CHA KWANZA WAMEKOSA LESENI” @issambuzi_tz Afisa Habari wa Fountain Gate FC baada ya kukandwa na Simba 😂😂😂😂🎥 @tvetanzania #mwamuziwakati
 
6 na 11 nimependa. 6 nimecheka mno na 11 umefafanua vizuri sana kama vile ni mchambuzi huru. Nina wasiwasi Mavambo ataondoka mapema sana kwenda Ulaya.

Ova
Kuweni na shukrani jamani, kweli leo Chama ni wa kumnanga kwamba ana kiguu kibovu?
Binadam wabaya sana!
 
Nikupinge kwasababu sina akili au?!

Heshima kwako.

Kila siku nawaambia raia, hii Simba SC chemistry ikikubali, kocha akajua mchezaji wake bora wa kila nafasi ni yupi, mfano hapo kwa Mzamiru, wajuaji watalia sana.
 
“SIMBA WAMEIFUNGA FOUNTAIN GATE FC B MAANA WACHEZAJI WA KIKOSI CHA KWANZA WAMEKOSA LESENI” @issambuzi_tz Afisa Habari wa Fountain Gate FC baada ya kukandwa na Simba 😂😂😂😂🎥 @tvetanzania #mwamuziwakati
Hivi hizo issue za lesseni mnazijua nyie tuu wachambuzi uchwara au hata TFF wanazijua? Timu iko ligi kuu inajua nini cha kufanya. Timu isilaumu wengine kwa matatizo yake yenyewe!.
Msimu uliopita tabora vs Azam, tabora walicheza pungufu but hamkuja na uchambuzi manyaunyau...kaeni kwa kutulia, timu iko ligi kuu na sio championship. 😆
 
1. Kipa wa Simba ana utulivu sana ni moja ya makipa bora kabisa ambao Simba msimu huu tunajivunia

2.Abdulrazak Hamza nimewaona akina Costa, Deo Njohole, Nico Bambaga wakati fulani akicheza namba nne, hata marehemu Method Mogella, Juma Limonga, Fikiri Magoso, Godwin Aswile, Mustafa Hoza, Juma Nyosso, ila dogo huyu ana utulivu sana ila aongeze spidi anapozidiwa mbio

3.Mzamiru Yassin hana uwezo wa kumweka benchi Yussuf Kagoma wala Augustine Okajepha, tunakosa kumaliza mchezo mapema kwa sababu yake, mechi tuliyofungwa na Yanga ni yeye alijisahau wakati Dube anagongeana Max Nzengeli, kila mechi na Yanga anachomesha yeye, namba 6 haiwezi, kwa sasa anapaswa kucheza dakika 10 za mwisho.

4.Yussuf Kagoma ndugu zanguni ni mtu makini sana, leo ndio mchezo wake wa kwanza lakini amedhihirisha kuwa Mwigulu Nchemba yuko nyuma ya matukio sana, pengine majukumu yamembana.Huyu kama Okajepha haanzi basi aanze yeye na sio Mzamiru.

5.Che Malone Fondoh ni kitasa kweli kweli ila aongeze umakini anajisahau sahau kidogo

6.Debora Mavambo Fernandez kila mtu ameona, kumlilia au kumkumbuka Chama na kiguu chake kibovu ni ulofa wa kiwango cha Chuo Kikuu.Huyu mtu aliyemsajili Mungu ambariki sana.

7.Valentino Mashaka ni mzuri lakini ajitahidi kupunguza uzito, anafunga mabao lakini uzito unamwelemea sana.

8.Fabrice Mwamba Ngoma aambiwe aongeze mazoezi mara 10, Kagoma na Okajepha ni habari nyingine

9.Jeans Charles Ahoua ameanza kujitafuta kidogo kidogo, aambiwe kazi yake sio kufunga ni kumlisha Mukwala, kufunga iwe Coincidence tu.

10.Kama Fahdu leo angemwenzisha Kagoma namba sita tangu mwanzo, nane Fernandes, 10 Awesu, wallahi Fountain Gate leo angeliwa 10.

11.Tofauti kubwa ya Simba na Yanga iko hivi, Yanga wanamtegemea sana Aziz Ki, jamaa ana uwezo mkubwa wa soka, amekamilika haswa mwanaume huyu sio masihara, Yanga wanapata taabu sana Aziz Ki akiwa nje, akiingia mambo yanabadilika sana, sisi Simba baada ya kuondoka Chama hilo halipo tena, timu imejengwa kama system vile, ukiondoka wewe mtu yupo.Yaani mchezaji anafanyiwa sub sio kwamba kachoka hapana, sub inafanyika kwa sababu wenzako wanataka nao kucheza.

12.Kocha Fahdu aendelee kuelekeza wachezaji waongeze Pressing maana kule Libya shughuli yake sio ndogo, tunahitaji kujipanga ili kuvuka makundi

Soma Pia: FT: Simba SC 4-0 Fountain Gates FC | NBC Premier League | KMC Complex | 25.08.2024

13.Mukwala ni mshambuliaji hatari sana, movement zake, vurugu, control, balance zinaonyesha ni mtu kuliko Fredy, kinachotakiwa ni Ahoua akipata mpira amwangalie tu yuko wapi ili amtemee

14.Kuna jitu halijacheza leo linaitwa Ateba, ngojeni liingie siku moja muone balaa lake

15.Wana Simba we have a good, good team, we have the quality players, tuamini mchakato, msibishane nao, hao akina Mzengeli, Chama, Pacome, Aucho umri umewatupa mkono hao.
16. Wachezaji wa kigeni wa singida fountain gate hawakucheza, reasons best know by TFF, (TFF wanasababu nzuri zaidi).
 
Namba 2 nakukatalia, bado tuna mechi nyingi za kudhiilisha uwezo wake.
Mzamiru sijui godfather wake ni nani, Hana utulivu, anapiga mapasi marefu haelewi hii ni Simba siyo yanga ingawa nayo imebadilika.
Kocha awape nafasi kina Chasambi na siyo kukariri wachezaji.
Kwa Chasamabi umenigusa na mimi. Huyo dogo ndio favorite player wangu katika timu ya Simba. Sijui kwa nini Kocha anamwacha nje.
 
1. Kipa wa Simba ana utulivu sana ni moja ya makipa bora kabisa ambao Simba msimu huu tunajivunia

2.Abdulrazak Hamza nimewaona akina Costa, Deo Njohole, Nico Bambaga wakati fulani akicheza namba nne, hata marehemu Method Mogella, Juma Limonga, Fikiri Magoso, Godwin Aswile, Mustafa Hoza, Juma Nyosso, ila dogo huyu ana utulivu sana ila aongeze spidi anapozidiwa mbio

3.Mzamiru Yassin hana uwezo wa kumweka benchi Yussuf Kagoma wala Augustine Okajepha, tunakosa kumaliza mchezo mapema kwa sababu yake, mechi tuliyofungwa na Yanga ni yeye alijisahau wakati Dube anagongeana Max Nzengeli, kila mechi na Yanga anachomesha yeye, namba 6 haiwezi, kwa sasa anapaswa kucheza dakika 10 za mwisho.

4.Yussuf Kagoma ndugu zanguni ni mtu makini sana, leo ndio mchezo wake wa kwanza lakini amedhihirisha kuwa Mwigulu Nchemba yuko nyuma ya matukio sana, pengine majukumu yamembana.Huyu kama Okajepha haanzi basi aanze yeye na sio Mzamiru.

5.Che Malone Fondoh ni kitasa kweli kweli ila aongeze umakini anajisahau sahau kidogo

6.Debora Mavambo Fernandez kila mtu ameona, kumlilia au kumkumbuka Chama na kiguu chake kibovu ni ulofa wa kiwango cha Chuo Kikuu.Huyu mtu aliyemsajili Mungu ambariki sana.

7.Valentino Mashaka ni mzuri lakini ajitahidi kupunguza uzito, anafunga mabao lakini uzito unamwelemea sana.

8.Fabrice Mwamba Ngoma aambiwe aongeze mazoezi mara 10, Kagoma na Okajepha ni habari nyingine

9.Jeans Charles Ahoua ameanza kujitafuta kidogo kidogo, aambiwe kazi yake sio kufunga ni kumlisha Mukwala, kufunga iwe Coincidence tu.

10.Kama Fahdu leo angemwenzisha Kagoma namba sita tangu mwanzo, nane Fernandes, 10 Awesu, wallahi Fountain Gate leo angeliwa 10.

11.Tofauti kubwa ya Simba na Yanga iko hivi, Yanga wanamtegemea sana Aziz Ki, jamaa ana uwezo mkubwa wa soka, amekamilika haswa mwanaume huyu sio masihara, Yanga wanapata taabu sana Aziz Ki akiwa nje, akiingia mambo yanabadilika sana, sisi Simba baada ya kuondoka Chama hilo halipo tena, timu imejengwa kama system vile, ukiondoka wewe mtu yupo.Yaani mchezaji anafanyiwa sub sio kwamba kachoka hapana, sub inafanyika kwa sababu wenzako wanataka nao kucheza.

12.Kocha Fahdu aendelee kuelekeza wachezaji waongeze Pressing maana kule Libya shughuli yake sio ndogo, tunahitaji kujipanga ili kuvuka makundi

Soma Pia: FT: Simba SC 4-0 Fountain Gates FC | NBC Premier League | KMC Complex | 25.08.2024

13.Mukwala ni mshambuliaji hatari sana, movement zake, vurugu, control, balance zinaonyesha ni mtu kuliko Fredy, kinachotakiwa ni Ahoua akipata mpira amwangalie tu yuko wapi ili amtemee

14.Kuna jitu halijacheza leo linaitwa Ateba, ngojeni liingie siku moja muone balaa lake

15.Wana Simba we have a good, good team, we have the quality players, tuamini mchakato, msibishane nao, hao akina Mzengeli, Chama, Pacome, Aucho umri umewatupa mkono hao.
Acha kufananisha Yanga na vitu vya kijinga.
 
Back
Top Bottom