Mambo 15 niliyoyaona Simba ikiiangamiza Fountain Gate leo

Mambo 15 niliyoyaona Simba ikiiangamiza Fountain Gate leo

1. Kipa wa Simba ana utulivu sana ni moja ya makipa bora kabisa ambao Simba msimu huu tunajivunia

2.Abdulrazak Hamza nimewaona akina Costa, Deo Njohole, Nico Bambaga wakati fulani akicheza namba nne, hata marehemu Method Mogella, Juma Limonga, Fikiri Magoso, Godwin Aswile, Mustafa Hoza, Juma Nyosso, ila dogo huyu ana utulivu sana ila aongeze spidi anapozidiwa mbio

3.Mzamiru Yassin hana uwezo wa kumweka benchi Yussuf Kagoma wala Augustine Okajepha, tunakosa kumaliza mchezo mapema kwa sababu yake, mechi tuliyofungwa na Yanga ni yeye alijisahau wakati Dube anagongeana Max Nzengeli, kila mechi na Yanga anachomesha yeye, namba 6 haiwezi, kwa sasa anapaswa kucheza dakika 10 za mwisho.

4.Yussuf Kagoma ndugu zanguni ni mtu makini sana, leo ndio mchezo wake wa kwanza lakini amedhihirisha kuwa Mwigulu Nchemba yuko nyuma ya matukio sana, pengine majukumu yamembana.Huyu kama Okajepha haanzi basi aanze yeye na sio Mzamiru.

5.Che Malone Fondoh ni kitasa kweli kweli ila aongeze umakini anajisahau sahau kidogo

6.Debora Mavambo Fernandez kila mtu ameona, kumlilia au kumkumbuka Chama na kiguu chake kibovu ni ulofa wa kiwango cha Chuo Kikuu.Huyu mtu aliyemsajili Mungu ambariki sana.

7.Valentino Mashaka ni mzuri lakini ajitahidi kupunguza uzito, anafunga mabao lakini uzito unamwelemea sana.

8.Fabrice Mwamba Ngoma aambiwe aongeze mazoezi mara 10, Kagoma na Okajepha ni habari nyingine

9.Jeans Charles Ahoua ameanza kujitafuta kidogo kidogo, aambiwe kazi yake sio kufunga ni kumlisha Mukwala, kufunga iwe Coincidence tu.

10.Kama Fahdu leo angemwenzisha Kagoma namba sita tangu mwanzo, nane Fernandes, 10 Awesu, wallahi Fountain Gate leo angeliwa 10.

11.Tofauti kubwa ya Simba na Yanga iko hivi, Yanga wanamtegemea sana Aziz Ki, jamaa ana uwezo mkubwa wa soka, amekamilika haswa mwanaume huyu sio masihara, Yanga wanapata taabu sana Aziz Ki akiwa nje, akiingia mambo yanabadilika sana, sisi Simba baada ya kuondoka Chama hilo halipo tena, timu imejengwa kama system vile, ukiondoka wewe mtu yupo.Yaani mchezaji anafanyiwa sub sio kwamba kachoka hapana, sub inafanyika kwa sababu wenzako wanataka nao kucheza.

12.Kocha Fahdu aendelee kuelekeza wachezaji waongeze Pressing maana kule Libya shughuli yake sio ndogo, tunahitaji kujipanga ili kuvuka makundi

Soma Pia: FT: Simba SC 4-0 Fountain Gates FC | NBC Premier League | KMC Complex | 25.08.2024

13.Mukwala ni mshambuliaji hatari sana, movement zake, vurugu, control, balance zinaonyesha ni mtu kuliko Fredy, kinachotakiwa ni Ahoua akipata mpira amwangalie tu yuko wapi ili amtemee

14.Kuna jitu halijacheza leo linaitwa Ateba, ngojeni liingie siku moja muone balaa lake

15.Wana Simba we have a good, good team, we have the quality players, tuamini mchakato, msibishane nao, hao akina Mzengeli, Chama, Pacome, Aucho umri umewatupa mkono hao.
Mchezaji wa maana pale Simba ni Debora tu, Kipa wa Simba ana ubora kwa kuweza kutumia miguu vizuri ila akikutana na timu nzuri ni mweupe kwenye one on one.
Ayubu si mzuri mguuni lakini one vs one Yuko mbali sana Kwa Camara.

Rejea Yanga vs Simba, kipa Camara zile one vs one zote zilimshinda, ukianza na Dube, Camara alizidiwa maarifa sema mpira uka gonga mwamba, akaja Max akampiga tobo, akaja Aziz k akalambishwa nyasi, akaja Pacome akalambishwa nyasi.

Kwa ujumla Camara ni mzuri kwenye taiming ya kutoka golini na kucheza mpira kwa miguu yote ila kwenye one vs one ni mweupe kuliko ata Ali Salim.

Kwenye kiungo Cha Simba Debora ni mtamu ila baada ya yeye anayefuatia Mzamiru kwa kuzuia ni Mzamiru alafu kagoma alafu Ngoma.

Kwenye maamuzi ya ushambulizi kutokea kwenye kiungo wa Chini ana Anza Ngoma, Debora na Mzamiru wako sawa kwenye kushanbulia na kagoma wa mwisho.

Namba 10 Ahoa ni kama Saidoo Tena Saidoo ni mzuri zaidi kwakua Ahoa yeye option yake ya kwanza ni kupiga golini na hana shabaha, katika mipira mitano anaweza kulenga Goli mar 2.
Mshambuliaji wa kati hakuna, anahitaji nafasi 3/4 akupe goli.
Nafasi nyingi kama izo atazipata kama mkicheza na timu dhaifu tu.
Kwa ujumla mpaka Sasa Simba si timu ya kugombea Ubingwa ila inaonuweso wa ku maintain nafasi ya tatu.

Mabeki wa kati wote wa Simba Wana Nguvu ila wazito wakikutana na washambuliaji wepesi ni mtihani labda refa aingilie kati kama ilivyotokea katika mechi ya Simba na Yanga.
 
Jipige kifua na ujisemee kuwa ww ni tikiti maji
 
Namba 2 nakukatalia, bado tuna mechi nyingi za kudhiilisha uwezo wake.
Mzamiru sijui godfather wake ni nani, Hana utulivu, anapiga mapasi marefu haelewi hii ni Simba siyo yanga ingawa nayo imebadilika.
Kocha awape nafasi kina Chasambi na siyo kukariri wachezaji.
Hizo pasi ndefu ulikuwa huoni zinavyofika kwa Shabalala?
 
SImba ilicheza kama kwenye kideo. Yanga Makopo ameanza kutetemeka. Na hapa bado simba inajitafuta.
 
Back
Top Bottom