Mambo 15 niliyoyaona Simba vs Al Hilal leo

Mambo 15 niliyoyaona Simba vs Al Hilal leo

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
1. Aishi Manula amebadilika na hasa anapowaiga Mussa Camara na Diarra kutembea na mpira, anastahili mkataba mpya

2. Kapombe jamani amepungua sana kama sio umakini wa Manula leo ingekuwa aibu

3. Valentine Nouma ni mchezaji wa kawaida sana, anachojua yeye ni mashuti tu lakini kukaba zero.

4. Chamou Karaboue apunguze uzito halafu aachane na mpira wa akina Salum Kabunda Ninja au Abdallah Msheli au Juma Nyosso.

5. Hamza ni mzuri lakini ana mapungufu kwanza yuko slow then hana speed

6. Che Malone apunguze utoto atakuja kuigharimu timu hatutamwelewa

7. Yussuf Kagoma ndio aina ya viungo wanaotakiwa, anarusha mipira ya mbali ili mawinga wakimbize, ila ana tabia za Tadeo Lwanga mtupu.

8. Debora Mavambo amefaulu mtihani wote utadhan tulitunga wote.

9. Augustine Okajepha ni aina ya viungo wa kisasa kabisa sijui kocha ana tatizo naye gani?

10. Chasambi anahitaji kucheza zaidi ili kuiletea mafanikio Simba

11. Kibu Denis namkubali sana na ndio tegemeo langu mimi hata kama alizingua kwenye usajili.

12. Valentine Mashaka apunguze uzito awe fiti zaidi.

13. Lionel Ateba ni Joseph Kaniki Golota mtupu.

14. Joshua Mutale ni Issa Kihange mtupu

15. Awesu Awesu ameikosea nini nchi hii hadi anaachwa timu ya Taifa? Yaan akina Mudathir sijui andambwile ndio wamweke benchi Awesu, Hemed Morocco unamkosea sana kiungo huyu mwenye udambwi udambwi mwingi kama enzi zile Michael Paul au Nylon.
 
Huu uchambuzi utadhani ni timu ya Madrid kumbe ni kombe la losers.
 
Simba inasubiri muunganiko utakuwa umeagizwa toka South Africa na Fadlu, bado uko njiani, labda Dec utafika bandarini DP World, kwasasa wanacheza rede tu! Hamna kitu pale mbumbumbu street!

Mbumbumbu leo mpira mdogo sana, ulikuwa mpira wa ndondo tu, Al Hilal walikuwa kumi tu uwanjani na goli likarudi je wangebaki 11 hadi mwisho naamini huu uchambuzi ungesema vingine km kawaida tumekufa kiume, tunasaka first eleven, tuna test mitambo nk!!
 
Nachoona Chasambi ni bonge la mchezaji, Ngoma bado anahitajika hamna kiungo anayepigwa pasi za mwisho vizuri, back pass zimekuwa nyingi, kocha tumpe muda Ila Kuna maswali mengi ya kujiuliza juu yake.
 
Simba hawana kocha,,, Nina wasiwasi Sana na mbinu zake na namna anavyoweza kusoma mchezo kwa haraka
 
Simba hawana kocha,,, Nina wasiwasi Sana na mbinu zake na namna anavyoweza kusoma mchezo kwa haraka
Mara hawana wachezaji mara hawana kocha. Ogopa supu ya vibudu akili inahama kabisa. Basi tufanye hivi Timu namba 7 Kwa ubora Africa haipo kabisa ni story Tu.🙄
 
Yaani mna mnacheza na wakimbizi ambao hawana ligi na walikuwa kumi bado wachezaji wengi wamekimbia then mnashindwa kupata ushindi!

Simba ni hasara
 
Back
Top Bottom