Mambo 15 ya kufanya kupata hati mpya ya kusafiria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Idara ya Uhamiaji imetoa maelekezo ya kujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao.
Msemaji wa Uhamiaji, Ally Mtanda amesema leo Februari 9, 2018 kuwa fomu hizo zipo kwa Kiswahili na kusisitiza kuwa mwombaji anapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa ili kukidhi moja ya sharti muhimu.

“Maombi kwa sasa ni mengi, changamoto ni baadhi ya waombaji kutokuwa na vitambulisho vya Taifa ambavyo sasa wanaona umuhimu wake na kulazimika kuvifuata Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa),” amesema Mtanda.

Pia, amesema muda ambao utatumika hadi mwombaji kupata hati yake ya kusafiria ni chini ya siku 14 za kazi ingawa hakubainisha ni siku ngapi.

Amesema mwombaji anayehitaji kupata hati hiyo, kwanza anapaswa kuingia katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz na kisha kwenda katika kitufe cha e-Services.

Pili, mwombaji atapaswa kuchagua fomu ya maombi ya hati. Tatu, kuchagua ombi jipya, nne, atatakiwa kutiki kiboksi kukubaliana na maelekezo na tano anaanza kujaza taarifa zake kwa ukamilifu ukifuata maelekezo na mpangilio katika kila kipengele.

Baada ya mwombaji kukamilisha kujaza taarifa zake, atafahamishwa ya kwamba usajili umekamilika na kupatiwa namba ya ombi, ambayo ni muhimu aiandike pembeni na kuihifadhi kwa kumbukumbu za baadae.

Amesema mwombaji atapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na kutakiwa kwenda kulipia malipo ya awali Sh20,000.

Mtanda amesema baada ya mwombaji kumaliza hatua hiyo, ukurasa huo, ataingia katika menu ya M-Pesa/Tigopesa (*150*00#/*150*01#).

Amesema baada ya hapo atatakiwa kubonyeza namba 4 (lipa kwa M-Pesa) au kubonyeza namba 4 (kulipia bili)-Tigo na baada ya kuchagua mtandao wa malipo, atatakiwa kuingiza namba ya kampuni 888999.

Mwombaji pia atatakiwa kuingiza kumbukumbu namba (Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….), kisha kiasi (kama ilivyo elekezwa Mfano: 20,000), atapata maelezo kuwa unalipa pesa NMB, baada ya hapo ataingiza namba ya siri, atahakiki na kupata ujumbe mfupi wa maneno kutoka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika.

Amesema baada ya hatua hiyo mwombaji atapata ujumbe kutoka kwenye mfumo namba 15200 kama muamala umekubalika, kisha kurudi katika ombi linaloendelea na mwisho ataingiza namba ya ombi au simu na namba ya risiti na hapo atapakua fomu yake ya maombi.

Mtanda amesema baada ya kuwa amepata fomu atatakiwa kuiwasilisha katika Ofisi ya Uhamiaji makao makuu au Ofisi Kuu Zanzibar.

Amesema malipo hayo yanaweza kufanyika pia kwa njia ya benki NMB/CRDB ambapo mwombaji atapaswa kujaza fomu ya malipo ya kielectroniki, kufuata maelekezo kama yanavyojieleza kwenye fomu, atapata meseji kutoka benki na kwenye mfumo namba 15200 kama muamala umekubalika.

mwananchi
 
Mkuu sasa kuhusu kitambulisho cha taifa inakuaje hapo maana wengi bado hawana vitambulisho vya taifa baada ya vile vya zamani kupigwa chini na mamlaka
 
Mm nauliza hivi kama mfano mtu ambaye passport yake.ya zaman iliungua moto bahat mbaya na akaja kushtukia tayari ni.majivu je mtu huyu anaweza je kupatiwa passport mpya? Na je ikiwa namba za ile iliyoungua anazo huyu mtu atapewa passport yenye namba ingine ama ile ile?
 
Mkuu sasa kuhusu kitambulisho cha taifa inakuaje hapo maana wengi bado hawana vitambulisho vya taifa baada ya vile vya zamani kupigwa chini na mamlaka
Je ofisi za nida hizi ktk Kila wilaya zinafanya kazi?
 
nimelipia toka jana iyo elf 20 na msg kutoka tigo pesa imekuja ila mpaka sasa iyo msg ya kwenye system sijapata na ukipiga tigopesa wanasema wao kazi yao ishakamilika muamala hauko kwao sasa sijui nafuatilia wapi kutokea apo au ndo nmb au uhamiaji au niendelee kuwait tu...... na hamna namba ya kupiga kuulizia why sijapata iyo msg ya kutoka 15200
 
Kulipia kwa njia ya mpesa na tigopesa inazingua sana...iv ni njia ipi nzur ya kukuwezesha kulipia hiz passport??
 
Ivi nomba kujua kqenye kujaza fomu ile sehem ya tarifa ya safari kama huna barua yeyote ya mualiko...kwan ni lazima ijazwe???
 
Mbona hayo mambo 15 sijayaona jamani!!
 
Idara ya Uhamiaji imetoa maelekezo ya kujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao.
Msemaji wa Uhamiaji, Ally Mtanda amesema leo Februari 9, 2018 kuwa fomu hizo zipo kwa Kiswahili na kusisitiza kuwa mwombaji anapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa ili kukidhi moja ya sharti muhimu.

“Maombi kwa sasa ni mengi, changamoto ni baadhi ya waombaji kutokuwa na vitambulisho vya Taifa ambavyo sasa wanaona umuhimu wake na kulazimika kuvifuata Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa),” amesema Mtanda.

Pia, amesema muda ambao utatumika hadi mwombaji kupata hati yake ya kusafiria ni chini ya siku 14 za kazi ingawa hakubainisha ni siku ngapi.

Amesema mwombaji anayehitaji kupata hati hiyo, kwanza anapaswa kuingia katika tovuti ya Idara ya Uhamiaji www.immigration.go.tz na kisha kwenda katika kitufe cha e-Services.

Pili, mwombaji atapaswa kuchagua fomu ya maombi ya hati. Tatu, kuchagua ombi jipya, nne, atatakiwa kutiki kiboksi kukubaliana na maelekezo na tano anaanza kujaza taarifa zake kwa ukamilifu ukifuata maelekezo na mpangilio katika kila kipengele.

Baada ya mwombaji kukamilisha kujaza taarifa zake, atafahamishwa ya kwamba usajili umekamilika na kupatiwa namba ya ombi, ambayo ni muhimu aiandike pembeni na kuihifadhi kwa kumbukumbu za baadae.

Amesema mwombaji atapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na kutakiwa kwenda kulipia malipo ya awali Sh20,000.

Mtanda amesema baada ya mwombaji kumaliza hatua hiyo, ukurasa huo, ataingia katika menu ya M-Pesa/Tigopesa (*150*00#/*150*01#).

Amesema baada ya hapo atatakiwa kubonyeza namba 4 (lipa kwa M-Pesa) au kubonyeza namba 4 (kulipia bili)-Tigo na baada ya kuchagua mtandao wa malipo, atatakiwa kuingiza namba ya kampuni 888999.

Mwombaji pia atatakiwa kuingiza kumbukumbu namba (Ingiza Control Number inayoanzia na 99109…….), kisha kiasi (kama ilivyo elekezwa Mfano: 20,000), atapata maelezo kuwa unalipa pesa NMB, baada ya hapo ataingiza namba ya siri, atahakiki na kupata ujumbe mfupi wa maneno kutoka M-Pesa/Tigopesa kama muamala umekubalika.

Amesema baada ya hatua hiyo mwombaji atapata ujumbe kutoka kwenye mfumo namba 15200 kama muamala umekubalika, kisha kurudi katika ombi linaloendelea na mwisho ataingiza namba ya ombi au simu na namba ya risiti na hapo atapakua fomu yake ya maombi.

Mtanda amesema baada ya kuwa amepata fomu atatakiwa kuiwasilisha katika Ofisi ya Uhamiaji makao makuu au Ofisi Kuu Zanzibar.

Amesema malipo hayo yanaweza kufanyika pia kwa njia ya benki NMB/CRDB ambapo mwombaji atapaswa kujaza fomu ya malipo ya kielectroniki, kufuata maelekezo kama yanavyojieleza kwenye fomu, atapata meseji kutoka benki na kwenye mfumo namba 15200 kama muamala umekubalika.

mwananchi
Na watoto wa chini ya miaka mi5 wanatakiwa wawe na kitambulisho cha uraia ili wapate passport?
 
HAYA NI MAMBO 15....safi sana MAMBO 15 konki
 
Ndugu tayarisha kitambulisho cha NIDA, Cheti cha kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa cha baba au mama na kama hawana barua ya kiapo inahitajika, 150k. Hayo ndo ya msingi sana. Mengine kama sababu ya safari andaa maelezo then ingia mtandaoni jaza fomu na waibukie uhamiaji kwa kujiamini utapewa kitabu chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom