NCHI YANGU MIMI NI NGUMU KUIELEWA. WANAOIELEWA MNISADIE.
Hivi mtu umepambana na maform kibao mpaka ukapata ID ya NIDA, kwa akili yangu ndogo, nilijua huo usajili utakidhi mahitaji yote popote utakapohitaji usajili kusudi upewe huduma ya serikali. Kama Uhamiaji wanataka record zangu kwa nini wasilink moja kwa moja na NIDA? Uhamiaji wanatakiwa kuniita pale ambapo kuna mkanganyiko wa habari au wanataka/wana maswali kuhusu uraia wangu. Lakini hii inabidi iwe specific. Case by case.
Sasa huyo mtu/idara ya E-GOVERNMENT KAZI YAKE NI IPI HASWA???
Hata hii ya TCRA, mtu kama una kitambulisho cha NIDA (na tunafanya usajili kwa alama za vidole), ya nini kuhangaisha watu kwamba wakasajiliwe upya? Kiukweli hii bureaucracy ndo inasababisha upigaji wa pesa za serikali kwa sababu records za NIDA zingekuwa zinafanya kazi sehemu zote ambapo usajili unahitajika.
Siamini kwamba serikalini hakuna watu wenye akili kiasi hiki.
It is a total wastage of time and resources!
Wahusika lifanyieni kazi hili swala.