Mambo 17 yaliyosababisha kuuawa kwa Gadaffi

Mambo 17 yaliyosababisha kuuawa kwa Gadaffi

Hatutaki mizungu, miarabu wala Gaddafi mwenyewe.

Mtu aliyeisapoti Uganda wakati wa vita ya TZ na Uganda. Mtu aliyesapoti ugaidi na kulipa fidia kwanini tumtetee?

Walibya wenyewe walimchoka na kumuua ndo sisi tumsapoti. Acheni uzwazwa
Kumbe
 
“Kila mwananchi wa Libya aliyekosa ajira baada ya kuhitimu kulingana na kiwango alichofikia, Serikali ilimlipa mshahara unaokaribiana na mtu aliyeajiriwa mwenye elimu sawa na aliyonayo yeye.“ .. basi hakuna ambae angetafuta ajira kama ndo unalipwa salary bure hivi
 
Watu wangap wanatengenezwa na hao wamarekan kisha wanakuja kuvuruga nchi zao????ukiongozwa na misingi ya chuki za kidini ambao weng ndyo wapo hvyo huwezi ona tatizo....lkn ushenzi wa nchi za magharibi ukiongozwa na Marekani haujaanza leo na ugaid basi hakuna anaeweza kuishinda Marekan kwa matendo yake ya kigaidi karibu ulimwengu mzima

Jirani akikwambia muue baba yako na wewe ukakubali kumuua hapo mjinga ni wewe sio jirani aliyekushawishi. Kama baba yako ni mwema na una akili timamu huwezi kumuua utamkingia kifua.

Gaddafi alikufa mikononi mwa walibya wenyewe. Anything nyie outsiders say is irrelevant, mtawabebesha Marekani lawama zote ila Gaddafi aliuwawa na walibya wenyewe, angekua mwema sana walibywa wangekuwa wa kwanza kumtetea na hadi Leo ni nyie walibya wa ileje mnaomtetea huyo bwana ila walibya wenyewe husikii wakipiga kelele.
 
R.i.P Classmate...😥
Roho bado inaniuma hadi leo kwajinsi ulivyo sulubiwa na wanachi wako ulio wapenda, tena chini ya mtaro wa maji taka..😪
 
R.i.P Classmate...😥
Roho bado inaniuma hadi leo kwajinsi ulivyo sulubiwa na wanachi wako ulio wapenda, tena chini ya mtaro wa maji taka..😪
Kumbe tulikuwa darasa moja na wewe pia, looh. Za siku
 
View attachment 2970158

MAMBO 17 YALIYOSABABISHA KUUAWA KWA GADAFFI

1. LIBYA kulikuwa hakuna bili ya umeme, means umeme ulikuwa bure kwa raia wote
2. Libya kulikuwa hakuna Riba kwenye mikopo, Benk zote Libya zilikuwa za Umma na mikopo ilitolewa kwa raia wote tena bila Riba.
3. Gadafi alisisitiza kwamba, wazazi wake hawatapata nyumba nzuri hadi raia wote wa Libya wawe na makazi. Baba mzazi wa Gadafi amefariki wakati, yeye, mke wake na mama yake wakiishi kwenye hema.
4. Kila mfanyakazi Mpya (Mwajiriwa mpya) nchini Libya alipewa Dola za kimarekani 50,000 ili aanzie maisha.
5. Kabla ya Gadafi, kulikuwa na 25% tu ya raia wa Libya ndio walikuwa na Elimu.
6. Elimu na Huduma za Afya (matibabu) nchini LIBYA zilitolewa bure.
7. Kama Mwananchi wa LIBYA aliyehitaji kujishughulisha na kilimo, alipatiwa ardhi, nyumba, mbegu na mahitaji mengine yaliyohitajika.
8. Iwapo mwananchi wa Libya akishindwa kupata Elimu au Huduma ya Afya ndani ya LIBYA, serikali ilimsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya mahitaji hayo, pia alipewa Dola milioni 3 za kimarekani kwa ajili ya gharama .
9. LIBYA, Kila raia wa LIBYA aliyenunua gari, serikali ilimwongezea nusu ya bei ya gari, means kama gari itauzwa sh milioni tano, basi raia alilipia shilingi milioni mili na laki tano na kiasi kingine kinalipwa na serikali.
10. Bei ya Petrol nchini LIBYA ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.14
11. Libya ilikuwa haina madeni ya Nje, ilikuwa haidaiwi na nchi yoyote na ilikuwa imehifadhi dola za kimarekani bilioni 150
12. Kila mwananchi wa Libya aliyekosa ajira baada ya kuhitimu kulingana na kiwango alichofikia, Serikali ilimlipa mshahara unaokaribiana na mtu aliyeajiriwa mwenye elimu sawa na aliyonayo yeye.
13. Sehemu ya mauzo ya mafuta nchini Libya ilipelekwa moja kwa moja kwenye akaunti za benki za kila raia wa LIBYA
14. Kila mwanamke aliyejifungua, alipewa Dola za kimarekani 5,000
15. Gharama ya mikate arobaini ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.15
16. 25% ya raia wa LBYA walikuwa na kiwango cha Elimu cha SHAHADA (a university degree)
17. GADAFFI aliaanzisha mradi mkubwa zaidi kuwai kutokea duniani, mradi wa Umwagiliaji uliojulikana kama MAN- MADE RIVER PROJECT, Mradi uliowezesha upatikanaji wa maji eneo zima la jangwa.
Kama huu uliitwa “UDIKTETA” Basi WANADEMOCRASIA wote watakwenda Motoni
Sio kweli DOLA 50000 haikuwa inatolewa kwa kila mwajiriwa mpya isipokuwa kwa Usalama wake wa taifa na usilolijua Gadafi alikuwa anazini na mabikira wengi toa upuz
 
HAKIKA NAMCHUKIA GAIDI GADAFI,,, BABU YANGU AKIWA LINDO WAKATI WA VITA YA UGANDA VS TZ AKIWA NA SECTION YAKE WALIPAMBANA NA MAGAIDI WA GADAFI WALIOKUWA WANAWAPELEKEA SILAHA UGANDA NDIPO WALIPOSHIKWA NA BABU YANGU ALIKUWA KIONGOZI SECTION TRAINII NDIPO ALIPOANZA KUWAHOJI MLINZI WA GADAFI AKATAMKA MANENO YAO MNAYAJUA KUSHTUKA BOMU MOJA MATATA ALILOKUWA AMEVAA GAIDI LIKA....
 
Wadanganye watoto, et mwanafunzi apewe dollar million 3 za Marekani? Mgonjwa apewe dollar million 300 za Marekani, asee we jamaa wadanganye watoto
 
Back
Top Bottom