Mambo 20 ya kumuambia mpenzi wako Kila siku

Mambo 20 ya kumuambia mpenzi wako Kila siku

"Kama malaika wanapaswa kuwepo peponi, sijajua ww unafanya nini hapa duniani"

Nimegundua wanawake wanapenda sana kuongopewa
 
Unaweza Sema yote hayo na usijipe asilimia zote kua uta win NI Mara chache saana mkuu..heading haikawii kubadilika sometimes "Asikwambie mtu tutu..😃
 
Wakati kijana uko kwenye process ya kutafuta na kujaribu kuuteka moyo wa msichana, unatakiwa kujifunza kutumia maneno matamu. Na lazima ujue kuwa sio kila neno unalotumia litagusa moyo wa mwanamke unayemtaka, Lakini maneno matamu yanafanya kazi ya kushangaza.

Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. Watu wengi pia huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza.

Sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unayempenda na unahitaji awe wako milele;
1. Macho yako ni mazuri, yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama.

2, Unanifanya niwe mwanaume bora, kwa hio nastahili mapenzi yako.

3. Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu.

4. Wewe ni mzuri na ni mrembo naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua.

5. Unapotabasamu huzuni kwangu hupotea, ghafla nakuwa mtu wa furaha.

6. Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani, lakini umenichagua mimi.

7. Hapana wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo.

8. Ninapokushika nahisi kulegea kwenye magoti.

9. Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako, ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu.

10. Siamini, maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi.

11. kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda, natamani niwe na wewe milele. yaani usife.

12. Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja.

13. Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda, nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia.

14. Kukutana nawe ni kitu ambacho hakijawahi kutokea.

15. Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia, hapo hupotea kabisaaa.

16. Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi.

17. Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama haitatosha kukupenda.

18. Napata furaha nikiwa na wewe.

19. Napenda kutumia muda na wewe.

20. Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa.
Lakin kabla haujamuambia mwanamke maneno haya ni vizuri umjue mwanamk uliyenaye ni wa aina gani asilimia kubwa haya uliyoyaandika hapa yanapendelewa zaidi na wanawake ambao hawajakuwa kiakili
 
Hizo maneno zingekuwa kwa kingereza ingekuwa romantic kweli ila kiswahili utakesha,kingereza buana hunogesha penzi mnajikuta tu mnalainikaaa
 
Biyo namba 3 kuhusu tumbo ni tumbo lip walinenea. Yaan mwanaume unachezwa na tumbo? SERIOUSLY?
 
Pamoja na hayo yote uhakikishe unampa ulinzi muda wowote huyo mke wako.

Ulinzi wenyewe siyo kuwa kama baunsa bali uwe financially stable. Muda wote akihitaji pesa ipo. Hakikisha hajui stress ni kitu gani.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] yaani akiyaacha yoote akasema hilo tu kila siku, huchoki kumsikiliza
Kwanza kila akiongea/andika unajikuta unafall in love zaidi na zaidi
 
Wanawake hawatabiriki hata kidogo kuna yule anaempa pesa penzi linanoga na kumpa hadi gali ila anakuja namjazia upepo kwenye tairi anamega kisera na pesa anapewa mwanaume mjaza upepo ukiliza kwanini kafanya hivi unambiwa shakaji yule mwenye pesa hayupo romantic ila huyu kapuku akianza kuzungumza haya demu utamsia wanataka pesa sio maneno hawa viumbe ni hatari kama wametoka sayari ya 5
 
Back
Top Bottom