Mambo ambayo hutakiwi kuchelewa kwenye maisha kama tayari una mpango wa kufanya jambo husika

Ila pombe inamahusiano makubwa na kizungu mkuu😅
Kaka inategemea mtu na mtu .
Mimi tukikutana Kama Sijalewa kiukweli maneno yangu mengi nachanganya kingereza Ila uwa nikilewa naanza kuhisi aibu kuongea kingereza hata kwa kuchanganya .

Sema hili ni kwasababu ya viumbe ninaolewa nao .
Huwezi amini Mimi ndiye naonekana mtu wa maana nikiwa na hawa wazee
 
Hapo tupo tofauti mimi nikishakua na kilevi kichwani huwa ndio nina kua smart zaidi hata watu wangu wa karibu wanapenda niwe hivyo ila nikiwa mzima naonaga kila mtu anazingua na hayupo makini nakuwa kama mnoko flani hivi😁😁😁😁
 
Ushauri ni mzuri ila sio katika mazingira ya dunia ya huku mavumbini(Tz)hasa katika kipindi hiki cha ukosefu mkubwa wa ajira.

Vijana wengi wanafika mpaka miaka 30 bado hawajaona mwanga au ndo kwanza kunaanza kukucha yamkini ushauri kama huu utazidi kuwatia STRESS na KUWAFANYA KUPOTEZA FOCUS.

Vijana mnaojitafuta mitazamo kama hii ni bora mkaiacha kama ilivyo. Afya ya akili ni muhimu sana....Depression is real!!!
 
Miaka inavyozidi kwenda mtibeli unazidi kupoteza focus,,,,umekuwa mediocore siku za hivi karibuni!!!!

Mwanachuo ambaye ni tegemezi, huyu mwanafunzi ambaye hana uwakika hata wa kupata kazi baada ya kuhitimu unamshauri aoe akiwa chuo. Embu kuwa realistic.

Msiwapeleke resi hawa vijana wa elfu mbili,hiki kipindi chao maisha yamekaza sana.,,,,zamani ukimaliza hata form six unapata hata kazi ya ukarani lakini saivi watu wanamasters na wanakosa hata sehemu ya kujitolea.

Washaurini vijana vitu kulingana na era yao. Hizi motivation speeches tusizikopi huko mitandaoni na kuzihamishia kwenye maisha halisi,tujitaidi kuhusianisha na mazingira yetu halisi kabla ya kuzitia katika utekelezaji.
Hiyo miaka 25/26 ya MD alianza shule Akiwa na Miaka 10 au?

Watu wanaoa wakiwa Chuo
 
Strong point
 
Kujenga na kuwa na makazi inaingia kwenye no. 2 au?
 
Ningekuwa sijawahi kufika Chuo labda ungeongea hayo.
Uhakika wa Kupata Kazi upo ila kupata ajira ndio haupo.
Msiwapeleke resi hawa vijana wa elfu mbili,hiki kipindi chao maisha yamekaza sana.,,,,zamani ukimaliza hata form six unapata hata kazi ya ukarani lakini saivi watu wanamasters na wanakosa hata sehemu ya kujitolea.
Zamani maisha yalikuwa magumu kuliko sasa.
Kadiri siku ziendavyo mambo ndio yanarahisishwa.

Kwa nini wajitolee?

Washaurini vijana vitu kulingana na era yao. Hizi motivation speeches tusizikopi huko mitandaoni na kuzihamishia kwenye maisha halisi,tujitaidi kuhusianisha na mazingira yetu halisi kabla ya kuzitia katika utekelezaji.

Mimi nazungumzia maisha halisi sizungumzii ndoto za abunuasi walizonazo wanafunzi wakiwa shuleni ambao wakifika mtaani huona uhalisia

Ninachoongea ndio uhalisia wenyewe.

Umemaliza chuo na Miaka 23-25 mbona ni Muda mzuri kama kijana kujua nini ufanye
 
Ushauri ni mzuri ila sio katika mazingira ya dunia ya huku mavumbini(Tz)hasa katika kipindi hiki cha ukosefu mkubwa wa ajira.
Kazi zipo ila za kuajiriwa ni chache.
Ukichagua Kazi alafu kijana maskini ndio mwanzo wa kuona Giza maishani mwako.

Vijana wengi wanafika mpaka miaka 30 bado hawajaona mwanga au ndo kwanza kunaanza kukucha yamkini ushauri kama huu utazidi kuwatia STRESS na KUWAFANYA KUPOTEZA FOCUS.
Bora wapate Stress mapema kabla hawajachelewa watachukua hatua kuliko wapate Stress wakiwa wamechelewa

Vijana mnaojitafuta mitazamo kama hii ni bora mkaiacha kama ilivyo. Afya ya akili ni muhimu sana....Depression is real!!!

Ukikariri huko shuleni hayo ndio MATOKEO.
 
Nilichojifunza mimi in real life ni kutochelewa kuoa.

Oa mapema.

Kwenye Jambo lolote ukiwahi unajiweka kwenye nafasi nzuri kuliko kuchelewa.

Kadiri unavyochelewa ndivyo unavyotengeneza mazingira ya kuanguka/kushindwa
 
Namshukru Mungu
Kwa umri wangu miaka 32
Nimefanya fujo nyingi ambazo zingine najuta na nyingine ni mafunzo
Nimefanya mengi, watoto ninao, mali kidogo zipo Pamba napambana Nina uhakika nitaacha legacy hapa duniani
 
Mungu akuongoze mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…