Mambo ambayo kijana wa sasa unatakiwa kuwa makini nayo sana

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
2,010
Reaction score
4,179
BD65EEAD-C97A-42A0-9484-DD14BBE2B058.jpeg

1. Epuka na ujitoe kabisa kutoka katika Kundi la watu wenye mitazamo hafifu juu ya maisha yao.

2. Acha kuwa king'ang'anizi kwa wale waliokutenga katika maisha yako.

3. Kuwa mtu wa haki na upendo hata kwa watu usiowajua.

4. Kuwa mtu wa heshima na upendo kwa kila mtu.

5. Kubali kuishi na watu kwa jinsi walivyo na sio wewe utakavyo.

6. Wahamasishe wenzio kufanya mambo yenye mafanikio na furahia mafanikio yao bila unafiki.

7. Kuwa mtu wa kuaminika kwa kila ukifanyacho.

8. Samehe watu na endelea na maisha yako bila kuwafikiria tena.

9. Kila siku fanya kitu kidogo kizuri kwa watu wakuzungukao.

10. Kuwa makini na mwangalifu kwa hao unaowaita marafiki.

11. Daima kuwa mkweli.

12. Wasialiana na kuwa karibu na watu unaowajali katika maisha.

13. Kuwa mtu wa kitimiza ahadi zako na kuwa mkweli.

14. Toa kitu ambapo nawe unatarajia upokee.

15. Sema unachomaanisha na maanisha unachosema.

16. Uwe mtu wa kukubali na wengine watoe maamuzi.

17. Ongea kidogo na kuwa makini katika kusikiliza.

18. Usiwe mtu wa mabishano kila mara yasiyo na tija.

19. Achana na umbea au maneno yanayoweza kuja kukunyima furaha.

20. Uwe makini na mahusiano yako mwenyewe na mahusiano yako na MUNGU.
 
Tunakumbushana nini na kipi haswa tunahitajika kuwa makini kipindi hiki cha kubadili namba ya mwaka, Ili tuitue mizigo mingi na kuwa huru mwaka ujao...

Nikutakie Kheri ya mwaka mpya na fanaka tele maishani mwako...
 
Maisha hayana formula wapendwa ila maneno ya kujifurahisha yapo
Maisha hufuata taratibu zako ulizojiwekea na matarajio unayohitaji kwa kipindi ulichopanga, Huwezi kwenda hovyo kama kuku aliekatwa kichwa ukafanikiwa ila ni kwa utaratibu tu na kumtanguliza mungu mbele utafanikiwa hivyo basi maisha yana formular.. na wewe ndie mlinganyo wenyewe unaepaswa kufungua vifungo vya njia sahihi maishani mwako.
 
Mimi sio Mungu nifanye yote hayoo ...

Hii duni ya fujo na makasiriko nianze kunyenyekea kila kitu ....
Ishi kwa misingi yako yenye kujiheshimu basi pasi na shaka utaheshimika na huto nyenyekea binadamu mwenzio kamwe...
 
View attachment 2463276
1. Epuka na ujitoe kabisa kutoka katika Kundi la watu wenye mitazamo hafifu juu ya maisha yao.

2. Acha kuwa king'ang'anizi kwa wale waliokutenga katika maisha yako.

3. Kuwa mtu wa haki na upendo hata kwa watu usiowajua.

4. Kuwa mtu wa heshima na upendo kwa kila mtu.

5. Kubali kuishi na watu kwa jinsi walivyo na sio wewe utakavyo.

6. Wahamasishe wenzio kufanya mambo yenye mafanikio na furahia mafanikio yao bila unafiki.

7. Kuwa mtu wa kuaminika kwa kila ukifanyacho.

8. Samehe watu na endelea na maisha yako bila kuwafikiria tena.

9. Kila siku fanya kitu kidogo kizuri kwa watu wakuzungukao.

10. Kuwa makini na mwangalifu kwa hao unaowaita marafiki.

11. Daima kuwa mkweli.

12. Wasialiana na kuwa karibu na watu unaowajali katika maisha.

13. Kuwa mtu wa kitimiza ahadi zako na kuwa mkweli.

14. Toa kitu ambapo nawe unatarajia upokee.

15. Sema unachomaanisha na maanisha unachosema.

16. Uwe mtu wa kukubali na wengine watoe maamuzi.

17. Ongea kidogo na kuwa makini katika kusikiliza.

18. Usiwe mtu wa mabishano kila mara yasiyo na tija.

19. Achana na umbea au maneno yanayoweza kuja kukunyima furaha.

20. Uwe makini na mahusiano yako mwenyewe na mahusiano yako na MUNGU.

Namba 11 ukiwa mkweli maisha haya hutoboi kwenye maeneo mengi sana.

Maisha ya sasa yanataka uwe muongo muongo, mnafki, maneno mengi, nk..
 
Kwani wewe umekua dalali hadi uwena porojo za namna hiyo😂😂
 
Back
Top Bottom