Mambo ambayo mzazi au mlezi anatakiwa kuzingatia pindi mtoto akiwa likizo

Mambo ambayo mzazi au mlezi anatakiwa kuzingatia pindi mtoto akiwa likizo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kipindi hiki watoto wamerudi nyumbani au kutokwenda shule kutokana na uwepo wa likizo, ni vizuri wazazi kuzingatia haya:

1. Jipe muda wa kuzungumza na mtoto kila siku.

2. Muulizie juu ya changamoto alizokutana nazo akiwa shule.

3. Kagua vitu anavyovitizama kama picha, simu.

4. Jadiliana naye kuhusu matokeo yake ya mwaka mzima.

5. Kuwa makini sana na aina ya marafiki anaokuwa nao, ikiwezekana angalia background ya familia za marafiki zake.

6. Mpe muda wa kwenda kwa wazazi wa pande mbili ajifunze mahusiano na familia.

7. Hakikisha anapata muda wa kiroho kushiriki ibada na pia kusali pamoja.

8. Usimpe kila anachotaka, mpe kwa sababu ni muhimu.

9. Usimdekeze, afanye kazi za mikono hata kama una dada au kaka kazi aoshe vyombo, asafishe nyumba, atandike chumba chake, afue nguo mwenyewe na hata kuhudumia kazi za uzalishaji hapo nyumbani.

10. Epukeni magomvi ya mara kwa mara yatakayomfanya aathirike kisaikolojia.

11. Kama mmeachana na mzazi mwenzako hakikisha mtoto anapata nafasi ya kumsalimia mzazi mwenzako.

12. Usiruhusu mtoto kushinda peke yake chumbani akicheza game, mpe nafasi ya kusociliaze lakini kuwe na mipaka.

13. Kama kuna kazi za kijamii kama kutembelea yatima mpe muda afanye charity work, itampa tabia ya kujali wengine.

14. Epuka sana kuonyesha kuwa unamuogopa na analosema utatekeleza, mahali fulani lazima kuwa strictly.

15. Mpangie revision kwa kiwango Ili akili ipumzike.

16. Anza kujadiliana naye kipawa chake na ndoto zako.

17. Mueleze changamoto zilizopo kama magonjwa na tabia hatarishi.

18. Mfundishe unyenyekevu na kuheshimu wengine.

19. Mtie moyo ukimjengea uwezo wa kuwa anaweza.

20. Jadiliana naye hali ya uchumi ilivyo katika familia, ajue katika maisha kuna up and down na mfundishe umuhimu wa kushare changamoto alizonazo.
 
Umezungukaaaa wee na kupangaa kote hoja zako, ila lengo ni hiyo No 17, na umeandika kwa herufi kubwaaa kuonesha mkazo.

Mtoto akiamua kuwa shogaa anakua tyuuh hata afanyiwe zaidi ya hayo uliyotajaaaa. Poleeeeeeeeh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakishua hao. Huku usukumani wanashinda shambani na kuhudumia mifugo. Matokeo yao namba 5 huwa hawavuki kwa wastani wa 241 kati ya 250
 
Back
Top Bottom