Mambo ambayo Yanafanya watu wengi waweke Fikra kwamba huenda dunia ni simulation au huenda hatuna free wills kama tunavyoambiwa case st JFK &Lincoln

Mambo ambayo Yanafanya watu wengi waweke Fikra kwamba huenda dunia ni simulation au huenda hatuna free wills kama tunavyoambiwa case st JFK &Lincoln

a CONFESSION
of a MAD PHILOSOPHER

MAANA YA UHURU,HUISHA BAADA YA UTAMBUZI,
BAADA YA KUTAMBUA,KWAMBA UHURU SI MAAMUZI,
MAANA KIFUNGO NA MIPAKA VINAFANANA,
ALIYEKUAMBIA KUNA UHURU, UTAUPATA KAKUDANGANYA,

IPO ASILI INAYOFANYA,MWILI WAKO MASHINE,
KUFANYA UGONJWA UWE JELA, ALAFU AFYA NI JELA NYINGINE,

MJAMAA AMEMWAGA DAMU TAYARI,
AwE HURU ILI AKAWE, MTUMWA KWA MABEPARI
CHAGUA KUFA UKIONA WAJA, HAWALIPI WEMA,
KUFA WOKOVU KILICHOKUFA HAKIFI TENА,
KUFA NI UHURU KAMILI TABU NI NINI?
HAUPO HURU SASA

UHURU WA KWELI NI KABURINI

UÑAKUMBATIA UHURU
WA KUAMBIWA

WAKATI UNAISHI
NA HAUKUCHAGUA KUZALIWA

UHURU HAUTAFUTWI
MSAFIRI, PUMZIKA KUBALI
CHАI

HAUWEZI KUWA HURU
UNGALI HAI

UHURU SI HALISI JAMAA
BADILI UMBO

UHURU SIOJIBU HATA
USIKARIRI FUMBO

UHURU NI FALSAFA
YA VITABU, ILIANDIKWA
NA MABABU

TUTAISOMA NA MWISHO ITABAKI HUKO

ANAYE HITAJI UHURU
AELEWE..

KUOGOPA KUFA NI UTUMWA
KWA MAANA KUFA

NDIO UHURU WENYEWE

HATA UWE MFALME AMBAYE
ANATOA IDHINI

HUWEZI KUWA HURU
UHURU WA KWELI NI KABURINI

××××××××××××××××××

UKIKUMBATIA MWANGA
JUA UTAIFICHA NURU

UHURU SI KWA MWAFRIKA
KUMKIMBIZA MKABURU

KUUTAKA UHURU SANAJAMAA
SI DALILI NJEMA

KA' UPO HAI NA
UNAHISI UKO HURU
FIKIRI TENA

CHEO HULETA NURU
PAHALA NURU HAIPITI

NA PESA NDIO NJIA
YA UHURU UKIIMILIKI

PESA NA CHEO HUPITA
КОТE HAКUINGIIKI

ALISEMA MLEVI MMOJA
AMBAYE POMBE TU
IMEMDHIBITIІ

MWATHIRIKA AMBAYE DAWa
ZA KULEVYA ZIMEMFUNGA

NA ANAHISI YUKO HURU
MARA BAADA TU YA KUVUTA

LABDA SI KWELI
HAUPO HURU UKIJIONGEZA

MAANA UKISHAUJUA UHURU
TAYARI USHAUPOTEZA

JE UTANIONA CHIZI AU MWIVI
AMA MSHENZI AU PUMBAVU
NINAYEONGEA VITUKO

AU UTAAMUA KUKAA
CHINI UTAFAKARI
KISHA UKAKUBALI

NDOA, AJIRA
NAVYO PIA VIFUNGO

ALIYE HURU NI NANI
NIELEZE

MTOTO ANAYEENDA
KWА VIBOKO?

AU MLOKOLE MTENDA MEMA
BAADA YA KUTISHIWA MOTO

AU MSOMI AMBAYE ELIMU
МРАКА СНUО КІНАКІКІ
I SWEAR...

KAMA UHURU NDIO HUO
SIUAFIKI

ANAYEHISI YUKO HURU
PITA MBELE

PIGA KELELE

HATA MUNGU WAKO
BADO HAYUKO HURU

HAWEZI KUBADILI MIPANGO

HAWEZI KUMUUMBA
MUNGU MWINGINE

MKUBWA KUPITA YEYE

UNAYETAFUTA UHURU
WA KWELI UTATESEKA

UTAPOTEZA DAMU

UTATOA MACHOZI
NA UTAKESHA

HAUWEZI KUUPATA
MAANA HAKUNA ULIPOUWEKA

UHURU HAUPATIKANI KWA
FEDHA

UHURU IS PRICELESS

KWAKUWA SI BIDHAA
HALISI

WENYE CHAPAA WALIHAKIKI

UTANIANGUSHA SANA
UKISHINDWA KUAMINI

UPO UHURU ILA
UHURU WA KWELI
NI KABURINI

View attachment 2855237
Huyu Dogo anaandika Sana na Mimi Ni shabiki yake pia.

Ameandika na kuviongea vitu fikirishi Sana Dizasta Vina
 
Swali zuri. Nilivyosoma tu mada ndilo swali lililokuja kichwani.
HIli nimelijibu kuwa kitu kinachowapa upekee ni kwamba hawakuwa Raia wa kawaida tu walikuwa Ni Marais wa Marekani

Nakupa Ruksa niletee marais wote Dunia nzima wwnye mfanano huo
 
Huyu Dogo anaandika Sana na Mimi Ni shabiki yake pia.

Ameandika na kuviongea vitu fikirishi Sana Dizasta Vina
Namkubali sana jmaa Kuna moja mpya katoa Haina wiki nyingi sana inaitwa wachezaji wa Timu

huyu jamaa ni Narrative Lyrical God..Nimeanza kumsikiliza Tangu 2021 na sijajuta kumjua Ni philisophical Brain
 
Ndivyo wanavyofanya illuminati, unapewa neno lililopinduliwa Ili kudanganya.

Majina yote mazuri ni ya Yesu, ndiye Mungu,

Ikiwa zipo nyota zenye kung'aa, basi yenye kung'aa kuliko zote ni Yesu,

Mama jusi waliiona nyota ambayo haijawahi onekana tangu Kuumbwa Ulimwengu, na wakati huo shetani akiwa kuzimu,

Sasa iweje Yesu awe huyo?

Yesu Anaitwa Mfalme wa Amani, Baba wa Milele, Mfalme wa Wafalme,Mungu mwenye nguvu.
Mkuu mbona unapinga jumla jumla bila kujishughulisha na mjadala husika?
Je tukisema wewe ni muongo kwasababu unaandika yanayotoka kwenye fikra yako tutakuwa tunakosea?
DR Mambo Jambo anatupa maelezo yaliyoshiba na rejea za vitabu mbalimbali wewe unaweka porojo.
 
Tupe na ya Yesu nayo maana kuna wadau wanasema simulation yake yule aliembebea msalaba ndie aliesulubiwa Ila yeye mwenyewe alijichanganya na umati akaingia mitini ili kuikwepa misumali
Unamsemea simon mkrene ww
Au sio mkuu?!
 
Attachments

  • 20240102_160027.jpg
    20240102_160027.jpg
    1.4 MB · Views: 8
Mkuu hii swali ni pana sana Na Ni swali ambalo hata ukiandika Majibu Yanaweza kuchukua Page 400s kuelezea Kwa sababu maaelezo yake ni kitabu kabisa..

Maana linahusisha mpaka Astrology na numerological literacy Na Pia kwa wale watu wa Theology watahusisha Judeo-Christian Metaphor na symbolism...
Ni wide sana kulielewa kwa mara Moja its All been metaphor since then na sio Literal kwamba kuna simba Wakaitwa hayo majina...

kwa kifupi

Najua unakoQuote ni hapa..

Kwa yesu kama Simba..

Ufunuo wa Yohana 5:5

"Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba."

Kwa Shetani kama Simba..

1 Petro 5:8

Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

Kabla sijakujibu nataka kukuchanganya zaidi na Gospel of thomas verse 7

Gospel of Thomas Verse 7🙁Injili ya Thomas aya ya 7)

"Jesus said, 'Blessed is the lion which becomes man when consumed by man; and cursed is the man whom the lion consumes, and the lion becomes man.'"

Sijui umenielewa?

Tuanze na Theological part ambayo ni simple kuidigest..

in biblical symbolism na metaphor. Kwenye Christian theology, kama nilivyoonyesha hapo kuwa Yesu katoka katoka kabila la yuda, so This symbolism comes from Biblia agano la kale Ambalo linamtaja Yuda kama Simba au Mwana simba (Mwanzo 49:9).

Kwahiyo simba anachorwa symbolically kimaana, Kwa kuonyesha strength, majesty, and kingship.

kwahyo Kumuita Yesu Simba kunaonyesha his royal and powerful nature.

Na shetani pia Ni simba kwa kigezo hicho hicho.

kama unakumbuka alipombeba yesu na kumuonyesha Falme zote za Duniani na kumwambia atampa..
Means ni zake pia...

na hiyo ndo context ya Judeo-Christian tradition.

Sasa Majibu upande wa astrological and numerological aspects kwa kifupi sana

Lion= Symbolysed by Leo
Which ruled By Sun (Jua)..(+1,-4)
Numerologically lion ruled by Number 1 (Positive +1)..
And number 4 (Negative Character -4)
Kwa watu wa Numerology mpaka hapa tayri.

Wameshanielewa tena sana..

Namba 4 (-4) ni number of dealth japo +4 ni namba ya birth..

Japo kwa ujumla namba 4 ni namba ya Dealth and Rebirth...

Hapo umenielewa?

Kwahyo The consuming Lion take -4
And the Lion of Juda take +1

Sasa kabla hatujaendelea unajua kwanini Yesu ametoka katika ukoo wa Yuda na anajiita Simba wa Yuda na Cha ajabu jina la mwanafunzi wake Yuda ndiyo aliemsaliti?

Yuda ni mtoto wa nne kuzaliwa kwa Yakobo..
Namba nne which symblolise Dealth and rebirth..

That means ili something crucial to be born it must follow the rules of number..

Turudi kwenye Simba sasa..

Kwahyo wote ni Moto elementary (Ruled by Fire)

Kibiblia..

Unakumbuka hapa..

Amosi 2:5

"Lakini nitapeleka moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu."

Ilitimia hapa..

Luka 12:49

"Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi? "

Ufunuo wa Yohana 19:12

"Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe."

Ufunuo wa Yohana 2:18

"Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.;"

Waebrania 12:29

"maana Mungu wetu ni moto ulao."

Vipi kuhusu shetani?

Ezekieli 28:14

"Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto."

Au umesahau aliumbwa kwa moto...

Waebrania 1:7

"Na kwa habari za malaika asema,
Afanyaye malaika wake kuwa pepo,
Na watumishi wake (Cherub) kuwa miali ya moto."

Sasa nina imani umepata Those two sides by the way namba 1 huwa ni namba ya Utawala ila namba nne hasi ni namba ya Adversary (Yaani Kupinga au kinyume )..

Kuna mengi sana ya kuongea kuhusu Haya mambo lakini Ni Magumu sana kuyapokea..
So conclusiom ni kwamba hapo kilikuwa kimazungumziwa Two Duality With the same Power Which can be traped a person..
Rejea Gospel of thomas Aya ya 7

Na ndo maana unaona wote wako katika Same Signs ambayo ni sun na ndo nyota yenye nguvu..
Dr uko very deep, natamani sana kujua vzr haya mambo unaweza kunisaidia pa kuanzia 🙏
 
Kama shetani anaweza Kuwa mungu, unataka kumaanisha mungu ndio shetani
kweni Shetani kaumbwa na nan?
Alafu evils spirit haziwakilishi giza bali giza ni sehemu tu ya ulimwengu in nature.
True creator of everything hes both dark and light( creation and destruction is perfection or the perfection of the system it is its imperfection(stefano from gaia).

Nilipenda movie ya marvel the Endgame character ya thanos iliwashinda, yale mawe au spirits stones mungu yehova anazo 7

Mungu Yehova ana nafsi saba ukitoa ya yake zinabaki sita maana yake akipoteza moja kati ya nafsi hizo ni shida na hawez kupoteza.
Lucifer kuna kitu anabeba kutoka mbinguni Wajuzi wanaita funguo bali ni code tu, Mungu alikiitaji hicho kwa gharama yoyote so kumtoa mwanae sio kwajili ya watu tu pia na Funguo
 
HIyo Movie inaitwaje mkuu..
Naona kama nimeipenda mandhari yake..
Maana ni kweli Yehova ana 7 spirit ambazo ndo wakristo huiita Seven Arch angel..
Hebu fanya kunipa jina
 
kweni Shetani kaumbwa na nan?
Alafu evils spirit haziwakilishi giza bali giza ni sehemu tu ya ulimwengu in nature.
True creator of everything hes both dark and light( creation and destruction is perfection or the perfection of the system it is its imperfection(stefano from gaia).

Nilipenda movie ya marvel the Endgame character ya thanos iliwashinda, yale mawe au spirits stones mungu yehova anazo 7

Mungu Yehova ana nafsi saba ukitoa ya yake zinabaki sita maana yake akipoteza moja kati ya nafsi hizo ni shida na hawez kupoteza.
Lucifer kuna kitu anabeba kutoka mbinguni Wajuzi wanaita funguo bali ni code tu, Mungu alikiitaji hicho kwa gharama yoyote so kumtoa mwanae sio kwajili ya watu tu pia na Funguo
Kwa hiyo Lucifer kamuibia mungu kitu chako
 
kitu changu? uliondoka nafunguo toka mbinguni na kasha pukonywa na kristo miaka mingi
Nilikuwa namaanisha Lucifer alitoroka na funguo za Mungu, baadaye kabisa yesu akazurudisha .

Hizo funguo ni codes AU ni funguo za kawaida , na hizo funguo Zina Kazi Gani mpaka Lucifer atokomee naz
 
Dah kuna sehemu nafeli ukiona had robot zinaanza kujioji nani kawatengeneza ni moja ya kujitambua ila haiwez mfanya mtengezaji akasquiz hahaha
 
Nilikuwa namaanisha Lucifer alitoroka na funguo za Mungu, baadaye kabisa yesu akazurudisha .

Hizo funguo ni codes AU ni funguo za kawaida , na hizo funguo Zina Kazi Gani mpaka Lucifer atokomee naz
Inasemekana ni funguo, yani mamlaka ya kuzimu na mauti, sasa wenda kiwakilish chake ni kitu halisi ndo maana kikaitwa funguo
 
Back
Top Bottom