Mambo gani ya fedheha umewahi kufanya kwasababu ya kufulia (kukosa Hela)?

Mambo gani ya fedheha umewahi kufanya kwasababu ya kufulia (kukosa Hela)?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Pesa ni muhimu aisee, pesa hainunui Kila kitu ila inakamilisha mambo mengi sana, ikose ujue namaanisha nini.

Nakumbuka kuna kipindi nlikuwa sina pesa nlikuwa nashindia kiazi utamu kilichochomwa, nashushia maji ya bombani, hicho kiazi ndio msosi wa siku nzima.

Nimewahi kukaa na chaja ya kutegesha kwa zaidi ya mwezi, yani inabidi utegeshe kwa ustadi, ikafika kipindi inabidi niiviringishe ule waya kwa mtindo maalum, ikafika kipindi inabidi niibane kwa kuingata na meno Ili ibane vizuri kwenye simu.

Kuna kipindi nlikuwa mvutaji wa sigara (saizi nmeacha) nlikuwa navuta nusu, siimalizi yote, inayobaki naitunza navuta baadae, kumbuka sigara ya spoti ni 200 tu.
 
Back
Top Bottom