Home hamna kitu na Nina Moto na mke jioni nikapata jero nikanunua vidagaa SASA inshu ikaja gas imeisha, mkaa hakuna SASA alternative ni kupika kuni hapo kuni nazo sjui napata wapi. Hapo ni Saa mbili usku mchana na asubuhi sjala Ila mtoto alikologewa uji Tu.
Basi wakati narudi home na kmfuko changu cha dagaa nikapita mahali nikaona limeza lipo road nikaona linafaa Kwa kuni nikabeba huyooo daaah mara nakutana na jamaa mmoja akanisimamisha akanambia meza Ile ni yake na mjomba ake huwa wanafanyia biashara kwaiyo Mimi ni mwizi akampigia simu HUYO mjomba wake kumpa taarifa ya wizi Yule mjomba wake akamwambia tukutane pale nilipoichukua Ile meza kweli tukarudi mpk pale halafu ni barabarani nashukuru kulikuwa na kagiza basi tumesubiri were Yule mjomba mtu akapiga simu nikapewa niongee naye akawa ananiambia niseme Mimi ni mwizi au nipelekwe polisi bs nikakili ndivyo nimeiba bs ye akasema kapata emergency kwahiyo hiyo meza ipelekwe kwake nikabebeshwa tena mpk Kwa HUYO mjomba wake kesi ikawa imeisha yaani stasahau sema ni zamani sana