Mambo makubwa aliyofanya Rais Samia kwenye sekta ya kilimo

Irene Darton

Member
Joined
Feb 25, 2024
Posts
18
Reaction score
22
Kwenye Sekta ya Kilimo Serikali ya Rais Samia imeongeza bajeti ya Kilimo kutoka Tsh. 751 mwaka 2022 hadi Tsh. bilioni 970.

Kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula Tani 17,148,290 hadi kufikia Tani 20,402,014 na kufikisha asilimia 124 ya kiwango cha utoshelevu wa chakula.

Ameipatia wakala wa uhifadhi wa chakula NFRA na bodi na nafaka na mazao mchanganyiko (CPB) kiasi cha Tsh. bilioni 116.

Ametoa ruzuku ya mbolea ya tani 204,818.16 kwa mikoa yote ya Tanzania yenye thamani ya Tsh. bilioni 67.82.

Serikali yake imetenga jumla ya eneo lenye ukubwa wa ekari 201,241 kwa ajili kuwaingiza vijana na wanawake kwenye kilimo kupitia mradi wa BBT

Serikali yake imeendelea kuwekeza katika Skimu za Umwagiliaji kwa kuongeza eneo kutoka hekta 727,000 hadi hekta 822,000.
 
Hakuna hata kimoja kilichomsaidia mkulima hapo angefanya yafuatayo.

Angeshusha pembejeo za kilimo kwa kutengeneza viwanda vya pembejeo hapahap nchini ningehakikisha mazao ya kilimo yana masoko ya uhakika hasa nje ya mipaka.

Mengine wangefanya wakulima wenyewe, ndugu chawa wa mama mkulima anaitaji kitu kimoja tu soko la uhakika hvy vingine ni upumbavu.
 
Hivyo vitu miaka yote yanazungumzwa kwa maraisi wote hata kikwete alikuja na kilimo kwanza hakuna kilichowahi kumkwamua mkulima akaondoka kwenye jembe la mkono mtampa sifa pesa zimeliwa na wajanja mnatangaza nadharia zilizo telekezwa ofisini kwenye makabrasha field hakuna kinachoonekana!
 
View: https://www.instagram.com/p/C9pib6kKQu3/?igsh=MTZmczJsbzZ3aDloZA==
 
Hakuna hata kimoja kilichomsaidia mkulima hapo angefanya yafuatayo.

Angeshusha pembejeo za kilimo kwa kutengeneza viwanda vya pembejeo hapahap nchini ningehakikisha mazao ya kilimo yana masoko ya uhakika hasa nje ya mipaka.

Mengine wangefanya wakulima wenyewe, ndugu chawa wa mama mkulima anaitaji kitu kimoja tu soko la uhakika hvy vingine ni upumbavu.
Soko/bei ni changamoto sana, kuna watu kati hapo wameachiwa wawanyonye wakulima bila huruma yoyote. BBT ni miongoni mwa miradi ambayo haitokuja kuleta tija kamwe zaidi ya kuwa sehemu ya wapigaji hapo wizarani. Waziri wa kilimo ni mtu janja janja na hakuna impact atakuaja kuacha hapo wizarani, bahati nzuri ni mwana mpendwa wa mama house.
 
Hivyo vitu miaka yote yanazungumzwa kwa maraisi wote hata kikwete alikuja na kilimo kwanza hakuna kilichowahi kumkwamua mkulima akaondoka kwenye jembe la mkono mtampa sifa pesa zimeliwa na wajanja mnatangaza nadharia zilizo telekezwa ofisini kwenye makabrasha field hakuna kinachoonekana!
Ile document ya kilimo kwanza ulikuwa ukiisoma unaona sasa mkulima wa Tanzania anaenda kunufaika na uchumi utabadilika. Kilichotokea ni cha kuhuzunisha na mkulima akaachwa hoe hae huku watu wachache wakiwa wameneemeka na mabilioni kuteketea. Mpaka leo nashindwa kuelewa ni wapi tumekwama kwenye sekta ya kilimo, sekta ambayo ingebadilisha hali ya maisha ya kaya nyingi sana nchi hii.
 
Hao Wakandarasi waliokaa na Bashe ndio waliomnunulia Mama Chopa?
 
Ile document ya kilimo kwanza ulikuwa ukiisoma unaona sasa mkulima wa Tanzania anaenda kunufaika na uchumi utabadilika. Kilichotokea ni cha kuhuzunisha na mkulima akaachwa hoe hae huku watu wachache wakiwa wameneemeka na mabilioni kuteketea. Mpaka leo nashindwa kuelewa ni wapi tumekwama kwenye sekta ya kilimo, sekta ambayo ingebadilisha hali ya maisha ya kaya nyingi sana nchi hii.
Inasikitisha sana.......!
 
Inasikitisha sana.......!
Yaani wanasiasa wameamua kilimo kiwe ni mtaji wao wa kisiasa na si kuwakomboa wakulima. Nayakumbuka sana mahojiano ya balozi wa Misri aliyekuwa anamaliza muda wake hapa nchini, akihojiwa na mwandishi wa gazeti la daily News miaka kadhaa nyuma. Alisema kama Misri ingepata asilimia kumi tu ya vyanzo vya maji vilivyopo hapa Tanzania, ingeliweza kulilisha bara zima la Afrika kwa chakula, ukiachilia mbali ardhi yenye rutuba na hali nzuri ya hewa. Mpaka leo bado tunategemea kilimo cha kujikimu tu.
 
Wanasiasa wa awamu ipi?
 
Ngonjera za kila mwaka hizi, tangu enzi za Kilimo Kwanza ambapo matrekta yakawa yanakopeshwa, ukaja ujenzi wa scheme za umwagiliaji, yote hayaleta neema yoyote.
Hujawaona Wazambia na Wamalawi wamekuja kununuwa mahindi Tanzania?
 
Yaani wanasiasa wameamua kilimo kiwe ni mtaji wao wa kisiasa na si kuwakomboa wakulima. Nayakumbuka sana mahojiano ya balozi wa Misri aliyekuwa anamaliza muda wake hapa nchini, akihojiwa na mwandishi wa gazeti la daily News miaka kadhaa nyuma. Alisema kama Misri ingepata asilimia kumi tu ya vyanzo vya maji vilivyopo hapa Tanzania, ingeliweza kulilisha bara zima la Afrika kwa chakula, ukiachilia mbali ardhi yenye rutuba na hali nzuri ya hewa. Mpaka leo bado tunategemea kilimo cha kujikimu tu.
Tena kama huyu waziri wa awamu ndio kapiga sana pesa halafu wanaleta blah blah nyingi ukipita kwenye nchi nyingine wanavyoendesha kilimo unapata hasira kila ukiona mambo yanavyoendeshwa na hakuna usimamizi wala nia thabiti sababu huo mradi wake wa magumashi hakuna mkulima wa kweli hata mmoja wote walikuwa wa maigizo na kuchukua posho watuonyeshe hata mmoja tu aliyefanikiwa!
 
Back
Top Bottom