Mambo makubwa aliyofanya Rais Samia kwenye sekta ya kilimo

Sokoni mkulima kafa
  • Pamba 1kg tzs 1,300
  • Tumbaku grades 64
Kilimo sio mazao hayo pekee,in fact Serikali imeweka Nguvu kwenye mazao ya chakula ambayo pia yamekuwa ya biashara.

Hizo traditional crops Hazina ishu sana Kwa Sasa japo tumbaku inafanya vizuri
 
Huo mradi wengi waliongea hata walioko wizarani lakini aliamua uendelee. Sasa hivi vyuo vya elimu vya kati vya kilimo (MATI) wana mpango viache kudahili wanafunzi wa stashahada, badala yake viwe vinapokea na kutoa mafunzo kwa wakulima na maafisa ugani, ngoja tuone tija yake.
 
Mkuu hakuna kitu hapo habari ndio imeisha 2026 agenda nyengine mpya hii imefungwa na vishikwambi kwa kila mmoja!
 
Mkulima siku zote ni wa kuumia tu. Anaingiza ghalama shambani, akivuna anaambiwa tumefunga mipaka.
Kuna system moja ya madalali huwa si ielewi na hawa watu hawalipi kodi wala nini. Mkulima akithubutu kupeleka mazao yake sokoni bila kupitia madalali anafanyiwa advertise moja matata hadi mtaji utakata.
 
Kuna tofauti yakuongeza bajeti nakufanya mapinduzi majority ya wakulima wako vile vile for the past three years labda utuambie mkulima amepata nafuu wapi na kwa namna gani shida zao zipo pale pale labda hiyo hela mnaibunya huko kwenye BBT zenu ila wakulima vilio tu na madeni kibao benki
 
Hao wakulima unaowasema wewe wanatakiwa kuhama kutoka Kilimo Cha Kujikimu na kutegemea mvua na kuhamia Kilimo Cha Umwagiliaji,jambo ambalo ndio Serikali inafanya Sasa.

Ni ajabu kudhani hayo mapinduzi yatafanyika ndani ya miaka 2
 
Hao wakulima unaowasema wewe wanatakiwa kuhama kutoka Kilimo Cha Kujikimu na kutegemea mvua na kuhamia Kilimo Cha Umwagiliaji,jambo ambalo ndio Serikali inafanya Sasa.

Ni ajabu kudhani hayo mapinduzi yatafanyika ndani ya miaka 2
Mapinduzi ndio haya yakuamua bei ya mahindi jukwaani?Hivi mnafika kweli huko ground kwa hawa wakulima? Nchi ambayo mazao yakipatikana tu kwa wingi inakua kama laana kwa mkulima mana watapata bei hafifu kabisa, oya Kilimo ndio uti wa Mgongo wa Taifa ndio mana Mwalimu Nyerere alikiweka kwe ye mitaala kutokea primary hakua mjinga, mechanisation bado watu wanatumia jembe la mkono tembelea wakulima zunguka hii nchi sio mnakaa kwenye warsa na report mkadhani ndio kilimo nenda kaone wakulima wenyewe field ndio utaona namna gani hela zinaliwa kwa kuoanga na semina sio kufika ground kuboresha miundombinu, pitia bajeji iliyopita hela iliyotengwa kaa ajili yabumwagiliaji chuuulia scheme zilizopo Mbarali tu huko Mbeya angalia utekelezaji ukoje? Tatizo letu tunafurahia hukisikia namba pale ziiisomwa hakuna anaefuatilia utekelezaji ndio mana usishangae unakuta miradi inatekelezqa chini ya kiwango na usikilizie maajabu
 
Sekta ya Umwagiliaji huioni? Kuna sekta ya Ufugaji wa Samaki wa vizimba nayo huoni? πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://www.instagram.com/reel/C9sK5MRtB1g/?igsh=dXc5c2Fqem14bWEx
View: https://www.instagram.com/reel/C9sRgEiPyIG/?igsh=MXJhaGw0czhhYmhxMA==
 
Tanzania ni ya watanzania na itaendelezwa na wananchi kwa sera na sheria nzuri pamoja na mipango mizuri ya serikali.
Hesabu ya pesa ya moja kwa moja siyo muhimu kama kutoa matokeo ya maendeleo ya wakulima kutoka katika hali duni kuelekea hali bora.
Tunaweza kutoa takwimu au namba halisi za uzalishaji mwaka hadi mwaka kama uthibitisho. Pia ubora wa mazao,.....
Kubeza juhudi za serikali haina maana yoyote, zaidi ni kutoa njia mbadala za kuongeza tija katika uzalishaji na kuboresha hali za wakulima.
 
Turudishe viwanda vya mbolea kana kile Cha tanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…