SoC01 Mambo manne muhimu kwa mwanamke kuijenga amani ndani ya ndoa yake

SoC01 Mambo manne muhimu kwa mwanamke kuijenga amani ndani ya ndoa yake

Stories of Change - 2021 Competition

Asha Hincha

Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
15
Reaction score
18
Salamu,

Kwa ujumla ndoa ni jambo kubwa lenye wigo mpana na mambo mengi ndani yake ambayo si siku moja wala mwaka utatosha kuyaelezea yote.

Hakuna ndoa iliyo kamilika kwa 100% wala binadamu aliye kamilika kwa 100%.

Lakini yapo mambo machache angalau kwa kuyafuata yanaweza kukubadilisha kutoka hali fulani na kuwa bora zaidi.
Kwa uchache, mambo manne muhimu nitayazungumzia hapa yanayo weza kumsaidia hasa mwanamke kwa namna moja ama nyingine kuijenga amani ndani ya ndoa yake.

1. Jiamini kuwa wewe ndiye mke wake hakuna mwingine,

Wanawake wengi wanapokua katika mahusiano au uchumba hujiaminisha zaidi kwamba huyu ndiye mume wangu lakini wanapoingia kwenye ndoa hawajiamini tena, kana kwamba itatokea siku atapata mwanamke mzuri zaidi yangu akaniacha/kuchepuka au labda simridhishi jikoni na maeneo mengine muhimu au hiki na kile.
hajiachii pale anapokuwa na mume wake na vitu kama hivyo.

2. Mjue mume wako hasa kitabia,

Hii itakusaidia kujiepusha na makwazo madogo madogo, kama ni mapungufu yake jifunze kuyaishi (kwa yale yanayo vumilika).

Mfano mwanaume wako si msafi basi wewe ndiyo kutwa nzima kukasirika, kafanya ivi kinakukera, lakini kama umemfahamu yukoje basi yapokee mapungufu yake madogo madogo, na kama yana zungumzika ongea nae lakini cha muhimu jizoeshe kuishi mapungufu ya mwenzio maana hakuna mkamilifu, na mantiki hii hutokaa ukikwazika na vitu vidogo vidogo kutoka kwa mwenza wako.

3. Kuwa muwazi kwa mwenzio

Katika masuala ya malezi ya familia, uchumi, imani ya kidini na mengineyo.

Usiwe na siri nyingi, kama kuna kitu kinakukwaza au matatizo basi zungumza, kama kuna wazo unalo kwaajili ya familia funguka na kadhalika.

Hii inakusaidia kujenga imani na mwenzio lakini inakupa amani ya moyo kwani unakuwa huna mizigo mingi moyoni mwako.

4. Usiwashirikishe watu wengi kwenye masuala yako ndoa

Sio kila kinachotokea ndani una wahabarisha marafiki, ndugu na jamaa wote.

Sio kila kitu unakwenda nje kutaka ushauri hata kwa mambo madogo madogo, mwisho wa siku ukija kuchanganya mashauri ya kila unaye muhadithia lazima upotee.

Kuwa smart katika kutatua na kupanga mambo yahusuyo ndoa yako na waswahili husema miluzi mingi humpoteza mbwa.

SHUKRAN
 
Upvote 3
nasikiliza habari za chanjo za gwajiboy na h.polepole
IMG-20210808-WA0015.jpg
IMG-20210808-WA0004.jpg


Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom