Mambo Manne Muhimu ya kuzingatia kabla ya kuoa au kuolewa

Meneja CoLtd

Senior Member
Joined
Mar 6, 2021
Posts
122
Reaction score
143
Vijana wengi wamekua wakishindwa kuchagua ni binti yupi anafaa kuolewa, hivyo hivyo wanawake nao wameshindwa kutambua ni mwanaume mwenye vigezo vipi anafaa kukubaliwa kuolewa nae.
Mambo mnne muhimu ya kuzingatia kabla haujafanya maamuzi ni;

1. HOFU YA MUNGU (DINI)
Hiki ni kigezo muhimu sana cha kuzingatia, kwani mume au mke mwenye hofu ya mungu kuna asilimia nyingi atakua mkweli na kukupenda kwa dhati kama mafundisho yanavyotaka

2.CHIMBUKO AU ASILI YAO
Unatakiwa kuchunguza historia au asili ya yule unaetaka kuoa au kuolewa nae.
NB: HAPA TUNAANGALIA ASILI NASIO KABILA

3. TABIA NA UZURI WAKE
Ili usije juta kutamani wanawake au wanaume wengine baada ya ndoa inapaswa uoe au kuolewa na mtu mwenye Tabia na uzuri unaoutaka. Hapa msisitizo ni TABIA maana Uzuri na muonekano hubadilika mda na mda.

4. MALI
Mwisho kabisa tutaangalia mali, duniani hamna anayetaka kuishi maisha magumu yeye wala familia yake, sasa kama akitokea mtu mwenye sifa kuu tatu za juu na ana mali (Mwanamme/Mwanamme) Basi huyo ndo mtu sahihi kwako.
 
Hofu ya Mungu haisaidii chochote.

Kufanya makosa ni kawaida kwa binadamu

Halafu unakuja kuongelewa mali, inaonesha kabisa wewe huna hiyo hofu ya mungu
Alafu jambo la mali utakeusitake lipo na ndomaana tunatoa Mahali ya kuolewa ili kulipa jambo umuhimu. Hapa sijamaanisha wasio na mali wasioe lahasha. Kama anavigezo vyengine anaweza kuoa bila shida.
 
Mtu anaoaje/kuolewa kwa vigezo Mkuu?. Kuishi na mtu kama wanandoa hakuhitaji vigezo, bali uwiano wa nguvu.

Anyway bado nipo kwenye kampeni ya KATAA NDOA.
Vigezo lazima, wewe ukiambiwa uoe chizi utakubali? Kama hapaba Basi umetumia kigezo cha kuchagua mwenye Akili timamu
 
Mawazo mazuri, lakini kuna asilimia nyingi mtu mwenye hofu ya mungu kutofanya upumbavu. (Hili litapingwa nawasio na hofu ya mungu)
Shida ya hizo hofu zenu za miungu, ni za kinafki

Mtu akiwa anaenda kanisani ovyo, ni kijana lakini anaongea kama mzee, ananyoa upara, basi ana 'hofu ya mungu'

Oa/kuolewa nae bila kumchunguza uone
 
Mwanaume awe na uwezo kuzidi mwanamke hiyo ndoa itadumu, ila kama mwanaume penda dezo unataka kuoa kwa fulani kisa pesa ipo, hiyo pesa sio yako, mwanaume tafuta pesa yakoooooo ndo heshima yako.
Basi hapo mwanammke atakua hana hofu ya mungu, maana kumsaidia mmeo ni jambo la kawaida tu. Mtu unayempenda utamlinda kwa gharama yoyote
 
Mwanaume awe na uwezo kuzidi mwanamke hiyo ndoa itadumu, ila kama mwanaume penda dezo unataka kuoa kwa fulani kisa pesa ipo, hiyo pesa sio yako, mwanaume tafuta pesa yakoooooo ndo heshima yako.
Wewe ni kausha damu pro max ultra.
 
Shida ya hizo hofu zenu za miungu, ni za kinafki

Mtu akiwa anaenda kanisani ovyo, ni kijana lakini anaongea kama mzee, ananyoa upara, basi ana 'hofu ya mungu'

Oa/kuolewa nae bila kumchunguza uone
Nimekuelewa, basi niseme Mke au Mume awe na hofu ya Mungu ya dhati nasio ya kinafki. Hpo si sawa
 
Mwanaume awe na uwezo kuzidi mwanamke hiyo ndoa itadumu, ila kama mwanaume penda dezo unataka kuoa kwa fulani kisa pesa ipo, hiyo pesa sio yako, mwanaume tafuta pesa yakoooooo ndo heshima yako.
Hata sisi wanaume hatutaki kuoa familia masikini, mambo yamegeuka mkuu dunia haitaki watu tegemezi tena, ndio maana hata nyie hamjabweteka, mpo mnatoka na kupambania kombe kama sisi.
 
Hamna kitu hapo vyote ni dynamic kuna watu kariakoo wanatumika uchawi ambao hawakutoka nao kwenye kabila lao, ukoo wala familia zao
 
Hamna kitu hapo vyote ni dynamic kuna watu kariakoo wanatumika uchawi ambao hawakutoka nao kwenye kabila lao, ukoo wala familia zao
Sasa hapo tunazungumzia tabia, kama anatabia mbaya ya kishirikina usioe au kuolewa nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…