THE FIRST BORN
JF-Expert Member
- Apr 24, 2019
- 2,224
- 4,472
Leo majira ya saa 12 jion kwa saa za Afrika Mashariki kutakua na tukio la kidunia pale Nchini Qatar. Mchezo wa leo utapigwa katika Dimba la Lusail.
Match itakua baina ya Miamba ya Ulaya France dhidi ya Miamba ya Amerika kusini Argentina.
Katika kuelekea Fainali hii yafuatayo ni mambo 5 Ya kusisimua ambayo unatakiwa kuyafahamu Mpenda soka.
1. Ufaransa Imeshinda Michezo mitatu(3) katika match 12 walizokutana na Argentina,
Na Argentina Imeshinda Michezo Miwili(2) katika Michezo Mitatu(3) walizokutana hivi karibuni. Na hii itakua Match ya 4 kukutana katika Mashindano ya Kombe la Dunia.
2. Timu zote mbili zimetwaa hili taji Mara Mbili kila Mmoja.
●Ufaransa imetwaa 1998,2018
●Argentina imetwaa 1978,1986
3. Ufaransa imefika Fainali ya Kombe la Dunia mara nne ambapo imefanya hivo Mwaka 1998, 2006, 2018 na hii ya sasa 2022 na hawajafungwa katika michezo yao 10 ya Mwisho dhidi ya Timu za America kusini katika Mashindano ya Kombe la Dunia.
4. Endapo Argentina itashinda mchezo wa leo, utakua ushindi wa 17 wa Messi katika mashindano ya Kombe la Dunia, hii itamfanya aungane na Mchezaji Miroslav Klose katika wachezaji walioshinda match nyingi katika Mashindano haya.
5. Mchezo wa leo utakua ni Fainali ya 11 ya Kombe la Dunia kuzikutanisha Team kutoka Ulaya na Amerika Kusini, cha kuvutia zaidi team kutoka Amerika Kusini zimeshinda katika Fainali 7 baina ya 10 walizokutana na team za Ulaya.
Je, leo itakuaje? Ni kusubiri na kuona.
#Because I Love This Game